Patrobas Katambi: Tutachunguza clip ya Bodaboda kuvutana na Askari Polisi, haki itatendeka

Patrobas Katambi: Tutachunguza clip ya Bodaboda kuvutana na Askari Polisi, haki itatendeka

KAULI YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, PATROBAS KATAMBI JUU YA MATUKIO MBALIMBALI MITANDAONI NA LA ASKARI NA DEREVA BODABODA LINALOSAMBAA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII,LEO TAREHE 9/8/2026

Ndugu zangu nimeona, nimesikiliza na nimesoma comments;

TUTACHUNGUZA kwa kina na kujua kiini cha tatizo ni nini,kwa video clip fupi hakuna mmoja wetu anaeweza kuamua jambo hili kwa haki.

MSINGI wangu hataonewa mtu wala hatapendelewa mtu ila haki itatendeka, baada ya pande zote kusikilizwa na ushahidi kuchambuliwa kwa hatua stahiki.

Bofya hapa kuona tukio lenyewe ~ Polisi adaiwa kumkodi Bodaboda na kukataa kumlipa baada ya kumzungusha kwa saa 1

SIO HAKI kuhukumu hapo na si haki kuhukumu Jeshi zima kwa tendo la mtu mmoja.Tuwe na uvumilivu tuepuke hukumu za chuki bila kujua ukweli ndugu zangu. Tupost na mengi mema pia🙏🏾

CHUKI isitangulie ukweli na uhalisia ambao sote hatuujui hapo.Tutaamua kwa haki,Mungu atupe uvumilivu Watanzania wenzangu.

PATROBAS KATAMBI,
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Mimi binafsi niliapa askari alievaa sare hawezi kupanda pik pik yangu hawa jamaa wanaroho mbaya sana. Askari kanikamata pale mbagala rangi tatu nimeegesha piki piki yangu pembeni tena sijashuka nanunua parachichi kwa wafanyabiashara ambao wao wamewaruhusu wakae bara barani, ghafla jamaa kanichomolea funguo alafu kanipeleka pale kuna bank siikumbuki jina ila ipo kushoto pale ukitokea mjini kwenye mataa ya rangitatu, basi jamaa kanikomalia anataka elfu 10 au anipige vyeti vitatu, me nikajua masihara nikamuuliza kosa akaniambia kosa langu nimefunga bara bara nasababisha foleni. Duh nikamuomba kwamba anisamehe sikujua kama nimefanya kosa basi achukue elfu 5 jamaa bila kupepesa macho akatoa mkeka wa vyeti viwili. Nilipatwa na mshtuko plus hasira basi na mimi kwa pupa nikalipia ili niondoke. Hapo ndo nikagundua yule polisi alinibambikia mkeka kwa makusudi yaani tayari alikua na mkeka upo pending na huenda labda kuna mtu alimkimbia wakati tayari kashamuandikia cheti ndo maana akawa anamtafuta boya wa kulipa ndo akanipata mimi. Tangu siku hiyo nikaapa askari yeyote hatapanda piki piki yangu tena akiwa amevaa sare au hata nimkute anaungua moto ntamuangalia tu ntamrekodi nimuweke status basi yani siwapendi hawa watu hatar.
 
Back
Top Bottom