Vita tangu inaanza mpaka inaisha Japan hajawahi peleka pua yake kwenye ardhi yoyote ya Marekani alafu unakuja na porojo kuwa wangeshinda. Pearl Harbour iliwezekana kwa kuwa ni ambush hata Tanzania sahivi inaweza jitutumua ikashambulia Misri kwa kuanzia, ila kitakachofuata ndio kingine. Au wewe unaijua ile vita kuliko waandishi wa Japan wote, kama walikuwa wanajua kilichowashinda kushinda vita ni kipi?
Vita sio mpira kwamba refa kawaonea. Wamepigana miaka, Marekani alikuwa na ammunition stockpile mara 40 zaidi ya Japan, anaweza tengeneza meli nyingi zaidi ya zinazoharibiwa na Japan, kazamisha aircraft carriers nne zote za Japan kwenye battle of Midway na kuuza zaidi ya marubani 300 kwa siku hiyo, kazamisha battleships zote kina Mushashi, Yamato na Kuga. Yet hakuna aircraft carrier hata moja ya Marekani ilizamishwa. Marekani kaingia vitani mpaka anamaliza ametoa fighters types nne na Japan anazo Mitsubishi Zero zilezile alizoanza nazo.
Marekani hakushindwa battle yoyote dhidi ya Japan. In fact hao unaosema wanamlaumu Emperor Hiroito kutangaza kuacha vita ndio wanalaumiwa kuanzisha vita, waliona vita ikiisha msako unawafuata kuwakamata kwa war crimes especially in China and South Korea. They were bunch of hooligans, poor mindend people waliodhani wakifanya attack kwenye Pearl Harbor Marekani ataogopa aombe mkataba wa makubaliano. Na ndio haohao walijiua ya kunyongwa kwa war crimes. Walidhani Marekani ni kina Manchuria ya China