MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Rais Paul Kagame alikuwa anaapisha mawaziri wapya hapo jana mapema. Alianza kutoa hotuba yake kwa lugha ya Kinyarwanda, lakini baadae akahamia kwenye lugha ya Kiingereza na baadaye akatoa kitisho kizito kwa lugha ya Kiswahili. Wengi wetu tumeona hicho kipande chenye lugha ya kiswahili kikisambaa huko mitandaoni hasahasa kwa raia wa Tanzania na Kenya. Kitendo cha kusambaa mtandaoni kwa kasi hivi, inaonesha kabisa walengwa wa ujumbe ni watu gani.
Kwenye FASIHI njia moja kuu ya kufikishia ujumbe ni kuifahamu HADHIRA, lakini kubwa zaidi ni kufahamu lugha ambayo HADHIRA hutumia. Siku zote kimetumika Kinyarwanda na Kiingereza, lakini leo hii na Kiswahili juu, tena sehemu ambayo anatoa vitisho. Kwenye Dakika ya 27, ameanza kuwaliza mawaziri wake kama wanafahamu lugha ya kiswahili, wakamjibu wanelewa, ndipo akaanza kuzungumza kiswahili.
Huu ujumbe siyo wa wanyarwanda, wazungumzaji wakubwa wa lugha ya kiswahili wanafahamika, hivyo hicho kitisho ni ujumbe kwenu. Hajataja mhusika, mimi binafsi sitamtaja, lakini naamini walengwa mapema leo, watakuwa washafikiwa na huu ujumbe.
Alichokisema Rais Paul Kagame ni kwamba ukubwa wa pua siyo wingi wa kamasi. Kwamba Rwanda doesn't have the means, but they have the methods (ways). Hivyo kijiografia Rwanda ni nchi ndogo isiyo na rasilimali nyingi, lakini wao siyo migomba mifupi kama wanavyofikiriwa. Binafsi naamini, haivuki miaka miwili (2) kuna mtu kwenye huu ukanda wetu wa maziwa makuu atatoa kilio kikubwa sana.