Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Labda hizo methods apate kwa mabwana zake huko USA na Ulaya na njia kubwa wanayoweza kutumia Ni kuratibu mapinduzi au sumu kwa Viongozi na sio kwenda front hiyo jeuri hawana.
Sasa unamfundisha njia ya kutumia?,nyie mlimfanyaje Magufuli na nchi imewashinda,wewe ni [emoji706][emoji706][emoji706]
 
You are my hero.
Quote Tweet
Muhoozi Kainerugaba
@mkainerugaba
·
Nov 6
As for M23, I think it is very, very dangerous for anybody to fight those brothers of ours. They are NOT terrorists! They are fighting for the rights of Tutsi in DRC.


Je wajua kwa nini Kagame na Museven hawatoki madarakani? Wajua kwa nini wanapigana kule DRC? The answer is said by Museven son!!

..M-23 wanafadhiliwa na Rwanda na Uganda.

..Waasi hao walishapigwa na kufukuzwa Congo na vikosi vya Tanzania, Afrika Kusini, na Malawi.

..Baada ya kupokea kichapo walikimbilia Rwanda na Uganda ambako ilitakiwa wanyang'anywe silaha na wasiruhusiwe kufanya chokochoko dhidi ya Congo.

..Kinachotakiwa kufanyika ni Congo na SADC-FIB kutoa kichapo kikali zaidi ya kile cha mwanzo.
 
tuko busy na uchaguzi 2025.
Huko barabarani tuko busy na maving'ora 24/7 maspeed na kuweka mafoleni, sijui huwa tunawahi wapi na tunawahi nini maana yale ya msingi tunayopaswa kuyafanya hatuyafanyi..

Ruto anapambana kuongeza idadi ya diaspora wakenya duniani, wakati huo anaendeleza utaratibu wa kuzalisha skilled and intelligent workforce ya kenya ili itapakae kila kona duniani..

Tupo busy kubrainwash vijana na kuendelea kuwa chawa wa viongozi, tuko busy kuendelea kuongeza workforce pumbavu inayowaza siasa, tuko busy kufanya vijana wawe tegemezi wa baba zao wezi waliokwenye system.. We paralysized kila mahala na maadui wetu wanafuatilia nyendo zetu kila siku ili siku ikifika watuslave.

Umemaliza kila kitu. Heshima
 
Kagame kama kweli anajiamini kwanini asianzishe hiyo vita anayojitapa kila siku yuko vizuri?

Huku kujisifu kwake kila siku bila vitendo vyovyote pia kunaweza kuwa ni dalili ya mtu asiyejiamini, anajihami tu, ili aachwe aendelee kuharibu amani ya eneo la maziwa makuu.

Huyu anaweza kuwa anaongoza kwa mdomo na ujuaji kuwashinda marais wote wa hili eneo, lakini sio zaidi ya hapo, kama anaona anachokozwa kila siku kwanini asiwafundishe adabu hao wachokozi?
Mara nyingi watu wenye mikwara huwa hawana uwezo wa kupigana. Rejea kipindi cha Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wakati hao M23 walipoteka maeneo ya karibu na Mji wa Goma. Kagame alimtishia Rais wetu Jakaya Kikwete kwenye mkutano wake na Vijana wa Kinyarwanda kuwa atamtwanga (I will hit him), kilichotokea baada ya Tanzania kupeleka Jeshi kule ni M23 wake kuchapwa na akamwomba Rais wa Uganda Mr. Museveni M23 wapate hifadhi kwenye nchi ya Uganda. Maana Rais Kikwete alishaamua kuwafuata M23 nchini Rwanda endapo wangekimbilia huko. Kwa hiyo, hapo anamtishia Kenya ambaye amepeleka majeshi nchini Congo D. R. C.
 
You are my hero.
Quote Tweet
Muhoozi Kainerugaba
@mkainerugaba
·
Nov 6
As for M23, I think it is very, very dangerous for anybody to fight those brothers of ours. They are NOT terrorists! They are fighting for the rights of Tutsi in DRC.


Je wajua kwa nini Kagame na Museven hawatoki madarakani? Wajua kwa nini wanapigana kule DRC? The answer is said by Museven son!!
Africa hii kichefuchefu tu
 
Rais Paul Kagame alikuwa anaapisha mawaziri wapya hapo jana mapema. Alianza kutoa hotuba yake kwa lugha ya Kinyarwanda, lakini baadae akahamia kwenye lugha ya Kiingereza na baadaye akatoa kitisho kizito kwa lugha ya Kiswahili. Wengi wetu tumeona hicho kipande chenye lugha ya kiswahili kikisambaa huko mitandaoni hasahasa kwa raia wa Tanzania na Kenya. Kitendo cha kusambaa mtandaoni kwa kasi hivi, inaonesha kabisa walengwa wa ujumbe ni watu gani.

Kwenye FASIHI njia moja kuu ya kufikishia ujumbe ni kuifahamu HADHIRA, lakini kubwa zaidi ni kufahamu lugha ambayo HADHIRA hutumia. Siku zote kimetumika Kinyarwanda na Kiingereza, lakini leo hii na Kiswahili juu, tena sehemu ambayo anatoa vitisho. Kwenye Dakika ya 27, ameanza kuwaliza mawaziri wake kama wanafahamu lugha ya kiswahili, wakamjibu wanelewa, ndipo akaanza kuzungumza kiswahili.

Huu ujumbe siyo wa wanyarwanda, wazungumzaji wakubwa wa lugha ya kiswahili wanafahamika, hivyo hicho kitisho ni ujumbe kwenu. Hajataja mhusika, mimi binafsi sitamtaja, lakini naamini walengwa mapema leo, watakuwa washafikiwa na huu ujumbe.

Alichokisema Rais Paul Kagame ni kwamba ukubwa wa pua siyo wingi wa kamasi. Kwamba Rwanda doesn't have the means, but they have the methods (ways). Hivyo kijiografia Rwanda ni nchi ndogo isiyo na rasilimali nyingi, lakini wao siyo migomba mifupi kama wanavyofikiriwa. Binafsi naamini, haivuki miaka miwili (2) kuna mtu kwenye huu ukanda wetu wa maziwa makuu atatoa kilio kikubwa sana.
Huyu anazeeka vibaya sasa, anadhani anachokifanya Congo anaweza kukifanya Tanzania? Athubutu aone, aliyekuwa kampanda mabegani hayupo tena
 
Back
Top Bottom