Wacha Bhwanah!. Binafsi naamini, haivuki miaka miwili (2) kuna mtu kwenye huu ukanda wetu wa maziwa makuu atatoa kilio kikubwa sana
Umezungukaweeee, kidogo nijiondokee zangu!
Hakuna kitu hapo mkuu, asipoangalia huu ndio utakuwa mwisho wa Bwana Fito. M23 ni jiwe litakalomwangamiza.
Lakini kinachonifurahisha ni kuona unafiki/utapeli wa baadhi ya mataifa ya ukanda huu wa kujitwisha mzigo kwa jina la Jumuia, halafu wanafanya ghelesha kupeleka jeshi huko eti kulinda maslahi yao (ya nchi yao) kwa mgongo wa Jumuia.
Haya, jeshi linafika eneo la mapambano, hapo hapo hadithi inabadilika, eti wao wamekuja kulinda amani na siyo kuimarisha amani! M23 anawaangalia tu na kucheka.
Nisitoe hadithi ndefu, lakini sasa ni wazi, waCongo wenyewe sasa wameamua, hawataki kuchezewa na hivi vikaragosi na vinyago.
Kinachonipa moyo kwa upande wetu, ni kutofuata mkumbo wa hao wanaotumia jina la Jumuia kujiingiza na kutumika kama 'tissue' bila ya kujitambua.
Lakini ifahamike, tukiona maslahi yetu yanachezewa, tusisite kuyalinda.