Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Congo wafuate ushauri huu WAngu. Waandae muswada wakae chini na TZ then ijiunge na TZ tuwe nchi Moja. So jukumu LA Hao waasi linakuwa letu zote. Nchi zote 2 zitanufaika kwa biashara na mambo mengine tukikaa pamoja kwa miaka hata 10 tu Hali Yao ya kiusalama itakuwa bora sana.

Aliyekudanganya TZ ni salama ni nani? Siajabu hata nchi yenyewe kama uijuavyo haipo tena, Tanzania ilishaenda, …
 
Kingine kinachowasumbua watusi hasa wa rwanda ni ugumu wa mioyo yao kuachilia na roho ya visasi inayowaandama na hii iko kwenye DNA ila tukumbuke mazingira yanabadilisha genotype za watu so wanaweza kubadilika lakini ni mpaka wakubali kuachilia.
"...tukumbuke mazingira yanabadilisha 'genotype' za watu..."

Mkuu 'SIRE', utaalam huu ndio leo nimeusikia kwako, sijawahi kamwe kuusikia au kuusoma popote!

Unaweza kufafanua kidogo, au kutoa mfano mahsusi unaoeleza swala hili?

Mi nadhani 'mazingira' unayoyazungumzia hapa ni tofauti na hayo yanayoelezwa kubadili hizo 'genotypes'.

Lakini niseme ninakubaliana na mengi ya uliyoyaeleza kuhusu hiki kikabila cha kitutsi, na historia inayowahusu.
 
Congo wafuate ushauri huu WAngu. Waandae muswada wakae chini na TZ then ijiunge na TZ tuwe nchi Moja. So jukumu LA Hao waasi linakuwa letu zote. Nchi zote 2 zitanufaika kwa biashara na mambo mengine tukikaa pamoja kwa miaka hata 10 tu Hali Yao ya kiusalama itakuwa bora sana.
Kwanini usiwashauri watafute Amani kwa njia dialogue?.
 
Ulisome ujifunze maana ya top dog. Kenya hamna utop dog wowote ule mbwiga.

Sina haja ya kusoma upupu wote huo, point yangu ni ile ile be a top dog sio kulia lia kila ukibwekewa na kambwa kadogo.
 
Jinsi ya kupambana na Paul Kagame ni kuadvance kwenye nyanja ya espionage na intelligence ,jeshi kama la Tanzania hili linalokomalia kuonyesha makomando wapasua matofali kwa vichwa , jeshini mnajaza wapumbavu tu kisa ni ndugu na watoto wa Makada ,jeshi hali adapt modern warfare tactics ,weapons NK ,jeshi ambalo haliupdate ,mmekalia kujifariji ujinga na military tactics za enzi za Idd Amin , kazi tunayo .
Ulimwengu uko mbali sana kwa sasa ,jeshi linahitaji brains si watu wenye miili mikubwa kama wabeba magunia wa pale mwanjelwa sokoni .
Hebu Tuonyeshe military tactics za Iddi amini, zinazotumiwa mpaka leo Tuzione mkuu.
 
Hu

Humjui Paulo mtu mrefu ,unamsikia tu ,lile jitu lina akili sana na uzoefu kwenye nyanja ya espionage na ni katili kupita maelezo wakianza kuhesabu roho zilizopotezwa na hilo dude , unaweza zimia ,Paulo Mtu mrefu kapiga misheni za hatari mpaka jamhuri ya kati na ana vikosi mpaka leo ,kapiga mishe za espionage mpaka Bukima faso kule west Africa tena kitambo anafanya mishe hizo na hata mauaji ya Thomas Sankara yaliinvolve spies na hitmen wake .Yule Blaize Campaore kule Bukina Faso aliyefanya yale mapinduzi alikuwa na back up ya Kagame kwa kiasi kikubwa .
Thomas sankara waliuwawa mwaka 1884 na compaore kwa msaada wa wafaransa,
Na kagame 1884 alikuwa na mu7 kumuondoa obote, sasa sijaelewa kama kagame alishirkiana na wafaransa au maana hoja yako ni dhahifu sana.
Wee unavyuona upo sahihi mkuu?
Hebu tuambie au umechukua kutoka kwa waraka wa Christopher mtikila nini, maana yeye ndo alisema.
 
Rais Paul Kagame alikuwa anaapisha mawaziri wapya hapo jana mapema. Alianza kutoa hotuba yake kwa lugha ya Kinyarwanda, lakini baadae akahamia kwenye lugha ya Kiingereza na baadaye akatoa kitisho kizito kwa lugha ya Kiswahili. Wengi wetu tumeona hicho kipande chenye lugha ya kiswahili kikisambaa huko mitandaoni hasahasa kwa raia wa Tanzania na Kenya. Kitendo cha kusambaa mtandaoni kwa kasi hivi, inaonesha kabisa walengwa wa ujumbe ni watu gani.

Kwenye FASIHI njia moja kuu ya kufikishia ujumbe ni kuifahamu HADHIRA, lakini kubwa zaidi ni kufahamu lugha ambayo HADHIRA hutumia. Siku zote kimetumika Kinyarwanda na Kiingereza, lakini leo hii na Kiswahili juu, tena sehemu ambayo anatoa vitisho. Kwenye Dakika ya 27, ameanza kuwaliza mawaziri wake kama wanafahamu lugha ya kiswahili, wakamjibu wanelewa, ndipo akaanza kuzungumza kiswahili.

Huu ujumbe siyo wa wanyarwanda, wazungumzaji wakubwa wa lugha ya kiswahili wanafahamika, hivyo hicho kitisho ni ujumbe kwenu. Hajataja mhusika, mimi binafsi sitamtaja, lakini naamini walengwa mapema leo, watakuwa washafikiwa na huu ujumbe.

Alichokisema Rais Paul Kagame ni kwamba ukubwa wa pua siyo wingi wa kamasi. Kwamba Rwanda doesn't have the means, but they have the methods (ways). Hivyo kijiografia Rwanda ni nchi ndogo isiyo na rasilimali nyingi, lakini wao siyo migomba mifupi kama wanavyofikiriwa. Binafsi naamini, haivuki miaka miwili (2) kuna mtu kwenye huu ukanda wetu wa maziwa makuu atatoa kilio kikubwa sana.

View attachment 2433276
Mwisho wake asha Anza kuuona Sasa wacha atapetape
 
Rais Kagame aachane na kauli za kujigamba na kutunisha misuli!!!
hilo haliwezi kumsaidia zaidi ya kuwatumbukiza wanyaruwanda kwenye matatizo.

Kiongozi mkongwe kama yeye hakupaswa kulopoka na kuonyesha jeuri mbele ya umma!!!
wakati huu aalipaswa aonyeshe ukomavu wake kwa kutatua matatizo kati ya nchi yake na Congo kuliko kuonyesha jeuri.

asijifanye hajui kuwa sio Congo tu inamtuhumu bali nchi zote za East Africa na hata SADAC all are against his conduct towards Congo, hivyo anapo ishutumu Congo maana yake anazishutumu nchi zote hizo!!!

madai yake kuwa ametishwa au maesingizingwa mgogoro wa Congo eti kwa kuwa nchi yake ni dhaifu huo ni ujanja wa kutaka kuficha uovu wake!!

kama anaweza kuwahadaa wanyaruwanda sawa lakini hawezi kuzihadaa nchi zote.

Ni vyema washauri wa Rais wakamshauri vyema kuliko kumuacha anapotea na mwishowe kuingiza nchi kwenye mgogoro mkubwa zaidi.
 
Na wewe usiwe mjinga,Tanzania haijalala kiasi hicho japo hatujafanya vya kutosha naona Kama unahemka kwa vijimaneno vya mfa maji hapo juu..

Tungekuwa hatufanyi kitu Leo hii tusingekuwa na urali wa biashara kuwazidi wote EAC yaana balance of trade yetu na majirani wote Ni surplus in terms of quantity and value licha ya changamoto zote..
Impact yake ikoje katika uhalisia na maisha ya watu wake?

Tusijekuwa na sifa za kijinga kusifiwa na kujisikia wakati tupo hoi.
 
Impact yake ikoje katika uhalisia na maisha ya watu wake?

Tusijekuwa na sifa za kijinga kusifiwa na kujisikia wakati tupo hoi.
Yaani mnachekesha Sana Sasa Serikali huwa inagwa Pesa?

Kwamba hujui impacts take? Hujaskia Serikali imewapa mikopo watoto wote wa elimu ya Juu? Hujaona ada ya form six kufutwa? Huoni ajira kila kukicha? Huoni mabarabara na miradi ya maji nk? Huoni Veta zinajengwa? Mahospitali je?

Ndio maana nikaanza nankukushangaa na kuuliza Serikali huwa inagawa Pesa?

Kitendo Cha exports kuongezeka manake Ni Watzn ndio wameuza zaidi sio Serikali
 
Na wewe usiwe mjinga,Tanzania haijalala kiasi hicho japo hatujafanya vya kutosha naona Kama unahemka kwa vijimaneno vya mfa maji hapo juu..

Tungekuwa hatufanyi kitu Leo hii tusingekuwa na urali wa biashara kuwazidi wote EAC yaana balance of trade yetu na majirani wote Ni surplus in terms of quantity and value licha ya changamoto zote..
Nikusaidie tu kidogo, Tz tuna zaidi ya eneo laki tisa, kenya laki 5, Burundi laki 2, Rwanda elfu 26 Square kms. Karibu wote hao kwa pamoja hawafiki ukubwa Taifa letu.

Unapolinganisha zingatia advantage uliyo na hatua zako dhidi ya wengine ili kujua ufanisi na ubora wako unavyotakiwa kuwa.

Tuko nyuma sana kwa kilometers nyingi.

Usijifie wanao kuvaa nguo zenye viraka wakati wannaweza kuvaa mpya, lakini unafikiri wewe uko bora kwa sababu tu kwa jirani wako uchi. Walio uchi kwa nafasi yao wako bora mara nyingi kuliko wewe mwenye viraka na siku moja watakufundisha jinsi ya kuvaa.
 
Yaani mnachekesha Sana Sasa Serikali huwa inagwa Pesa?

Kwamba hujui impacts take? Hujaskia Serikali imewapa mikopo watoto wote wa elimu ya Juu? Hujaona ada ya form six kufutwa? Huoni ajira kila kukicha? Huoni mabarabara na miradi ya maji nk? Huoni Veta zinajengwa? Mahospitali je?

Ndio maana nikaanza nankukushangaa na kuuliza Serikali huwa inagawa Pesa?

Kitendo Cha exports kuongezeka manake Ni Watzn ndio wameuza zaidi sio Serikali
Unaongea maigizo?
Hao watoto waliopata mikopo wakurudi nyumbani hakuna chakula kwa wazi itasaidia Nini au watarudi kula mikopo?
Watu wanakula mli mmoja wewe unazungumzia mabalabala ambay mvua ikinyesha yanabaki mashimo?

Nyie endeleeni kulamba asali tu, huku kitaa hamjui Nini kinaendelea.
 
Wewe Ni mjinga asiye na chakula anaweza msomesha mtoto Hadi Chuo?
 
Rais Paul Kagame alikuwa anaapisha mawaziri wapya hapo jana mapema. Alianza kutoa hotuba yake kwa lugha ya Kinyarwanda, lakini baadae akahamia kwenye lugha ya Kiingereza na baadaye akatoa kitisho kizito kwa lugha ya Kiswahili. Wengi wetu tumeona hicho kipande chenye lugha ya kiswahili kikisambaa huko mitandaoni hasahasa kwa raia wa Tanzania na Kenya. Kitendo cha kusambaa mtandaoni kwa kasi hivi, inaonesha kabisa walengwa wa ujumbe ni watu gani.

Kwenye FASIHI njia moja kuu ya kufikishia ujumbe ni kuifahamu HADHIRA, lakini kubwa zaidi ni kufahamu lugha ambayo HADHIRA hutumia. Siku zote kimetumika Kinyarwanda na Kiingereza, lakini leo hii na Kiswahili juu, tena sehemu ambayo anatoa vitisho. Kwenye Dakika ya 27, ameanza kuwaliza mawaziri wake kama wanafahamu lugha ya kiswahili, wakamjibu wanelewa, ndipo akaanza kuzungumza kiswahili.

Huu ujumbe siyo wa wanyarwanda, wazungumzaji wakubwa wa lugha ya kiswahili wanafahamika, hivyo hicho kitisho ni ujumbe kwenu. Hajataja mhusika, mimi binafsi sitamtaja, lakini naamini walengwa mapema leo, watakuwa washafikiwa na huu ujumbe.

Alichokisema Rais Paul Kagame ni kwamba ukubwa wa pua siyo wingi wa kamasi. Kwamba Rwanda doesn't have the means, but they have the methods (ways). Hivyo kijiografia Rwanda ni nchi ndogo isiyo na rasilimali nyingi, lakini wao siyo migomba mifupi kama wanavyofikiriwa. Binafsi naamini, haivuki miaka miwili (2) kuna mtu kwenye huu ukanda wetu wa maziwa makuu atatoa kilio kikubwa sana.

View attachment 2433276
tayar, bongo dpw ameileta!
 
Late Mch. Mtikila kumchambua tolu vibaya mno. Tolu kajaza spy kwenye kila idara. Siku hizi kukuta wanyarwanda wakipiga mishe hapa Tanzania bila hata vibali sio ajabu tena.
 
Back
Top Bottom