Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Na wewe usiwe mjinga,Tanzania haijalala kiasi hicho japo hatujafanya vya kutosha naona Kama unahemka kwa vijimaneno vya mfa maji hapo juu..

Tungekuwa hatufanyi kitu Leo hii tusingekuwa na urali wa biashara kuwazidi wote EAC yaana balance of trade yetu na majirani wote Ni surplus in terms of quantity and value licha ya changamoto zote..
huna akili.
 
Tuko busy na uchaguzi 2025.

Huko barabarani tuko busy na maving'ora 24/7 maspeed na kuweka mafoleni, sijui huwa tunawahi wapi na tunawahi nini maana yale ya msingi tunayopaswa kuyafanya hatuyafanyi..

Ruto anapambana kuongeza idadi ya diaspora wakenya duniani, wakati huo anaendeleza utaratibu wa kuzalisha skilled and intelligent workforce ya kenya ili itapakae kila kona duniani..

Tupo busy kubrainwash vijana na kuendelea kuwa chawa wa viongozi, tuko busy kuendelea kuongeza workforce pumbavu inayowaza siasa, tuko busy kufanya vijana wawe tegemezi wa baba zao wezi waliokwenye system.. We paralysized kila mahala na maadui wetu wanafuatilia nyendo zetu kila siku ili siku ikifika watuslave.
Fact yaani totally nonsense
 
..M-23 wanafadhiliwa na Rwanda na Uganda.

..Waasi hao walishapigwa na kufukuzwa Congo na vikosi vya Tanzania, Afrika Kusini, na Malawi.

..Baada ya kupokea kichapo walikimbilia Rwanda na Uganda ambako ilitakiwa wanyang'anywe silaha na wasiruhusiwe kufanya chokochoko dhidi ya Congo.

..Kinachotakiwa kufanyika ni Congo na SADC-FIB kutoa kichapo kikali zaidi ya kile cha mwanzo.
Unazungumza kwa mihemko ila Kuna sehemu umesema wanafadhiliwa na Rwanda na Uganda Ni Kweli

Ila sas kosa kubwa alililifanya tshekedi Ni kujumuisha Uganda kwenye operation hyo ya kuwaondoa waasi na kuleta amani mashariki mwa Kongo[emoji41]

Kosa la kuwjulisha Uganda ktk Operation no kosa ambalo watajuta maishani
 
Kagame ameshakaa madarakani muda mrefu sana,amefikia sasa ile hali ya kujiona kuwa hakuna anayemuweza,hizo ni lugha za viongozi wengi waliokaa muda mrefu kwenye madaraka na anafikiri kwakuwa wananchi wameshindwa kumtoa kwenye kura basi anaamini kuwa ni untouchable kwenye kila kitu,sasa aendelee kujitutumua tu,lakini nadhani sasa atakuwa anajiandalia mwisho wa utawala wake kama asipotumia hekima...
 
Wamekuwa dhaifu Tena si unawaona wa maana wewe au? Huna msimamo na hata huelewi unachosimamia.
Usiwe mjinga wewe, wapi nimesema wa maana? Ni juha ndiye anasifia anachopata bila kujali ni kiasi gani hasa anastahili kupata kulingana na nguvu na uwezo alio nao..ndio maana kwenye boxing wanapima uzito, haiwezekani mwenye uzito heavyweight apigane na middle weight halafu unajisifu umeshinda.. wewe ni nchi yenye watu 61 million unajisifu kuwashinda watu hawazidi hata 35 million..unless kichwani hazitoshi ndio huwezi kuona ukweli ninaousema.
 
Rais Paul Kagame alikuwa anaapisha mawaziri wapya hapo jana mapema. Alianza kutoa hotuba yake kwa lugha ya Kinyarwanda, lakini baadae akahamia kwenye lugha ya Kiingereza na baadaye akatoa kitisho kizito kwa lugha ya Kiswahili. Wengi wetu tumeona hicho kipande chenye lugha ya kiswahili kikisambaa huko mitandaoni hasahasa kwa raia wa Tanzania na Kenya. Kitendo cha kusambaa mtandaoni kwa kasi hivi, inaonesha kabisa walengwa wa ujumbe ni watu gani.

Kwenye FASIHI njia moja kuu ya kufikishia ujumbe ni kuifahamu HADHIRA, lakini kubwa zaidi ni kufahamu lugha ambayo HADHIRA hutumia. Siku zote kimetumika Kinyarwanda na Kiingereza, lakini leo hii na Kiswahili juu, tena sehemu ambayo anatoa vitisho. Kwenye Dakika ya 27, ameanza kuwaliza mawaziri wake kama wanafahamu lugha ya kiswahili, wakamjibu wanelewa, ndipo akaanza kuzungumza kiswahili.

Huu ujumbe siyo wa wanyarwanda, wazungumzaji wakubwa wa lugha ya kiswahili wanafahamika, hivyo hicho kitisho ni ujumbe kwenu. Hajataja mhusika, mimi binafsi sitamtaja, lakini naamini walengwa mapema leo, watakuwa washafikiwa na huu ujumbe.

Alichokisema Rais Paul Kagame ni kwamba ukubwa wa pua siyo wingi wa kamasi. Kwamba Rwanda doesn't have the means, but they have the methods (ways). Hivyo kijiografia Rwanda ni nchi ndogo isiyo na rasilimali nyingi, lakini wao siyo migomba mifupi kama wanavyofikiriwa. Binafsi naamini, haivuki miaka miwili (2) kuna mtu kwenye huu ukanda wetu wa maziwa makuu atatoa kilio kikubwa sana.
Nikawaida kwa debe tupu kupiga makelele.
 
Magufuli (rip) aliyekuwa anatuhimiza kufanya kazi kwa bidii hayupo, sasa kwa nini tusishinde mitandaoni? Enzi za kuuza ngada na kujikusanyia mipesa na kushinda vijiweni zimerudi, wewe unataka tuwe bize na nini tena?
Acha yeye aendelee kubeba magunia sisi atuache tushinde mitandaoni huku tukiuza ngada na maisha yanaenda
 
Mimi sijui kwa nini nna imani kubwa sana na nchi yangu ya Tanzania. Naamini malalamiko ya wananchi huwa hayakosi kwenye nchi yoyote ile iwe Tajir au maskini. Lakini kwenye ishu ya usalama wa nchi, ni kitu ambacho hakuna nchi inalala usingizi.
Ukiangalia sana, katika ukanda wa Afrika mashariki, ni Tanzania tu ambayo haijigambi kabisa kuhusu jeshi lake, ipo kimya sana as if hakuna kinachoendelea kwenye majeshi yetu.
Sasa kwa ukimya huo, nchi nyingine zisichukulie poa sana. Tz ipo vizuri zaidi ya tuijuavyo.
Kama hotuba ya jamaa ilichomekwa kwa kiswahili, inaamana TZ pia ilikua ni target kwa sababu ingeishia kwenye English, basi tungejua anawalenga Kenya, Congo na Uganda na nchi nyingine zinazoweka English mbele.
Kiswahili ilikua kwa ajili yetu! Lakini hatujalala. Tangu 1978 tunatambua umuhimu wa kuimalisha usalama eneo lote la kaskazini Magharibi na Magharibi kwa ujumla.
 
Magufuli (rip) aliyekuwa anatuhimiza kufanya kazi kwa bidii hayupo, sasa kwa nini tusishinde mitandaoni? Enzi za kuuza ngada na kujikusanyia mipesa na kushinda vijiweni zimerudi, wewe unataka tuwe bize na nini tena?
Halafu hakuwah kuajili
 
Kama kamtisha Rutto basi nasikitika kusema Kagame ataondoka madarakani na Rwanda utakuwa mkoa wa Kenya.

Rutto anaonekana kama padri lakini ni moja ya watu wenye mioyo ya chuma kupigania anachoamini.

Tusidanyike humu na maneno ya vijiweni Rwanda is overrated na haina uwezo wa kupigana na Kenya
 
Tuko busy na uchaguzi 2025.

Huko barabarani tuko busy na maving'ora 24/7 maspeed na kuweka mafoleni, sijui huwa tunawahi wapi na tunawahi nini maana yale ya msingi tunayopaswa kuyafanya hatuyafanyi..

Ruto anapambana kuongeza idadi ya diaspora wakenya duniani, wakati huo anaendeleza utaratibu wa kuzalisha skilled and intelligent workforce ya kenya ili itapakae kila kona duniani..

Tupo busy kubrainwash vijana na kuendelea kuwa chawa wa viongozi, tuko busy kuendelea kuongeza workforce pumbavu inayowaza siasa, tuko busy kufanya vijana wawe tegemezi wa baba zao wezi waliokwenye system.. We paralysized kila mahala na maadui wetu wanafuatilia nyendo zetu kila siku ili siku ikifika watuslave.
Tena kirahisi kabisa !
 
Na wewe usiwe mjinga,Tanzania haijalala kiasi hicho japo hatujafanya vya kutosha naona Kama unahemka kwa vijimaneno vya mfa maji hapo juu..

Tungekuwa hatufanyi kitu Leo hii tusingekuwa na urali wa biashara kuwazidi wote EAC yaana balance of trade yetu na majirani wote Ni surplus in terms of quantity and value licha ya changamoto zote..
Naongea kwa uchungu mkubwa toka Moyoni mwangu,nakupenda Tanzania yangu,Lakini ipo siku watu watasema nyie CCM na mafisadi,Majizi yote muende mkapigane wenyewe Vita,kwa maslai yenu wenyewe,wanyonge na wapinzani na wapenda haki wataungana na adui bila kujua dhumuni la adui ni nini?hiyo siku ngumu inakuja tena haiko mbali
 
Back
Top Bottom