Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Hujamuelewa naona katumia Kiswahili ili kuongea na wakongomani wa kunako uwanja wa mapambano maana wanazungumza Kiswahili cha ‘kwa fasi ya’

Kwakweli ni Speech nzuri, na amegusa mambo yote muhimu na sintofahamu zinazosambazwa na Watu wasiotaka Amani italamaki katika Kongo ya Mashariki

Kudos Raisi wa Rwanda Paul Kagame.
 
Rais Paul Kagame alikuwa anaapisha mawaziri wapya hapo jana mapema. Alianza kutoa hotuba yake kwa lugha ya Kinyarwanda, lakini baadae akahamia kwenye lugha ya Kiingereza na baadaye akatoa kitisho kizito kwa lugha ya Kiswahili. Wengi wetu tumeona hicho kipande chenye lugha ya kiswahili kikisambaa huko mitandaoni hasahasa kwa raia wa Tanzania na Kenya. Kitendo cha kusambaa mtandaoni kwa kasi hivi, inaonesha kabisa walengwa wa ujumbe ni watu gani.

Kwenye FASIHI njia moja kuu ya kufikishia ujumbe ni kuifahamu HADHIRA, lakini kubwa zaidi ni kufahamu lugha ambayo HADHIRA hutumia. Siku zote kimetumika Kinyarwanda na Kiingereza, lakini leo hii na Kiswahili juu, tena sehemu ambayo anatoa vitisho. Kwenye Dakika ya 27, ameanza kuwaliza mawaziri wake kama wanafahamu lugha ya kiswahili, wakamjibu wanelewa, ndipo akaanza kuzungumza kiswahili.

Huu ujumbe siyo wa wanyarwanda, wazungumzaji wakubwa wa lugha ya kiswahili wanafahamika, hivyo hicho kitisho ni ujumbe kwenu. Hajataja mhusika, mimi binafsi sitamtaja, lakini naamini walengwa mapema leo, watakuwa washafikiwa na huu ujumbe.

Alichokisema Rais Paul Kagame ni kwamba ukubwa wa pua siyo wingi wa kamasi. Kwamba Rwanda doesn't have the means, but they have the methods (ways). Hivyo kijiografia Rwanda ni nchi ndogo isiyo na rasilimali nyingi, lakini wao siyo migomba mifupi kama wanavyofikiriwa. Binafsi naamini, haivuki miaka miwili (2) kuna mtu kwenye huu ukanda wetu wa maziwa makuu atatoa kilio kikubwa sana.
Wacha woga wewe, Rwanda anaweza kutisha nchi dhaifu siyo imara
 
Usiwe mjinga wewe, wapi nimesema wa maana? Ni juha ndiye anasifia anachopata bila kujali ni kiasi gani hasa anastahili kupata kulingana na nguvu na uwezo alio nao..ndio maana kwenye boxing wanapima uzito, haiwezekani mwenye uzito heavyweight apigane na middle weight halafu unajisifu umeshinda.. wewe ni nchi yenye watu 61 million unajisifu kuwashinda watu hawazidi hata 35 million..unless kichwani hazitoshi ndio huwezi kuona ukweli ninaousema.
Wewe no zwawa ndio maana huna sequence ya unachoongea..

Ukipiga hatua hujipongezi Lisa hujafikia viwango ulivyotarajia?
 
Kagame kama kweli anajiamini kwanini asianzishe hiyo vita anayojitapa kila siku yuko vizuri?

Huku kujisifu kwake kila siku bila vitendo vyovyote pia kunaweza kuwa ni dalili ya mtu asiyejiamini, anajihami tu, ili aachwe aendelee kuharibu amani ya eneo la maziwa makuu.

Huyu anaweza kuwa anaongoza kwa mdomo na ujuaji kuwashinda marais wote wa hili eneo, lakini sio zaidi ya hapo, kama anaona anachokozwa kila siku kwanini asiwafundishe adabu hao wachokozi?
Mbona alishafanya 1st and 2nd Congo war. Unless umesahau vifo vya Congolese million 5 kati ya 1998 na 2003!!
 
Hali yake ni mbaya sana tangu Sir Ruto kuingia imekuwa pigo kwake alijaribu kumtumia mtoto wa museveni kuchonganisha ikabuma,ni kati ya marais wapumbavu EAC anayetumika na mabeberu bila kificho
Ruto kwa Kagame ni sisimizi tu, majibu atayapata kama kilichowakuta kule Kapedo!!
 
Bila kupepesa macho mi nipo upande wa kagame , namkubali Sana Raisi anayeipambania nchi yake...!! Huwez kuwa unaninyonya , umeme hakuna alaf wakat wa shida nikupambanie
Mbona ikifika utapelekwa frontline kwa lazima
 
577153h700.jpg

Vita yetu Tanzania
 
Rais Paul Kagame alikuwa anaapisha mawaziri wapya hapo jana mapema. Alianza kutoa hotuba yake kwa lugha ya Kinyarwanda, lakini baadae akahamia kwenye lugha ya Kiingereza na baadaye akatoa kitisho kizito kwa lugha ya Kiswahili. Wengi wetu tumeona hicho kipande chenye lugha ya kiswahili kikisambaa huko mitandaoni hasahasa kwa raia wa Tanzania na Kenya. Kitendo cha kusambaa mtandaoni kwa kasi hivi, inaonesha kabisa walengwa wa ujumbe ni watu gani.

Kwenye FASIHI njia moja kuu ya kufikishia ujumbe ni kuifahamu HADHIRA, lakini kubwa zaidi ni kufahamu lugha ambayo HADHIRA hutumia. Siku zote kimetumika Kinyarwanda na Kiingereza, lakini leo hii na Kiswahili juu, tena sehemu ambayo anatoa vitisho. Kwenye Dakika ya 27, ameanza kuwaliza mawaziri wake kama wanafahamu lugha ya kiswahili, wakamjibu wanelewa, ndipo akaanza kuzungumza kiswahili.

Huu ujumbe siyo wa wanyarwanda, wazungumzaji wakubwa wa lugha ya kiswahili wanafahamika, hivyo hicho kitisho ni ujumbe kwenu. Hajataja mhusika, mimi binafsi sitamtaja, lakini naamini walengwa mapema leo, watakuwa washafikiwa na huu ujumbe.

Alichokisema Rais Paul Kagame ni kwamba ukubwa wa pua siyo wingi wa kamasi. Kwamba Rwanda doesn't have the means, but they have the methods (ways). Hivyo kijiografia Rwanda ni nchi ndogo isiyo na rasilimali nyingi, lakini wao siyo migomba mifupi kama wanavyofikiriwa. Binafsi naamini, haivuki miaka miwili (2) kuna mtu kwenye huu ukanda wetu wa maziwa makuu atatoa kilio kikubwa sana.
Kuna haja ya kuifuta Rwanda kwenye ramani ya Africa sasa. Hayo majigambo yake yanafaa yajibiwe kama alivyojibiwa Dada Iddi Amin
 
Mama kamuweka BASHUNGWA wizara ya Ulinzi hakika atavuna alichokipanda kwa Mnyarwanda huyu
Sio kweli bashungwa kama kisu kisicho na makali kuchinjia ng’ombe
Je unajuwa yule mama alipopewa uwaziri wq ulinzi kuna wakuu wa jeshi walimgomea.
 
Tatizo mpo divided sana, ikitokea vita trust me Kuna watu wataombea Ruto apinduliwe!!!

Then Kenya Haina jeshi imara, kama mlidunguliwa na amateurs huko samburu au trans mara ndio mtaweza kupambana na Battle-hardened RPF??

Bora Uganda au Tanzania, ila Kenya is weak na mtapata mnachokitafuta.

Una uhuru wa maoni ila thubutu, mahuasiano ya kimataifa sio hizi tambo unaleta hapa ulizozoea za Simba/Yanga....
 
Kama kamtisha Rutto basi nasikitika kusema Kagame ataondoka madarakani na Rwanda utakuwa mkoa wa Kenya.

Rutto anaonekana kama padri lakini ni moja ya watu wenye mioyo ya chuma kupigania anachoamini.

Tusidanyike humu na maneno ya vijiweni Rwanda is overrated na haina uwezo wa kupigana na Kenya
Unajua ili ufike Rwanda tokea Kenya lazima Upite Uganda?
 
Kuna haja ya kuifuta Rwanda kwenye ramani ya Africa sasa. Hayo majigambo yake yanafaa yajibiwe kama alivyojibiwa Dada Iddi Amin
Kushindwa Vita kunatakiwa vitu viwili 1. Support ya wananchi 2. Jeshi imara

Kikikosekana kimoja Kati ya hvyo viwili hamna kitu utafanya...sasa jiulize wananchi wako na wewe au wamepoteza matumaini na serikali yako
 
Huyu Usitake Ncheke anajikuta na yeye ni kama Israel ndani ya Middle East!,kutwa kuwaasumbua Waarabu.Lakini JK alikosea sana kipindi kile alivyowachapa M23 na kumuacha huyu mwehu madarakani.
Tanzania ndo ingepata hasara maana angetuletea Wakimbizi ambao wangekuja lipa kisasi hata miaka 50 ijayo
 
Back
Top Bottom