Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Kuna mambo hii nchi yetu inaweza kuwa imelala..ila sio kila jambo.

Kuwa tu Incharge kwenye Hospitali zetu kubwa mfano JKCI kuna vetting ya hatari inapitishwa..itakuja kuwa Wizara ya ulinzi?.

Na jambo jingine Waziri pale WU anampelekea tu Rais maombi ya Jeshi na bajeti zao..hakuna lingine la maana analoweza kuingilia na kuinfluence lifanyike kama Jeshi halitaki.
Vetting Bongo!!!!

Takataka kabisa
 
Rais Paul Kagame alikuwa anaapisha mawaziri wapya hapo jana mapema. Alianza kutoa hotuba yake kwa lugha ya Kinyarwanda, lakini baadae akahamia kwenye lugha ya Kiingereza na baadaye akatoa kitisho kizito kwa lugha ya Kiswahili. Wengi wetu tumeona hicho kipande chenye lugha ya kiswahili kikisambaa huko mitandaoni hasahasa kwa raia wa Tanzania na Kenya. Kitendo cha kusambaa mtandaoni kwa kasi hivi, inaonesha kabisa walengwa wa ujumbe ni watu gani.

Kwenye FASIHI njia moja kuu ya kufikishia ujumbe ni kuifahamu HADHIRA, lakini kubwa zaidi ni kufahamu lugha ambayo HADHIRA hutumia. Siku zote kimetumika Kinyarwanda na Kiingereza, lakini leo hii na Kiswahili juu, tena sehemu ambayo anatoa vitisho. Kwenye Dakika ya 27, ameanza kuwaliza mawaziri wake kama wanafahamu lugha ya kiswahili, wakamjibu wanelewa, ndipo akaanza kuzungumza kiswahili.

Huu ujumbe siyo wa wanyarwanda, wazungumzaji wakubwa wa lugha ya kiswahili wanafahamika, hivyo hicho kitisho ni ujumbe kwenu. Hajataja mhusika, mimi binafsi sitamtaja, lakini naamini walengwa mapema leo, watakuwa washafikiwa na huu ujumbe.

Alichokisema Rais Paul Kagame ni kwamba ukubwa wa pua siyo wingi wa kamasi. Kwamba Rwanda doesn't have the means, but they have the methods (ways). Hivyo kijiografia Rwanda ni nchi ndogo isiyo na rasilimali nyingi, lakini wao siyo migomba mifupi kama wanavyofikiriwa. Binafsi naamini, haivuki miaka miwili (2) kuna mtu kwenye huu ukanda wetu wa maziwa makuu atatoa kilio kikubwa sana.

View attachment 2433276
Vitisho hivyo hivyo,
Maneno mengi, hakuna lolote we unafikili kenya wakipeka askari 30k na equipment zao kule congo zitatoka nini .
 
Bahati nzuri mibongo ni VIAZI waioumbiwa kusahau.
Huyu jamaa ilikuwa 2013 , hakukimbia walimuua kinywa kinywa, waliogopa familia yake watamtafuta , ni ile ishu, kugombana na kikwete.
 
Chonde wadau tusishabikie sanaa hili swala bali tumuombe Mwenyezi Mungu aingilie kati, DRC ameharibu sanaa kwanza aliaza kutuhumu mashirika yakimataifa kwamba yanachochea vita na uvunjifu wa amani DRC,Pili akamfukuza balozi wa Rwanda harshly wakati EAC ipo ndo mahali pakusemea, Tatu akaituhumu serikali ya Rwanda directly kuwa wanajihusisha na M23,wazungu wanaweza kuwa nyuma ya Rwanda maana na wao walituhumiwa pia kupitia mashirika yao ya UN(vita sio ukubwa wa nchi vita ya sasa ni technology) Tusali na kuswali tuombe Mungu atuepushe na hili pepo Viongozi wetu wajazwe hekima na busara aminaaaa
DRC Hawaii tayari kuanzisha vita coz wenyewe wanajua jeshi Lao lipo disorganised, hawataweza kupigana.
 
Kwahiyo unafikiri alikiwa huyo tu mmoja?
Wapo wengine baadhi kwa kipindi kile walistaafishwa na hawakuwa wengi. Mzee wangu niliiona anaongea na kanali wa jeshi ni rafiki yake,
Walimwambia walikuwepo ila waliondolewa wote na wengine waliamua tuu muache kazi.
Kwa sasa sina UHAKIKA kama wapo coz baada ya ile ishu walikuwa makini sana. Na usajili wa watu jeshini.
 
Acha uwongo na kujipa matumaini yasiyokuwepo.
 
Hivi yule jamaa wa mabakamabaka mwenye asili ya Tall aliyechomoka na kompyuta mpakato yenye mabaka alipatakina? Hata hvyo kuna wenye mabakamabaka wenye asili ya Tall kadhaa tunajumuika nao halafu hatushituki. Tall anaweza kuwa na info nyingi sana za wananchi wa uswahilini kuliko tunavyodhani. Uswahilini tumejiachia sna hadi kwenye sehemu nyeti. Tall huwa yupo smart sana kwenye data/info na anajua azitumie vp. Hivyo usije ukashangaa Argentina kufungwa Saudi Arabia.
Mpira unafananisha na vita.
Kagame anaijua vizuri sana congo.
Baada ya second congo war , waasi wa RCD walikuwa ni watutsi wengi wao kutoka rwanda.
Na baada ya ile vita 2003, na kusaidiwa matamba walikubaliana waasi wa RCD wajiunge kwenye jeshi la congo , wacongo coz walikuwa WANATAKA kumaliza wakalazimika kufanya hivyo. Bila kujali kundi la RCD walikuwa ni wanajeshi la rwanda .
Na kweli wanajeshi wa rwanda wakaingia ndani ya jeshi la congo. Na waliingia wengi tuu.
Lakini baada ya kuingizwa amejitaidi sana KUMPINDUA kabila mdogo na wanajeshi wake hao hao aliyowapenyeza ila akashidwa mpaka leo.
Jeshi lake mara ya mwisho kufika Kinshasa ni 1997 kama sijakosema. Licha ya kupenyeza wanajeshi wengi ndani ya jeshi la congo na kuwatumia kina laurent nkunda batwale, bosco ntaganda na wengine kashidwa kuipindua serikali ya congo.
 
Vita sio jambo la kuchukulia kirahisi...
Kwanza inategemea mfadhili wako ni nani na ana maslahi gani kwenye hiyo vita.
Vita haitegemei ukubwa wa nchi wala wingi wa watu ulionao bali kuwa na watu sahihi na wa kutosha katika sehemu nyeti za ulinzi wa nchi...Hilo ni la muhimu sana, halafu inafuata teknolojia...
Mimi natabiri kuwa kagame atakuja kusumbua sana siku za baadae...yeyote aliyefika Rwanda anaweza kuthibitisha hilo...inaonekana kagame na ubaya wake wote lakini ana vision flani na nchi yake na hili ni tofauti sana na nchi nyingi zinazomzunguka ambazo zinaendeshwa kwa miluzi mingi...
Ni vizuri tusimpuuze ila tujipange vizuri hasa kwenye intelegensia manake wabongo wengi tuna tabia ya kuropoka mambo nyeti ya nchi tena hata kwenye sehemu za starehe.
 
Acha uwongo na kujipa matumaini yasiyokuwepo.
Wewe ndo muoga , unavyoonekana unamuogopa sana kagame ,
Hivyo ni vitisho,
Ni sawa na vita vya Mongolia, waliokuwa wanakupa kitisho kimoja tuu, unakuwa mpole. Wewe Hufai hata kuwa mwanajeshi tena hata kiongozi, pole sana.
Vitisho tuu ville tuu.😃😃😃
 
Mpira unafananisha na vita.
Kagame anaijua vizuri sana congo.
Baada ya second congo war , waasi wa RCD walikuwa ni watutsi wengi wao kutoka rwanda.
Na baada ya ile vita 2003, na kusaidiwa matamba walikubaliana waasi wa RCD wajiunge kwenye jeshi la congo , wacongo coz walikuwa WANATAKA kumaliza wakalazimika kufanya hivyo. Bila kujali kundi la RCD walikuwa ni wanajeshi la rwanda .
Na kweli wanajeshi wa rwanda wakaingia ndani ya jeshi la congo. Na waliingia wengi tuu.
Lakini baada ya kuingizwa amejitaidi sana KUMPINDUA kabila mdogo na wanajeshi wake hao hao aliyowapenyeza ila akashidwa mpaka leo.
Jeshi lake mara ya mwisho kufika Kinshasa ni 1997 kama sijakosema. Licha ya kupenyeza wanajeshi wengi ndani ya jeshi la congo na kuwatumia kina laurent nkunda batwale, bosco ntaganda na wengine kashidwa kuipindua serikali ya congo.
Kupigana vita siyo lazima ushike bunduki. Hiyo huwa ni hatua ya mwisho kabisa!
 
Wewe ndo muoga , unavyoonekana unamuogopa sana kagame ,
Hivyo ni vitisho,
Ni sawa na vita vya Mongolia, waliokuwa wanakupa kitisho kimoja tuu, unakuwa mpole. Wewe Hufai hata kuwa mwanajeshi tena hata kiongozi, pole sana.
Vitisho tuu ville tuu.😃😃😃
Wewe endelea kujipa ujasiri wa Simba kwa usichokijua. Tunaojua Hali HALISI TUNAKUONA wa ajabu kweli.

Endelea kuishi kwa historia na matumaini ya mwendawazimu.
 
Kuwahusisha Uganda na kuitenga Rwanda ilikuwa makosa...

Bora wangehusika wote tu.
Unazungumza kwa mihemko ila Kuna sehemu umesema wanafadhiliwa na Rwanda na Uganda Ni Kweli

Ila sas kosa kubwa alililifanya tshekedi Ni kujumuisha Uganda kwenye operation hyo ya kuwaondoa waasi na kuleta amani mashariki mwa Kongo[emoji41]

Kosa la kuwjulisha Uganda ktk Operation no kosa ambalo watajuta maishani
Bukyanagandi MALCOM LUMUMBA lwaitama1 Kichuguu
 
Wewe endelea kujipa ujasiri wa Simba kwa usichokijua. Tunaojua Hali HALISI TUNAKUONA wa ajabu kweli.

Endelea kuishi kwa historia na matumaini ya mwendawazimu.
Tena mkuu kwa kipindi kile Kagame Nakumbuka alisema anajua hata shuka la kulalia la kikwete, tena alimwambia nakusubili sehemu sahihi nikupige, tena alidhamilia sana tena sana, Sana tena sana, na kwa kipindi kile alisema kabisa hata michoro wa ikulu ya DSM anaujua , na alikuwa na watu wengi tuu hapa bongo mpk huyo tuliyemsema.
Kwa alifanya nini kipindi kile? Naomba nijibu
 
Miaka miwili hapo aligombana na museveni mapaka wakafungiana mipaka, tena museveni alikuwa anauwa RAIA wa rwanda anarudisha maiti rwanda. Na museveni akakamata mtu mwenye asili ya rwanda kwenye jeshi sijui la police like,
Kagame alisema kabisa atamfanya kitu flani .
Tena museveni alikuwa anawatena mpaka wasichana wa rwanda na kuwaweka gelezani , kagame mwishowe akawaambia raia wake mseende Kule uganda. Kuwalinda siwezi , kwani alifanya nini mkuu
Tena Uganda kuna watutsi wengi sana kutoka rwanda zaidi ya huku, kama hujui tena kule ndo wanajiita kabisa banyarwanda wapo wengi sana, tena wametengeneza Mpaka umoja,
Vitisho tuu hakuna lolote ni mtu wa mikwara sana
Hacha uoga kijana.
 
Kagame kama kweli anajiamini kwanini asianzishe hiyo vita anayojitapa kila siku yuko vizuri?

Huku kujisifu kwake kila siku bila vitendo vyovyote pia kunaweza kuwa ni dalili ya mtu asiyejiamini, anajihami tu, ili aachwe aendelee kuharibu amani ya eneo la maziwa makuu.

Huyu naona anaweza kuwa anaongoza kwa mdomo na ujuaji kuwashinda marais wote wa hili eneo, lakini sio zaidi ya hapo, kwasababu kama anaona anachokozwa kila siku kwanini asiwafundishe adabu hao wachokozi?
😀😀😀😆😁😁
Si ndo hapo yeye anadai congo kuna Makundi ya wahutu wanaotaka kurudi rwanda kuuwa watu , na anapeleja m23 kutafuta wahutu hao na kulinda watutsi wa congo wasiuwawe, lakini cha ajabu m23 wanapigana na jeshi la congo eneo la kivu ya kaskazini tuu hawaende kwengine. Na wanapigana eneo la mpakani na congo na rwanda , pembezoni mwa mpaka na MARA nyingi tuu wanapigwa sana , kuna siku walipigana mpaka wakaomba mabigano wasimamishwe.
 
Back
Top Bottom