Mimi sijui kwa nini nna imani kubwa sana na nchi yangu ya Tanzania. Naamini malalamiko ya wananchi huwa hayakosi kwenye nchi yoyote ile iwe Tajir au maskini. Lakini kwenye ishu ya usalama wa nchi, ni kitu ambacho hakuna nchi inalala usingizi.
Ukiangalia sana, katika ukanda wa Afrika mashariki, ni Tanzania tu ambayo haijigambi kabisa kuhusu jeshi lake, ipo kimya sana as if hakuna kinachoendelea kwenye majeshi yetu.
Sasa kwa ukimya huo, nchi nyingine zisichukulie poa sana. Tz ipo vizuri zaidi ya tuijuavyo.
Kama hotuba ya jamaa ilichomekwa kwa kiswahili, inaamana TZ pia ilikua ni target kwa sababu ingeishia kwenye English, basi tungejua anawalenga Kenya, Congo na Uganda na nchi nyingine zinazoweka English mbele.
Kiswahili ilikua kwa ajili yetu! Lakini hatujalala. Tangu 1978 tunatambua umuhimu wa kuimalisha usalama eneo lote la kaskazini Magharibi na Magharibi kwa ujumla.