Paul Kimiti akiri kuhujumu Katiba ya Joseph Sinde Warioba

Paul Kimiti akiri kuhujumu Katiba ya Joseph Sinde Warioba

Leo jumatatu katika kipindi cha Dakika 45 cha ITV kinachoongozwa na Farhia Middle aliyekuwa Waziri wa Kilimo na pia kada maarufu wa CCM amekiri kuhujumu katiba ya Warioba ambayo ilipendekeza serikali tatu.

Itakumbukwa Kimiti alikuwa mjumbe wa Tume ya Warioba iliyozunguka nchi nzima kutafuta maoni ya wananchi juu ya katiba mpya. Aidha alikuwa Mwenyekiti wa kamati namba 16 ndani ya Bunge la katiba.

Katika kipindi cha leo amesema aliona serikali tatu zitaleta mgawanyiko na hatimaye kuvunjika kwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar na hivyo kwenda kinyume na makubaliano ya Tume ya Warioba. Kwa hiyo alishiriki kuwashawishi wajumbe wa kamati yake namba 16 kupinga mapendekezo ya Tume ya Warioba.

Pole sana Mzalendo Warioba kwa kusalitiwa wa wajumbe wanafiki wa Tume yako!
HAO WAZEE WATACHOMWA MOTO WA GAS
 
Daaah!! Siri zingine si ni zakuondoka nazi ukilala kimoja au??? Y aseme sasa hivi? Ana nia gani au kakumbwa na nini?.. labda toba ya uwazi. Ana bahati wananchi watulivu, nchi zingine angeshaona majanga.

Ameboa lakini.. Angelanalo kimya.. Inasikitisha.. kideo wapi tumuwone na sura yake akiyaongea..
 
tukiweza kudhibit external forces within our internal politics, na tukaweza kudhibit imotions zetu wenyewe kwenye masuala ya kitaifa, tukaamua kuwa waungwana na wastahimilivu dhidi ya mawazo na mitazamo tofauti yetu au ya wengine, Lazima tutapiga hatua kubwa mno ya maendeleo 🐒

misimamo binafsi na ya vyama vyetu wala haina tija, zaidi sana inatuchelewesha tu na kudhoofisha umoja na uzalendrooo wetu kwa Taifa letu...
Still we have a chance, we can...
Wewe unalipwa nyingi sana huko Lumumba FC umekua mtetezi wa mafisadi mpaka Lucas mwashambwa anakuogopa
 
Wewe unalipwa nyingi sana huko Lumumba FC umekua mtetezi wa mafisadi mpaka Lucas mwashambwa anakuogopa
sina haja ya malipo hata kidogo napodhihirisha ukweli bayana na kinagaubaga 🐒🐒

daima ukweli na uzalendo hauhitaji malipo unajilipa wenyewe 🐒

nitawaombea kwa Mungu, viongozi wa nchi hii bure, na nitawasilisha maoni na mtazamo wangu kwa jamii dhidi ya viongozi wa nchi bure 🐒

Mungu ampetupatia vyote tulivyo navyo, mathalani karama, uwezo na vipaji mbalimbali bure, yafaa basi tutoe bure, tena kwa ukarimu 🐒
 
Unafiki ni tabia ya mtu kutokuonyesha hisia zake halisi au kutokuwa mkweli, yaani mtu anafuata mkumbo ili asieleweke vibaya!

Kwa hiyo mtu wa namna hiyo si wa kumwamini katika kutoa maamuzi magumu kwani anaweza kuwaponza. Mtu wa hivyo haoni shida kwenda kuwachongea au hata kutoa siri kwa maadui wenu.

Kwa kifupi HAFAI KUSHIRIKIANA NAYE!
kiufupi kabisa hafungwi na mtazamo au maoni ya mtu au taasisi fulani. Ni mtu mzima mwenye upeo na utashi wake binafsi wa kua assess faida na madhara ya hoja fulani.🐒

Lakini zaid sana, yule Mzee si nyumbu au ng'ombe wa kupelekwa pelekwa tu bila uelekeo ati kwasabb fulani kaamua hivi au vile 🐒

he is, determined, bold and very focused senior politician we have in this country 🐒

Lazima muheshimu maoni na mtazamo wake, sio kubabaika na kuzubaa na mrengo aliechukua dhidi ya serikali3, mkadhani atayumba na kupanic kwenu 🐒
 
Ndiyo kwa kuwa alikuwa anawakilisha Tume ili kutoa ufafanuzi wa mambo ambayo wajumbe wa kamati yake hawayaelewi! Ilikuwa hafai kuongoza kamati na angekataa kubeba majukumu ambayo hayawezi!
Sio hoja..hujui siasa
 
Ni hatari sana kuwa na wazee wanafiki! Tume imekubaliana jambo na yeye akiwa anakubali kumbe anachora tu wenzake!
Nani amekwambia tume imekubaliana..sema wamepiga kura wengi wape..matumizi ya demokrasia tu..haimaanishi hawakutofautiana kimawazo
 
Nani amekwambia tume imekubaliana..sema wamepiga kura wengi wape..matumizi ya demokrasia tu..haimaanishi hawakutofautiana kimawazo
Acha uongo! Kazi ya Tume ilikuwa kukusanya maoni ya wananchi na kuyawasilisha na siyo kutoa maoni yao! Kwa hiyo demokrasia haihusiki hapo!
 
Hiyo soda ni ya mwaka 1987,alienda nayo studio mwaka huu? Sijaelewa vizuri
Nami nilimsikia na kumuona kupitia hicho kipindi cha dk 45 ITV,alikuwa yupo na SODA aliyopewa na Bonite Bottles,soda ya PILI kuzalishwa mwaka 1987,ya KWANZA alipewa Hayati Ali Hasan Mwinyi

Ila yote kwa yote Jaji Warioba,atabaki SHUJAA wangu,kazi aliyofanya na TUME yake,ilikuwa ni KAZI TUKUKA..Kongole kwake !
Ya
 
Leo jumatatu katika kipindi cha Dakika 45 cha ITV kinachoongozwa na Farhia Middle aliyekuwa Waziri wa Kilimo na pia kada maarufu wa CCM amekiri kuhujumu katiba ya Warioba ambayo ilipendekeza serikali tatu.

Itakumbukwa Kimiti alikuwa mjumbe wa Tume ya Warioba iliyozunguka nchi nzima kutafuta maoni ya wananchi juu ya katiba mpya. Aidha alikuwa Mwenyekiti wa kamati namba 16 ndani ya Bunge la katiba.

Katika kipindi cha leo amesema aliona serikali tatu zitaleta mgawanyiko na hatimaye kuvunjika kwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar na hivyo kwenda kinyume na makubaliano ya Tume ya Warioba. Kwa hiyo alishiriki kuwashawishi wajumbe wa kamati yake namba 16 kupinga mapendekezo ya Tume ya Warioba.

Pole sana Mzalendo Warioba kwa kusalitiwa wa wajumbe wanafiki wa Tume yako!
Wazee wa aina hii ndiyo waliofikisha taifa kusiko husika. Sijuhi uko kwenye Baraza la mawaziri nako alikuwa akiwasaliti wenzae? Mtu yuko kwenye tume na mmekubaliana na kutoa ripoti. Wakati wa utekelezaji unawageuka na kuwasaliti wenzako. Ni sawa tu na alivyofanya Kikwete. Na tunao wengine wengi wa aina hii, anzia kwa Kabudi, Bashiru na Polepole
 
Back
Top Bottom