Paul Kimiti akiri kuhujumu Katiba ya Joseph Sinde Warioba

Wazee wa aina hii ndiyo waliofikisha taifa kusiko husika. Sijuhi uko kwenye Baraza la mawaziri nako alikuwa akiwasaliti wenzae? Mtu yuko kwenye tume na mmekubaliana na kutoa ripoti. Wakati wa utekelezaji unawageuka na kuwasaliti wenzako. Ni sawa tu na alivyofanya Kikwete. Na tunao wengine wengi wa aina hii, anzia kwa Kabudi, Bashiru na Polepole
Kwenye Baraza la mawaziri atakuwa alikuwa anakubali kila hoja ya Rais na kutikisa kichwa kwa nguvu ili ampendeze!
 
Kueleza ukweli kinagaubaga, bayana tena hadharani, sio usaliti ni ungwana na uzalendrooo wa kiwango cha juu sana [emoji205]
Tlaatlaah, tofautisha unafiki na kueleza ukweli. Kama hasingekuwa kwenye tume ningekubaliana na wewe, lakini aliwezaje kuigeuka ripoti ya tume ambayo na yeye alikuwa sehemu ya hiyo ripoti?
 
Leo jumatatu katika kipindi cha Dakika 45 cha ITV kinachoongozwa na Farhia Middle aliyekuwa Waziri wa Kilimo na pia kada maarufu wa CCM amekiri kuhujumu katiba ya Warioba ambayo ilipendekeza serikali tatu.

Itakumbukwa Kimiti alikuwa mjumbe wa Tume ya Warioba iliyozunguka nchi nzima kutafuta maoni ya wananchi juu ya katiba mpya. Aidha alikuwa Mwenyekiti wa kamati namba 16 ndani ya Bunge la katiba.

Katika kipindi cha leo amesema aliona serikali tatu zitaleta mgawanyiko na hatimaye kuvunjika kwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar na hivyo kwenda kinyume na makubaliano ya Tume ya Warioba. Kwa hiyo alishiriki kuwashawishi wajumbe wa kamati yake namba 16 kupinga mapendekezo ya Tume ya Warioba.

Pole sana Mzalendo Warioba kwa kusalitiwa wa wajumbe wanafiki wa Tume yako!
Mtu kama huyu anatakiwa akamatwe afungwe, sisi hatuitaki Zanzibar
 
Tlaatlaah, tofautisha unafiki na kueleza ukweli. Kama hasingekuwa kwenye tume ningekubaliana na wewe, lakini aliwezaje kuigeuka ripoti ya tume ambayo na yeye alikuwa sehemu ya hiyo ripoti?
wacha nikufunue fikra kidogo apo. ...

nadhani jambo hili wewe pamoja na wengine wengi wasiokua na ufahamu na uelewa wa kutosha juu ya mambo haya, wanadhani ati yote yaliyokuwamo kwenye rasimu ya warioba eti wajumbe wote wale walikubaliana nayo 100%. That's wrong, haikua hivyo, na haiko hivyo na haitawahi kua hivyo, that one you must understand..🐒

mnajadiliana, mnaeleweshana, mnaeleweshana, mnarekebishana na completely mnaweza kukubaliana au kutokubaliana kabisa on some issues, but kwa ungwana, utashi na uzalendrooo wenu mnaweza tafuta namna ya kufikia maridhiano na hatimae maafikiano, kwa labda wingi au uchache wa kura za wajumbe mliopo, halafu mnasonga mbele kwenye jambo lingine 🐒

kutokubaliana na jambo fulani si unafiki, huenda ulipotoshwa awali, ama ni slow learner umekuja kuelewa uzuri au ubaya wa jambo hilo na sasa umeerevuka na huwezi kustahimili kuishi kwenye upotovu huo 🐒

ni ambaye hajakomaa kifikra, dhaifu hoja na ushawishi, na mwenye majibu yake mfukoni ndio pekee anaeweza ita maoni, mitazamo au msimamo wa mwingine unafiki, akidhani wote wanafikiri kama yeye, no haipo hivo🐒

The Muzee yuko sahihi, na nadhani ameatract mamilioni ya waTz kuungana na mtazamo wake na hivyo jambo hili kuamuliwa kirahisi sana siku za usoni 🐒
 
Tume haikutakiwa kukubaliana au kutokubaliana na maoni ya wananchi. Kazi ya Tume ilikuwa kukusanya maoni na kuyawasilisha na siyo kuweka mbwembwe zao. Hivyo katika kamati alitakiwa kuwafafanulia wenzake ambao hawakuwa katika Tume nini makundi mbalimbali ya wananchi waliyataka kuingizwa katika katiba mpya.
 
maoni ya wanainchi ni pamoja na maoni yake mwenyewe, ambayo ndio hayo yanaleta joto kwa wanainchi wengine wanaotofautiana na maoni yake 🐒
 
sina haja ya malipo hata kidogo napodhihirisha ukweli bayana na kinagaubaga 🐒🐒

daima ukweli na uzalendo hauhitaji malipo unajilipa wenyewe 🐒

nitawaombea kwa Mungu, viongozi wa nchi hii bure, na nitawasilisha maoni na mtazamo wangu kwa jamii dhidi ya viongozi wa nchi bure 🐒

Mungu ampetupatia vyote tulivyo navyo, mathalani karama, uwezo na vipaji mbalimbali bure, yafaa basi tutoe bure, tena kwa ukarimu 🐒
Ripoti ya CAG nayo utaitetea? Au ndio tupotezee
 
Leo jumatatu katika kipindi cha Dakika 45 cha ITV kinachoongozwa na Farhia Middle aliyekuwa Waziri wa Kilimo na pia kada maarufu wa CCM amekiri kuhujumu katiba ya Warioba ambayo ilipendekeza serikali tatu.

Itakumbukwa Kimiti alikuwa mjumbe wa Tume ya Warioba iliyozunguka nchi nzima kutafuta maoni ya wananchi juu ya katiba mpya. Aidha alikuwa Mwenyekiti wa kamati namba 16 ndani ya Bunge la katiba.

Katika kipindi cha leo amesema aliona serikali tatu zitaleta mgawanyiko na hatimaye kuvunjika kwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar na hivyo kwenda kinyume na makubaliano ya Tume ya Warioba. Kwa hiyo alishiriki kuwashawishi wajumbe wa kamati yake namba 16 kupinga mapendekezo ya Tume ya Warioba.

Pole sana Mzalendo Warioba kwa kusalitiwa wa wajumbe wanafiki wa Tume yako!
Sasa hapo ndio amehujumu?
 
Back
Top Bottom