Paul Kimiti akiri kuhujumu Katiba ya Joseph Sinde Warioba

Kwahiyo anafurahia hicho kitendo alichokifanya ??!
 
Tlaatlaah, tofautisha unafiki na kueleza ukweli. Kama hasingekuwa kwenye tume ningekubaliana na wewe, lakini aliwezaje kuigeuka ripoti ya tume ambayo na yeye alikuwa sehemu ya hiyo ripoti
 
Naamini muungano wa sasa ni mbovu kuliko uliopendekezwa na Tume ya warioba kwa sababu pande zote mbili zinakosa haki iliyokamilika.Aidha,toka tumeungana hakujatokea nchi jirani Afrika kuiga muungano huu; jambo linaloashiria madhaifu yaliopo.Tafuteni maoni ya wanan chi muone!
 
Ukiwa mjinga utadhani unajua mambo kuliko wengine. Ni hivi, kamati iliundwa kutafuta maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya, na moja hoja kwenye adidu rejea lilikuwa swala la muungano. Baada ya maoni kukusanywa wajumbe walikuwa na wajibu wa kuyachambua na kutoa mapendekezo. Kamati kama kitu kimoja mmekaa, kujadili na kutoa mapendekezo kama timu moja, ni upuuzi uliopitiliza kugeuka wenzako kwa kile ulichokisaini wenyewe. Alikuwa wapi kuwaelimisha wenzake hadi wakamuelewa? Na kama hayo maoni yake yalikataliwa kwa wingi wa wenzake ktk kamati kulikuwa na options mbili, kujitoa kwenye hiyo kamati au kukaa kimya, siyo kuzunguka kwa mlango wa nyuma.
 
nimeeleza sana mwanzoni kwamba, kua katika tume au kamati moja haimanishi mnakubaliana na kila kitu miongoni mwenu..
ukiwa mzalendo utakua willing kuwin in some isues, lakini pia utakua willing to loose on some issues....

na ndivyo ambavyo tume ya katiba na kamati zake mbalimbali waliweza kufikia muafaka hata kuandika ile rasimu...
hapakuwapo aliekua anang"ang"ania jambo fulani ati, liwe kama anavotaka yeye tu, au kama ambavyo wale wajumbe wa bunge la katiba walio susa na kutokomea na fedha za walipa kodi walifanya.....

wenye tabia ya kujitoa, kususa, kudekadeka na kuzira wanafahamika....

mtu makini, muungwana, mahiri, mbobevu, mzalendo na mwana demokrasia mkomavu kama yule hawezi kubabaika na kufanya mambo ya fedheha ati kujitoa, kujiuzulu, kukaa kimya au kususa....

kwanza amsusie nani mbaba wa watu yule?

waliotumwa na vyama vyao, na majibu yao mfukoni pekee ndio wanaoweza kufanya hayo mambo ya kuzira na kususa....
 
Labda inafaa kwa sasa, ndio maana amekiri kosa lake.
 
Sijuhi ni kwann unajikanyagakanyaga. Unatuambia mpaka kufikia hatua ya kutoa rasimu ni baada ya majadiliano, sawa nakubali. Kwa nini mwisho wa siku uwageuke wenzako kwa mlango wa nyuma hata kama hukukubaliana na walio wengi ndani ya tume juu ya hoja fulani? Tuambie, huyo Warioba na wenzie unadhani wao walikuwa wakibaliana na kila hoja ktk ile rasimu? Jibu ni hapana, kuna sehemu walikuwa wakitofautiana, lakini baada ya rasimu hakuna aliyegeuka wenziwe.

Waliosusa bunge la katiba, hawakukubaliana na uhuni wa kiini macho cha kusigina maoni ya wananchi. Je, waliobaki ndani hawakulipwa, kwann uhoji? Je, kwa kazi ipi walioifanya....na wakati walikuwa wengi wenye uwezo wa kupitisha chochote. Usanii tu na kutumia hovyo fedha ya wavuja jasho.
 
Ni kweli na kumbuka wakati ule aliyekuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa alikuwa mtu wa kwao Rukwa Marehemu Walingozi.
Nyie ni Wahenga.
 
maoni ya wanainchi ni pamoja na maoni yake mwenyewe, ambayo ndio hayo yanaleta joto kwa wanainchi wengine wanaotofautiana na maoni yake 🐒
Kazi ya wajumbe wa tume haikuwa kwasilisha maoni yao wenyewe, bali maoni ya wananchi, bila kuongezea maoni yao wenyewe.
 
walosisa bunge la katiba, hawakua wangwana kwao wenyewe binafsi, na kwa wanainchi kama ambavyo pia unaonyesha ungwana wakao kufifia kwa tone, rythm na style ya reply yako inavyo jieleza....

na hicho ndicho kinasababisha wTz kuchelewa kupiga hatua kwa haraka, bila sababu za msingi,
wakati iko bayana na dhahiri, shahiri kwamba unae msusia au kumziria yuko determined na yuko focused kuwatumikia na kuwahudumia wanainchi, ukadhani ataacha hiyo kazi muhimu sana na ati ababaike na wewe mwenye msimamo wako wa kulazimisha, ambao sio tu hauwezekani lakini pia hautekelezeki....

kila moja ana haki, na yuko huru kutoa maoni na mtazamo wake juu ya mambo mblilmbali bila kujali wengine wana maoni gani dhidi ya mambo hayo hayo....

hakuna kushurutishana, kulazimishana wala kutukanana kwa sabababu ya utofauti wa maoni na mtazamo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…