Paul Kimiti akiri kuhujumu Katiba ya Joseph Sinde Warioba

Yale yalikuwa maoni ya wananchi lakini CCM wakayatupilia mbali!
 
Na aliyekuwa makamu wa BMK ambaye mchakato ulipoishia anaujua kwanini atoe tena miaka 3 ya elimu ya katiba mpya?hii inadhihirisha kuwa Kimiti hakuwa peke ake.
 
Kila mmoja ana Uhuru wa kutoa maoni.....!!! unaongea kama hukuwepo kipindi cha utawala wa Magufuli akitumia vijana wake kama akina Makonda, Sabaya na task force ya wasiojulikana?

Kwa mzee Kimiti swala si kutoa maoni, tatizo hayo maoni kayatolea wapi na yeye alikuwa kwenye tume ipi. Kuna kitu kinaitwa "collective responsibility" sijuhi mwenzetu kinakupiga chenga?

Hata hao unaowasema kususia bunge kwa kutokukubaliana na maamuzi ya yasiyo kuwa na tija kwa wananchi, bado hayo maamuzi yakishapitishwa kwa wingi wa kura yanakuwa maamuzi ya Bunge zima siyo ya wale tu waliokubaliana nayo. Ni bahati mbaya mlikaririshwa na dikiteta Magufuli kwa kauli za "wabunge wenu walikataa kupitisha budget hivyo siwaletei maendeleo". No sense, walipa kodi ni wananchi wote bila kujali wanaongozwa na mbunge wa chama gani. Si kila budget hata kama haina maslahi kwa taifa ipitishwe kisa tu imeletwa bungeni. Nyie vijana mnahitaji elimu ya siasa.
 
Hata hao unaowasema kususia bunge kwa kutokukubaliana na maamuzi ya yasiyo kuwa na tija kwa wananchi, bado hayo maamuzi yakishapitishwa kwa wingi wa kura yanakuwa maamuzi ya Bunge zima siyo ya wale tu waliokubaliana nayo.

πŸ˜€sasa uanababaika na nini na mtu ambaye hakubaliani na wewe kwenye jambo fulani, hali ya kua unajua fika baadae jambo lile mnalotofautiana linakua la wananinchi na nyinyi wote?..

wewe unaelewa kabisa mambao jinsi yanavyopaswa kua lakini, nadhani umeamua tu kinuchatisha kujifurahisha.......
 
Ninachokushangaa wewe ni kukubaliana na Kimiti kwa kile alichokifanya nje ya tume ya Warioba. Tungesema kwamba hakujuwa, lakini huyu mzee amekuwa kwenye baraza la mawaziri muda mrefu. Si kwamba huwa kila mtu kule anakubali na kila jambo, lakini baada ya maamuzi huwa wanabanwa na kile nilichokwambia "collective responsibility". Nitaendelea kumshangaa kwa kuigeuka tume ambayo yeye alikuwa mjumbe.
 
Mzee Warioba alisema '' tulijadiliana na kubishana kwa muda mrefu hadi tulipopata suluhu''

Paul Kimiti ni mnafiki mkubwa. Alikuwemo ndani ya Tume na hakueleza chochote. Miaka zaidi ya 10 ndipo anatoka na kutueleza alikuwa ''snitch'! Huyu mzee kajivunjia heshima sana

Kilichotoka ndani ya Tume ni makubaliano ya pamoja kwa maana unapata na pia unapoteza ili kufikia muafaka

Kimiti anaposema kulikuwa na dalili za kuvunja Muungano ni Unafiki na uongo kwasababu hizi
Warioba( PM na VP), Salim Ahmed( PM), Mzee Butiku (Katibu wa Nyerere) waliridhia na walitoka kutetea walichokifanya, Kimiti ni nani katika Muungano.

Maelezo ya Kimiti hayawezi kutetewa kwa namna yoyote. Kwanza ni Mnafiki, pili ni snitch, tatu hana integrity na kubwa zaidi ni muongo. Mzee Kimiti angekaa kimya ingesaidia hii interview kajivunjia heshima

Kwa upande mwingine huyu Furahia Middle anasoma maswali hana uwezo wa kufuatilia na kumbana mtu
1. Angemuuliza kwanini kero zimemalizwa na SSH na siyo Watangulizi wake.
2. Nani alisimamia kero za Tanganyika
3. Kijana wa leo unamwambia Muungano una faida gani
4. Alikuwa ndani ya Tume kwanini hakupinga alisubiri kinafiki ndani ya Bunge
5. Kwanini alikaa kimya miaka 10
6. Faida za Muungano za kufundishwa mashuleni ni zipi, azitaje 2 tu.

Huyu mtangazaji wa ITV kafeli sana kama wanavyofeli Watangazaji wetu, hawafanyi ''homework' wala hawana weledi wa mada. Wakibabaishwa kidogo wananywea

Ni kama wale wa Global radio waliambiwa na mwenezi wa CCM Zanzibar kwamba Katiba inataka Zanzibar ipewe mgao wa pesa kwa Matrilioni.
Watangazaji wale hawakuuliza katiba ipi na kifungu kipi, walikaa kimya na kuacha uongo utamalaki

JokaKuu Pascal Mayalla
 
we ninachokiona kwako sasa ni kulazimisha au kutaka mawazo na maoni ya huyo mzee yawe samabamaba na maoni na mtazamo wako na pengine wa chama chako kitu ambacho si sawa na hakiwezekani....

na wala hakuna sababu ya kughadhabishwa na amabae anatofautiana na wewe bana...

kwahiyo kukiwa na collective responsibility nazuiwa kua na maoni na mtazami yangu binafsi?

sikuhitaji kung"ang"ania msimamo wangu kwasababu ungekwamisha kupatikana huyo document inaitwa ya warioba,

niliamua kukaa kimya na kutokua mbishi nikaweka uzalendo mbele, ili mambo yasikwame lakini sasa nimepata fursa kusema mtazamo wangu juu ya jambo hilo inakua nongwa πŸ˜€
 
relax bas,

kuwa na staha na muungwana kidogo...
 
wasingetoa maoni yao kuchakata maoni ya wanainchi wasingelipata ile kitabu...
Kazi yao ilikuwa ni kutafasiri tu(kuchakata)maoni ya wananchi na kuyaweka kwny bunge la katiba, siyo kuweka maoni yao.

Wao walikuwa ni wajumbe, kazi ya mjumbe ni kufikisha ujumbe, sio kuongezea maneno yake.
 
Kazi yao ilikuwa ni kutafasiri tu(kuchakata)maoni ya wananchi na kuyaweka kwny bunge la katiba, siyo kuweka maoni yao.

Wao walikuwa ni wajumbe, kazi ya mjumbe ni kufikisha ujumbe, sio kuongezea maneno yake.
it is amazing πŸ’πŸ’

kama unaweza toa tafsiri ambayo haipo bila maoni, well and good πŸ’
 
relax bas,

kuwa na staha na muungwana kidogo...
Nimecheka sana, sasa ndugu yangu jina mbadala la Mnafiki ni lipi?
Hawa Wazee hawana stara sasa tuwape ipi? Fikiria mzee huyu anakuwa 'snitch' utamwita Muungwana

Warioba, Salim, Butiku hawa ni Vijana wa Mwalimu mwenye Muungano, leo Kimiti ''anawachoma'' eti wanataka kuvunja muungano. Halafu hakufanya hivyo kwenye Tume, alitoka nje kisha kuwasaliti wenzake.

Mnafiki ni Mnafiki tu hana jina jingine.
 
Sahihi kabisa, hakuna jambo la kuongeza kwenye ufafanuzi wako. Huyu mzee kidogo ningemwelewa kama hii miaka 10 baada ya jambo lenyewe kumalizika ndio aseme jinsi alivyotofautiana na wajumbe wenzie kwenye tume juu ya muungano. Lakini kutuambia aliitisha watu pembeni kupinga kile kile kilichopitishwa na tume na yeye akiwemo ni unafiki wa hali ya juu.
 
Hawa ndo wazee walosababisha watu waseme siasa ni mchezo mchafu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…