Uchaguzi 2020 Paul Makonda achukua fomu ya Ubunge Kigamboni, kupitia CCM

Uchaguzi 2020 Paul Makonda achukua fomu ya Ubunge Kigamboni, kupitia CCM

Dah hapa ndo jiwe hua anajichanganya. Mbona wengine wote walilazimika kujiuzulu nyadhifa nyingine ili wagombee ubunge huyu imekuaje? Naanza kushawishika kuna jambo la ziada nyuma ya uswahiba wa hawa watu wawili
Yeye alisema hapo nilipokuweka ndio nataka kukutumia au msaada wako ??
Mwisho wa kunukuu, sasa kama RC kaenda kuchukua fomu labda Raisi ajaye ndiko anakotaka awe
 
Bila kujiuzulu Ukuu wa Mkoa?

Kwa hiyo ni Mkuu wa Mkoa pekee nchi nzima aliechukua fomu akiwa na madaraka yake yote ya Ukuu wa mkoa.

Mnaweza kuhisi amekuja kwenye kampeni kumbe yupo kwenye ziara ya kikazi, halafu mkaonyesa vidole vyenu vya Peopleeeeesss.

Na atapiga kampeni huku akiwa na Cheo Chake Cha Ukuu wa Mkoa kama Kawaida.

Halafu Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi yupo chini ya Mkuu wa Mkoa.

Kuna hatari Makonda akawa Mbunge, Mkuu wa Mkoa na Waziri kwa wati mmoja.

Chalamila, Ole Sabaya mnajisikiaje huko mliko.??
Moja ya mapungufu ya Magufuli ni kumuogopa Makonda.
 
Tunategemea ajiuzulu la sivyo hii itakuwa ni double standard kwa JPM na uongozi hovyo wa awamu hii.
 
Hatimaye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa sana Paul Christian Makonda achukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Kigamboni.

...
IMG-20200715-WA0030.jpg
 
Hatujasikia akifanyiwa replacement, na Mnyeti pia kachukua form hatusikii replacement yao.

Wengine wakigusa tu unasikia wametumbuliwa.

Mshikaji kwa double standard hajambo.

Mnyeti na Makonda ni wasukuma.

Mnyeti anagombea misungwi halaf kitwanga rafiki yake sana sijui nae kachukua fomu
 
Ila inavyoonekana ataondolewa, lakini kimkakati, kwani si miezi miwili tu imebaki? Akishinda au akishindwa atapewa cheo tu kwa namna yoyote si unajua tena Afrika yetu...?
 
Manyara yameshapita hayo masaa 48,mbona hausemi upendeleo?
Huyo wa Manyara kawekwa kama kinga tu ili mtoto mpendwa akichukua basi kuwe na visingizio vya kishenzi kama hicho chako..

Hawa wote wasipotenguliwa basi utakuwa ni upendeleo kwa maana yeye mwenyewe alisema viongozi aliowateua wakitaka kugombea waombe ruhusa na yeye atawapa na kuzijaza nafasi zao. Sasa inakuwaje hao wawili hawatenguliwi??

BTW wote ni Wasukuma na serikali hii ni ya kisukuma..
 
Huo Waraka unawahusu employees wa kawaida na SIYO POLITICAL APPOINTEES jamani mbona mnataka kulazimisha mambo. Hebu nendeni mkausome sawasawa na kujua ukweli wa mambo yalivyo.
Mkuu wa Mkoa ni kiongozi Mkuu wa serikali katika Mkoa waraka huo unamhusu mwaka 2010 wapo wakuu wa mikoa na wilaya wengi walichukua fomu za CCM kuomba ridhaa ya chama hicho kugombea ubunge kupitia CCM katika kipindi cha kura za maoni waliomba tu ruhusa na ambao walipitishwa na chama kupepersha bendera walijiuzuru nafasi zao na wale ambao chama hakikuwapitisha walirudi kazini tatizo la sasa ni hiyo kauli ya Rais na mchanganyiko wa mambo hivi naye DAS naye ni poltical appointee?
 
Tunategemea ajiuzulu la sivyo hii itakuwa ni double standard kwa JPM na uongozi hovyo wa awamu hii.
Double std haijaanza leo wala jana, kama Magu akishinda tena tegemea kuona double std ya hatari kuliko hii ya sasa.
 
Back
Top Bottom