Yeye alisema hapo nilipokuweka ndio nataka kukutumia au msaada wako ??Dah hapa ndo jiwe hua anajichanganya. Mbona wengine wote walilazimika kujiuzulu nyadhifa nyingine ili wagombee ubunge huyu imekuaje? Naanza kushawishika kuna jambo la ziada nyuma ya uswahiba wa hawa watu wawili
Waziri mtarajiwa wa habari, michezo na sanaa.
Moja ya mapungufu ya Magufuli ni kumuogopa Makonda.Bila kujiuzulu Ukuu wa Mkoa?
Kwa hiyo ni Mkuu wa Mkoa pekee nchi nzima aliechukua fomu akiwa na madaraka yake yote ya Ukuu wa mkoa.
Mnaweza kuhisi amekuja kwenye kampeni kumbe yupo kwenye ziara ya kikazi, halafu mkaonyesa vidole vyenu vya Peopleeeeesss.
Na atapiga kampeni huku akiwa na Cheo Chake Cha Ukuu wa Mkoa kama Kawaida.
Halafu Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi yupo chini ya Mkuu wa Mkoa.
Kuna hatari Makonda akawa Mbunge, Mkuu wa Mkoa na Waziri kwa wati mmoja.
Chalamila, Ole Sabaya mnajisikiaje huko mliko.??
Dar asipoteuliwa RC mpya ndani ya masaa 48 huu utakuwa upendeleo wa dhahiri kabisa..
...Hatimaye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa sana Paul Christian Makonda achukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Kigamboni.
Hatujasikia akifanyiwa replacement, na Mnyeti pia kachukua form hatusikii replacement yao.
Wengine wakigusa tu unasikia wametumbuliwa.
Mshikaji kwa double standard hajambo.
Mnyeti na Makonda ni wasukuma.
Na katambi je?
Kupata ulaji bila jasho. Shughuli ya wabunge wengi ni kukubali na kusifia. Hiyo ni kazi ndogo tu ukilinganisha na kipato.ubunge una nini jamani ?!
Peke yake ajiuzulu au ?wengine mnawaogopa?Tunategemea ajiuzulu la sivyo hii itakuwa ni double standard kwa JPM na uongozi hovyo wa awamu hii.
Kwahiyo wasukuma wana exception sio?? Katambi, Makonda, MnyetiNa katambi je?
Huyo wa Manyara kawekwa kama kinga tu ili mtoto mpendwa akichukua basi kuwe na visingizio vya kishenzi kama hicho chako..Manyara yameshapita hayo masaa 48,mbona hausemi upendeleo?
Mkuu wa Mkoa ni kiongozi Mkuu wa serikali katika Mkoa waraka huo unamhusu mwaka 2010 wapo wakuu wa mikoa na wilaya wengi walichukua fomu za CCM kuomba ridhaa ya chama hicho kugombea ubunge kupitia CCM katika kipindi cha kura za maoni waliomba tu ruhusa na ambao walipitishwa na chama kupepersha bendera walijiuzuru nafasi zao na wale ambao chama hakikuwapitisha walirudi kazini tatizo la sasa ni hiyo kauli ya Rais na mchanganyiko wa mambo hivi naye DAS naye ni poltical appointee?Huo Waraka unawahusu employees wa kawaida na SIYO POLITICAL APPOINTEES jamani mbona mnataka kulazimisha mambo. Hebu nendeni mkausome sawasawa na kujua ukweli wa mambo yalivyo.
Double std haijaanza leo wala jana, kama Magu akishinda tena tegemea kuona double std ya hatari kuliko hii ya sasa.Tunategemea ajiuzulu la sivyo hii itakuwa ni double standard kwa JPM na uongozi hovyo wa awamu hii.
Utopolo..JPM asipoteua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hakika itakuwa ni zaidi ya....!