MENGELENI KWETU
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 9,552
- 24,166
Huu uzi unapaswa ujitegemee lakini mods wameshauunganisha..i dont know why..Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amechukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Kigamboni, kitendo hicho kinaweza kuibua upya madai yake ya kughushi vyeti vya elimu na nyaraka zingine.
Kuna tuhuma kuwa Paul Makonda alitumia vyeti vya Daud Albert Bashite. Siasa ni mchezo mchafu, inaweza kupelekea kuwekewa pingamizi kwenye Tume ya Uchaguzi au ushindi wake kuja kupingwa mahakamani.
Mwaka 1995 Ramadhan Ali Kihiyo alishinda ubunge jimbo la Temeke kwa tiketi ya CCM, baadae NCCR Mageuzi ilienda Mahakamani kupinga kuwa Kihiyo alitumia vyeti visivyo vyake kuwania ubunge. Wakati kesi ikiwa inaendelea Mahakama kuu Kihiyo alijiuzulu ubunge.
Pls Mkuu Maxence Melo and your team, tunaomba sana sio kila kitu kiwe kinaungwa..mfano content nzuri ya uzi kama huu inapotea.