Paul Makonda aiomba Mahakama siku 21 ili ajibu hoja za Kubenea

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
1646305366114.png

Picha: Paul Makonda

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kinondoni impe muda wa kujibu maombi yaliyofunguliwa na mwanahabari, Saed Kubenea ya kutaka kumfungulia kesi ya jinai.

Maombi hayo yaliwasilishwa Machi 2, 2022 mbele ya Hakimu Aron Lyamuya na Wakili wa Makonda, Goodchance Reginald, aliyedai amechelewa kupata wito huo kwa kuwa ameupata kupitia vyombo vya habari.

"Mteja wangu ameni-engage hivi karibuni kwamba hakupata taarifa yoyote ya summons (wito), ingependeza tungepata summons na muda wa kujibu," alidai Wakili Reginald.

Ombi hilo lilipingwa na Hekima Mwasipu, Wakili wa Kubenea aliyedai hajaiambia mahakama Makonda alipataje taarifa hadi amemtuma afike kumwakilisha mahakamani huko.

Wakili Reginald alijibu pingamizi hilo akidai: "Mteja wangu alipata hizi habari kupitia vyombo vya habari, akaona si vyema yeye alikuwa kiongozi wa serikali, akaona ni vyema alete wakili lakini summons hajapewa."

Kutokana na maombi hayo, Hakimu Lyamuya alimpa siku 21 Makonda ili kuwasilisha hati kinzani dhidi ya maombi hayo yaliyofunguliwa na Kubenea.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Subira Mwalumuli, alidai mahakamani huko kuwa wajibu maombi namba moja na mbili, ambao ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), wanatarajia kuleta mapingamizi ya awali dhidi ya maombi hayo.

"Shauri liko kwa ajili ya kutajwa lakini pia tarehe hii ilipangwa kuletwa hati kinzani kwa wajibu maombi wa kwanza na wa pili wameleta taarifa ya kutoa pingamizi la awali na pingamizi hili la awali ni juu ya shauri lililo mbele ya mahakama yako. Kwa hivyo, tunaomba kutoa hiyo taarifa mbele ya mahakama yako," alidai Wakili Mwalumuli.

Hakimu Lyamuya aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 25, mwaka huu, huku upande wa wajibu maombi namba moja na mbili, yaani DPP na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) wakidai wanakusudia kuleta pingamizi la awali juu ya maombi hayo.

Katika kesi hiyo, Kubenea anawakilishwa na jopo la mawakili wakiongozwa na Nyaronyo Kicheere na Hekima Mwasipu.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Makonda anadaiwa kuwa siku ya tarehe 17, Machi 2017, akiwa na watu waliobeba silaha za moto, alivamia kituo cha Clouds TV na kumwagiza mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu kurusha video inayomwonyesha mwanamke (jina tunalihifadhi) aliyedaiwa kuonekana akifanya tendo la ndoa na mmoja wa viongozi wa dini nchini (jina tunalihifadhi).

Kwa mujibu wa hati ya kiapo ya Kubenea, anadai kitendo cha Makonda kuvamia kituo cha televisheni, tena akiwa ameongozana na askari waliobeba silaha za moto, ni kinyume cha Sheria ya Kielektroniki na Posta ya Mwaka 2010.

Maombi ya kutaka kumshtaki Makonda yaliwasilishwa mahakamani chini ya kifungu cha 99 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Sura ya 20.

Mbali na Makonda, wengine walioitwa mahakamani ni DCI na DPP wanaotuhumiwa wameshindwa kuchukua hatua za kumfungulia mashtaka ya jinai mtuhumiwa huyo.

Source: Nipashe
 
Dpp dci wakikutwa na hatia inakuwaje? Kesi ya hovyo sana
 
Kubenea anataka kuuza magazeti yake tu hamna kesi
 
Mh! Kumbe ni kesi ya kujibiana hoja mkiwa nyumbani tu, kumbe hamna kitu pale.
 
Mie ni me uliza dpp na dci wakikutwa na hatia adhabu yao ni ipi?
 
View attachment 2137352

Hapa ni nguvu ya wauza madawa na mashoga ndio wanamsakama makonda kwa baraka za wahuni wanaodhibiti awamu inayojiita ya sita... JPM rip
 
Back
Top Bottom