Paul Makonda aipasua CCM, kigogo ndani ya chama atishia kujiuzulu

Paul Makonda aipasua CCM, kigogo ndani ya chama atishia kujiuzulu

Rais Samia amechanganyikiwa kwenye hili. Repercussions zake ni mbaya sana. Kuna methali inasema "adui mwombee njaa"

Hapa naona maadui wa Samia wamefanikiwa kumuombea NJAA. Makonda hakufaa kurudi kwenye utumishi wa chama wala Serikali bali alipaswa kuwa gerezani tu. Hii ni DHIHAKA kubwa kwa Watanzania

Ila iko siku Paul Makonda ataingia tu gerezani na kutumikia kifungo kwa maovu yake
Naunga mkono hoja 👍👏
 
Makonda kafanya kile ambacho CCM walitaka, kufanya watu waiongelee CCM sana
But, it is negative publicity.

Ndio, tunaiongelea CCM au Makonda lakini ni taswira hasi.

Paul Makonda atakuwa ndio the face of CCM from now on going forward.

Ukitaja neno Makonda utakumbukwa utawala wa mabavu!

Mada zitakuwa ni mbili tu, Bandari, Makonda. Massive distraction on the CCM agenda.
 
HALI NDANI YA CCM siyo shwari baada ya Paul Makonda kuteuliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM katika kikao ambacho kilijaa masikitiko na lawama nyingi sana kwa nini na sababu zipi zinafanya apewe hiyo nafasi. Wajumbe wengi wa NEC wametafsiri kuwa ubabe ukitumika kumsimika kwenye nafasi hiyo na wakidai hana sifa za kuwa Mwenezi wa CCM kuna ambao walidiriki kusema bora angeridishwa Polepole au Shaka lakini siyo Makonda.

Chanzo chetu toka ndani ya kikao cha NEC zinasema wa kwanza kabisa kupinga uteuzi wa Makonda alikuwa ni waziri mkuu mstaafu Mzee Mizingo Pinda ambaye alisema " kijana huyu katukana wastaafu wote na kafanya kila aina ya makosa na uovu lakini leo anafaaje kuwa na cheo kikubwa kiasi hiki ndani ya chama" Pinda aliendelea kusema kama kuna ulazima sana wa kurudishwa kwenye serikali au kupewa madaraka basi atafutiwe cheo kingine lakini siyo kuwa mwenezi wa chama kwa sababu ana historia chafu na ya hovyo sana ndani ya chama na nje ya chama na kwa watanzania CCM haitaeleweka kuteua mtu mhalifu kiasi kile kuwa kiongozi tena wa nafasi ya mwenezi.

Hali ilikuwa mbaya zaidi pale wajumbe wengi walipoonekana kutoridhishwa na kuletwa jina la Makonda na wengine mpaka wakaonya kwa nini kunakuwa na mabadiliko ya nafasi ya Katibu Mwenezi wa chama mara tatu ndani ya miaka 2 tu? Kuna mjumbe alihoji kuwa "mwenyekiti ulituletea Shaka ulipoingia,baada ya muda ukamtoa ukamleta Mjema na sasa unamtoa unamleta Makonda shida ni nini"

Baada ya kuona majibizano ni makali sana na wajumbe hawataki kabisa jina la Mkonda tunataarifiwa kuwa Mwenyekiti akaamua kura ipigwe kwa majina mawili aliyopendekeza ambayo yalikuwa nai jina la CHALAMILA na MAKONDA na baada ya kupigwa kura Makonda akamzidi CHAKAMILA kwa kura moja na akawa mwenezi kama ulivyotangwazwa.

Baada ya kikao cha NEC tunaarifiwa Kinana na JK na kundi la vjana wao wanaojiita wamekulia kwenye chama walikubaliana kukutana Dar Es Salaam nyumbani kwa Kinana na kikao kilifanyanyika na moja ya mambo waliyoazimia ni kuwa MAKONDA PAUL hafai kuwa Mwenezi wa CCM na watahakikisha kazi yake inakuwa ngumu sana na wameshaanza chini kwa chini kupeleka sumu mikoani na wilayani kuwashawishi wana CCM kutompa ushirikiano atakapoanza kuzunguka mikoani na mawilayani kwa ajili ya kukitangaza chama.

Suala la pili ni kuwa wamempa jukumu Chenge kuhakikisha kanda ya ziwa CCM inakataliwa kwa kiasi kikubwa na dalili zianze kuonekana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 ili mwaka 2025 kwa pamoja wamtake mwenyekiti wao apishe mtu mwingine asimame kwenye urais kwa kuwa chama kimemkataa na kimepasuka kwa sababu ya maamuzi yake.

Kinana kapewa jukumu la kujiuzulu umakamu uenyekiti kabla ya mwezi December 2023 na aweke wazi kuwa hakubaliani na mwenyekiti kwenye maamuzi mengi na hasa ya kumteua Makonda kuwa Katibu Mwenezi na kuwa hakumshirikisha na hivyo bora akae pembeni kulinda heshima yake na heshima ya chama.

Kwa hiyo muda wowote kuanzia sasa Kinana ataomba kujiuzulu umakamu mwenyekiti wa chama na kukaa pembeni sasa kuratibu mipango ya kumuondoa Rais 2025 akishirikiana na akina Chenge na JK na January Makamba yeye kapewa jukumu la kukusanya fedha za kukamilisha mipango hiyo na anashirikiana na Luhanga Mpina sasa kuoroshesha na kuzunguka majimbo yote ya kanda ya Ziwa ambayo CCM ni lazima ishindwe ili kuwe na sababu ya kumtaka mwenyekiti wao asiwe mgombea 2025 na kwa kifupi wanajipanga kufanya mapinduzi na hawataki Rais Samia awe mgombea 2025.

Sasa wenye kusikia wasikie na wenye kukaa kimya wakae kimya lakini HABARI NDIYO HIYO..

#KigogoMedia

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh 🙄 ! Mambo mazito haya kama ni kweli !! Ngoja Tusubiri tuone !!
 
Tumesoma gazeti lako la Leo Alhamisi October 28 mpaka November 01.

Umeandika
"Makonda Aipasua CCM!"
Ukweli ni kwamba wewe na Nape Nnauye hamtakaa mfurahie Mafanikio yoyote ya Makonda!

Tunajua jinsi Kundi la Nape na January lilivyokutumia wewe Said Kubenea kufungua kesi lukuki dhidi ya Makonda!

Tunajua jinsi ulivyofutwa machozi kwa kufunguliwa magazeti yako ya Mwanahalisi na Mawio!

Pia tunajua kwamba Kigogo unayemficha jina kwenye gazeti lako la Mwanahalisi kwamba amepinga uteuzi wa Makonda ni Nape Nnauye!

Sasa anatishia nyau kujiuzuru chama as if yeye ni ngome ya chama! Wakati tunajua Nape ni mojawapo ya wanasiasa wa CCM aliekalia kuti kavu jimboni kule anakowakilisha ilhali si mzaliwa wala mkuliaji wa hapo Mtama!

Nawashaurini enyi team roho mbaya mkae mtulie! Hatuipendi CCM ndiyo!
Lakini pia tunawachukia watu kariba ya Nape, Makamba,Kinana na team nzima iliyoko sambamba na maburushi kuifilisi nchi hii.

Lakini pia muelewe kwamba CCM ni taasisi ya wananchi ingawa kwa sasa imetekwa nyara.

Tuonane 2025 kwenye maamuzi magumu toka pande za Pwani ya Ziwa Magharibi. Polepole tutaheshimiana tu!
Naunga mkono hoja,ni kweli kbs,mie ni mwana ccm,lkn ninaichukia mno ccm kwa sababu ya hao vijana wapigaji,Nape,makamba na hata mwigulu pia,lkn pia ukimya wa mama unanikela na kunikatisha tamaa,hii nchi sio Mali ya ccm,hii nchi ni Mali ya watanzania woote.
 
Je Kuna ushaihid ya kuhusika kwake kwenye mauaji ya mtu yoyote au chuki kwake imetewala
Serikali ndiyo yenye nguvu ya kisheria ya kushughulikia tuhuma yo yote ya kijinai. Ukiomba ushahidi kama njia ya kumtetea mtuhumiwa haipendezi, unataka kila mtoa tuhuma awe mpepelezi? Hapo utawala bora utakuwa kaputi! Ila ni sahihi kama mtoa tuhuma akawa mtu wa kwanza kuonesha chimbuko la tuhuma kwenye chombo teule cha upelelezi.
 
View attachment 2793650
SASA ni rasmi kuwa CCM inaingia na iko kwenye mpasuko mkubwa sana baada ya habari za kuaminiki kutoka kwa watu wa karibu sana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana kuwa anajipanga kujiuzulu umakamu mwenyekiti wa chama hicho kikongwe na king'ang'anizi kutoka madarakani.

Kinana ameweka wazi kuwa anapinga uteuzi wa Paul Makonda kama Katibu Mwenezi wa CCM na pia ameweka wazi kwa watu wake wa karibu kuwa hakushirikishwa na kushauriana kabla ya uteuzi wa Makonda kitu ambacho amekitafsiri kuwa anadharauliwa na hayuko tayari kuburuzwa kwenye mambo ndani ya chama na hataki kuwa sehemu ya historia ya hovyo ndani ya chama hicho kumsafisha Paul Makonda ambaye ana uchafu mwingi sana aliofanya akiwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam.

Mtu huyu aliyetupa habari hizi za ndani ndani sana ambaye ni mmoja wa wale wanaofahamika kuwa vijana wa Kinana tena wa karibu sana, amesema tayari Kinana ameomba apointimenti ya kukutana na Mwenyekiti wa CCM kumueleza azma yake hiyo na amesikika kuwa atafanya kwa staili ile ile ya kipindi cha Magufulu alipojiuzulu kupinga ubabe na ukatili wa Magufuli.

Wakati hali ndani ya CCM ikiwa mbaya kiasi hiki tayari kumekuwa na mgawanyiko mkubwa sana ndani ya chama hicho na wazee wa chama na makada wanafikiria kufanya yasiyotarajiwa kwenye uchaguzi wa 2025 na zaidi wamefika mahali kuanza kuunda kambi za kumkwamisha Rais Samia kuwa mgombea mwaka 2025 na bahati mbaya sana kambi ya ya akina JK ile ile ya mwaka 2005 inasemekana imeshaingia kazini na wameweka wazi kuwa hawawezi kuona chama kinachezewa na akina Makonda kwa kiasi hiki na wanapinga kwa nguvu zote maamuzi ya Makonda kuwa Katibu Mwenezi wa CCM.

Mgawanyiko huu umekwanda mbali zaidi na tayari kundi hili la makada wanaanza kushawishi baadhi ya wastaafu wa vyombo vya usalama kuwa sehemu ya mpango huu ili kufanikisha azma yao hiyo ifikapo 2025. Kama jambo hili ni kweli kama tulivyoambiwa basi tunaweza kushuhudia kupasuka na kuzama kwa CCM kwa staili ya KANU kule Kenya na UNIP kule Zambia miaka mingi nyuma. Vyama hivi vilikuwa na nguvu sana toka uhuru wa nchi zao lakini zilikuja kuzama na kufa kimzahamzaha tu na mpaka leo havijanyanyuka tena.

SISI YETU NI MACHO NA TUTAWALETEA TAARIFA KADRI TUNAVYOAMBIWA NA KUZIPATA.. LAKINI KWA SASA TUMEKAAA PALEEEE [emoji1542]

#KigogoMediaUpdates
Kinana bonge la fisadi na mhujumu uchumi,sijui kwa nn mpk mda huu yupo uraiani,amesomba wanyama wetu na pembe za ndovu kwa mda mrefu sana na hao waarabu wake.
 
Nadhan kama angetaka muongeaji wa kupambana na wapinzani basi hata Chalamila angefaa ila kumrudisha huyu mwamba , naona ni kama kosa na sitegemei wengi kukubaliana na hili ndani ya chama.
Makonda ni zaidi ya kila kitu ccm,hakuna kitu kama makonda,said kubenea na Nape nnauye waendelee tu na hiyo ndoa yao ya jinsia moja.
 
Kinana bonge la fisadi na mhujumu uchumi,sijui kwa nn mpk mda huu yupo uraiani,amesomba wanyama wetu na pembe za ndovu kwa mda mrefu sana na hao waarabu wake.
Kwani wewe ulitaka wanyama ufanyie nao nini? Kama wateja wa kununua wanyama wapo kwa nini tukae nao !?
 
Paul Makonda mikono yako inanuka damu damu za binadamu wenzako una chuki na visasi. Ajabu unamtaja mara kwa mara Mungu aliyemtukufu. labda ni mungu wa Kolumije.

Mama yako mama bashite (samia) atalipa uovu huu wako
 
Back
Top Bottom