Paul Makonda akutana na Viongozi wa madhehebu na Taasisi za dini, asema anayoyafanya Rais Magufuli yanazidi maelekezo ya ilani ya CCM

Ushamba na ujanja ni maoni ya mtu binafsi cha muhimu ni tija ya mtu anapopewa nafasi ya uongozi.

Wajanja ndio hao waliokuwa wanakula bata kwa mishahara hewa.
Phillipo wewe ni wa zamani sio kama hawa wa Jana. Sema ukweli wako, siku za nyuma kulikuwa na tabia hizi za kujikomba komba kitoto namna hii? Hata wewe ukifika kwako jioni ukiona familia inaanza kukupa sifa tena unajua na wao wanajua kuwa za uongo utakaa kwenye sofa na kuchekelea badala ya kutembeza makofi kwa kukufanya "fala" kama waitavyo vijana wa mjini!
Tena nikushtue mzee mwenzangu, hapo ujue mama na watoto wana nia mbaya nawe. Shtuka!
 
Baba swalehe! kwanza swalehe hajambo?
Pili naona unakerwa,na usanii wa hawa vjiongozi wa dini, hats Sisi waumini tunakerwa na huu usanii
 
KAtika watu wenye wakati mgumu kwenye hii awamu ni viongozi wa dini. Wanalazimika kuongea uongo.Sijui kama Mungu atawasehe. Ila nimekuja kugundua kuwa viongozi wa dini wana dhambi nyingi sana kupita hata sisi waumini
 
Pengo amewabeza wale wote wanaomzodoa na kumsema JPM kwa madai ya kwamba haleti maendeleo ya watu bali ya vitu.

'Maendeleo ya kumfanya mtu asome na atibiwe si maendeleo ya watu!?'Alihoji Pengo.Ameenda mbele zaidi kwa kudhani pengine kwa akili zake za kizee ndiyo maana hawaelewi wakosoaji hao.

Pia,Mzee Pengo amempongeza Makonda na ametamka bayana kuwa Makonda ni baadhi ya wasaidizi wachache bora kabisa wa JPM!
 
Cardinal Pengo ni nembo ya ukatholic Tanzania

Km amemkubali Magufuli sisi ni nani hadi tukatae
 
Askofu asibishane na wajinga wa taifa ,ukawa na wanahakati njaa wengi wana sonona kali


State agent
 
Mzee amezeeka vibaya, pia yeye kama kiongozi wa dini anatupungizia imani yetu.
Matukio ya kutekwa na kuuwa kwa watu.
Tatizo la ajira kwa vijana.
Zoezi la uchaguzi wa serekali za mitaa, vyote vingetakiwa vikemewe na kanisa. Kama kanisa linatakiwa kusifia na kukosoa pia.
 
Kashiba kazeeka kachoka kachakaa ataongea nini zaidi ya unafiki? .

Wazee kama uyu wanatakiwa kdanja tu kuliko kutuongezea kinyaa.
 
Ni bora aache kuongea apumzike zake tu,maana hii ni aibu kwake na Kanisa
 


John Stuart Mill aliwahi kusema ukizoea kujipendekeza sana unaweza kumtukana mtu unayejipendekeza kwake ukidhani umemsifia.

Dar - Mbeya 813 Kms.
Dar - Mwanza km 1114 Kms.
Mwanza - Musoma 222 Kms.
Dar - Mtwara 560 Kms.
Iringa - Dodoma Km 240
Dodoma - Arusha Km 432

Na nyingine nyingi zilizojengwa kabla ya JPM. Kimsingi utawala uliojenga barabara nyingi zaidi tangu uhuru ni utawala wa Kikwete. Alianzisha miradi mingi ya barabara hata alipoondoka aliacha mingine ikimaliziwa ambayo JPM alichofanya ni kuizindua tu.

Mwaka 2005 nilitoka Arusha kwenda Dodoma kwa basi, ilikua safari ya kutwa nzima kuzungukia Chalinze. Leo ukitoka Arusha asubuhi, saa 4 unakunywa chai Dodoma kwa kupitia Kondoa. Wananchi wa Iringa nao kwenda Dodoma walilazimika kuzunguka Morogoro. Lakini kwa sasa ni mwendo wa masaa machache kupitia Mtera. Unaweza kutoka Iringa kwenda Dodoma kufanya shopping na ukageuka tena Iringa siku hiyohiyo.

Tuache kujipendekeza. Lets give credit where credit is due. JK pamoja na madhaifu yake mengine lakini ndiye aliyeunganisha mtandao wa barabara nchini kuliko Marais wote waliomtangulia na hata huyu aliyemfuatia.

JPM ana yake aliyofanya lakini si kwenye barabara. Kwenye ndege apewe credit (regardless zinajiendesha kwa hasara). Kwenye reli apewe credit (japo ni mradi wa hasara). Lakini kwenye barabara NO THANK U. Hakuna nominal impact.

JK alitaka kuwa na mtandao wa barabara wa kuunganisha mikoa yote jirani. Akaanza Dom to Iringa (via Mtera), Arusha to Dom (via Kondoa), Singida to Tabora (via Itigi) etc.

Lakini ndoto hii ya JK imezimwa. Barabara ya Singida - Tabora ambayo JK alishajenga zaidi ya 250Kms, JPM ameshindwa kumalizia 80Kms tu zilizobakia. Kipande kinachounganisha Morogoro - Tanga JK alikijenga, but JPM kashindwa kumalizia 70Kms tu za Turiani - Handeni. Kipande cha Sikonge - Chunya kimetelekezwa, Njombe - Moro (via Lupembe) kimetelekezwa, Ifakara - Songea kimetelekezwa.

Leo tunaambiwa JPM ndio anaongoza kwa kujenga mtandao wa barabara? Labda hizi za Goba na Kinyerezi, ambazo hata hivyo zilijengwa na JK yeye kafanya kumalizia tu.!

Na G Malisa
 
nafikiri labda ni kipindi akiwa waziri wa kikwete ..lakini kwa hili kikwete alikuwa yupo sawa ... nadhani alijenga km 35,000 hivi .kwa mujibu ya taakwimu za dotto bulendu .nilizo soma hivi punde.
 
hahaha mambo ya aibu sana km 800+ useme anaongoza benny pia alijenga km za kutosha

magu kaja kumalizia barabara za jk mf. tabora-katavi, katavi-kgm.

badala ya kumsifia anamfunua jiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…