John Stuart Mill aliwahi kusema ukizoea kujipendekeza sana unaweza kumtukana mtu unayejipendekeza kwake ukidhani umemsifia.
Dar - Mbeya 813 Kms.
Dar - Mwanza km 1114 Kms.
Mwanza - Musoma 222 Kms.
Dar - Mtwara 560 Kms.
Iringa - Dodoma Km 240
Dodoma - Arusha Km 432
Na nyingine nyingi zilizojengwa kabla ya JPM. Kimsingi utawala uliojenga barabara nyingi zaidi tangu uhuru ni utawala wa Kikwete. Alianzisha miradi mingi ya barabara hata alipoondoka aliacha mingine ikimaliziwa ambayo JPM alichofanya ni kuizindua tu.
Mwaka 2005 nilitoka Arusha kwenda Dodoma kwa basi, ilikua safari ya kutwa nzima kuzungukia Chalinze. Leo ukitoka Arusha asubuhi, saa 4 unakunywa chai Dodoma kwa kupitia Kondoa. Wananchi wa Iringa nao kwenda Dodoma walilazimika kuzunguka Morogoro. Lakini kwa sasa ni mwendo wa masaa machache kupitia Mtera. Unaweza kutoka Iringa kwenda Dodoma kufanya shopping na ukageuka tena Iringa siku hiyohiyo.
Tuache kujipendekeza. Lets give credit where credit is due. JK pamoja na madhaifu yake mengine lakini ndiye aliyeunganisha mtandao wa barabara nchini kuliko Marais wote waliomtangulia na hata huyu aliyemfuatia.
JPM ana yake aliyofanya lakini si kwenye barabara. Kwenye ndege apewe credit (regardless zinajiendesha kwa hasara). Kwenye reli apewe credit (japo ni mradi wa hasara). Lakini kwenye barabara NO THANK U. Hakuna nominal impact.
JK alitaka kuwa na mtandao wa barabara wa kuunganisha mikoa yote jirani. Akaanza Dom to Iringa (via Mtera), Arusha to Dom (via Kondoa), Singida to Tabora (via Itigi) etc.
Lakini ndoto hii ya JK imezimwa. Barabara ya Singida - Tabora ambayo JK alishajenga zaidi ya 250Kms, JPM ameshindwa kumalizia 80Kms tu zilizobakia. Kipande kinachounganisha Morogoro - Tanga JK alikijenga, but JPM kashindwa kumalizia 70Kms tu za Turiani - Handeni. Kipande cha Sikonge - Chunya kimetelekezwa, Njombe - Moro (via Lupembe) kimetelekezwa, Ifakara - Songea kimetelekezwa.
Leo tunaambiwa JPM ndio anaongoza kwa kujenga mtandao wa barabara? Labda hizi za Goba na Kinyerezi, ambazo hata hivyo zilijengwa na JK yeye kafanya kumalizia tu.!
Na G Malisa