Paul Makonda akutana na Viongozi wa madhehebu na Taasisi za dini, asema anayoyafanya Rais Magufuli yanazidi maelekezo ya ilani ya CCM

Paul Makonda akutana na Viongozi wa madhehebu na Taasisi za dini, asema anayoyafanya Rais Magufuli yanazidi maelekezo ya ilani ya CCM

Nadhani takwimu hizi alilenga Dar pekee lakini napo haziingii.
 
Katika kipindi cha miaka 10 ya Serikali ya Awamu ya Nne, barabara zenye urefu wa km 17,762 zilifanyiwa tafiti na jumla ya km 5,568 zilikamilika kujengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya jumla ya shilingi bilioni 4,090 na barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 3,873 ziliendelea kujengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya jumla ya Shilingi bilioni 4,533 ambayo malipo yafinyika kipindi cha awamu ya nne lakini mikataba ilimalizika kipindi cha awamu ya tano. Aidha, barabara zenye urefu wa km4,965 zilifanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa gharama ya Shilingi bilioni 29.257 na Serikali ilikuwa inaendelea kutafuta fedha za kuzijenga kwa kiwango cha lami. Vilevile,upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara zenye km 3,356 uliendelea kwa gharama ya Shilingi bilioni 34.263 na ujenzi wa nyumba 10,000 za watumishi wa umma ulifanyika ambapo nyumba 643 zimekamilika Tayari madaraja makubwa 12 yamekamilikana na vivuko 28 vinatoa huduma katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikilinganishwa na vivuko 13 mwaka 2005.

Jaribu kupitia JARIDA LA WIZARA YA UJENZI, Barabara Kichocheo cha Maendeleo ya Nchi tolea la 1Juni 2015
 
Makonda japo alipata zero darasani lkn,anajua kucheza na timing na ndiye opportunist mzr kuliko wote Bongo...Makonda anajua madhaifu ya Mkulu ni kutaka kusifiwa sasa Konda all the way from Kolomije anamsifia Mkulu hata akipumulia kisogoni ana mwambia "Mkulu hiyo gesi yako inanukia kama perfume"
 
Naona Kardinari Pengo anataka tuwaenzi Hitler na Mussolini.Anasema pamoja na hawa watu kuuwa kinyama mamilioni ya raia wema bado kuna mazuri walifanya.Ametoa mfano kuwa Mussolini alishiriki katika vita dhidi ya ugonjwa wa malaria.
 
Kishalu,
Napenda sana mtu anayejibu kwa hoja.haya tumuulize makonda izo km 800+ ni nyingi kuliko km 17k alizojenga kikwete?
 
Hivi Magufuli kwenye ujenzi wa jumla wa barabara atafikia hata nusu ya km zilizojengwa wakati wa Kikwete? Au Makonde ana nia ya kumsimanga Rais?
 
Makonda alipaswa kuongelea kuhusu mkoa wake na hadi sasa amefanya nini na anatarajia kufanya mambo yapi...haya mengine anapaswa kuongea waziri
 
Hii sio habari nzuri kwa lile genge la wajinga wa taifa ,wao kulialia tu

Asante makonda kwa msumali huu

State agent
Find a place to hide your foolishness. Hv Makonda zimo kweli kwamba JPM ameingia madarakan ameķuta km 400s za lam hvyo yey kajenga km 800s what a joke. Kukubali ujïnga huu kusifia unahitaji kuwa mwendawazimu
 
Je miaka hiyo yote 50 nchi hii ilikuwa inaongozwa na chama gani?
Mnategemea nini kutoka kwa kilaza Makonda a.k.a Bashite? Matunda ya kufoji vyeti ndo hayo. Anachanganya takwimu. Akashughulikie tu mambo ya tezi dume!
 
Mhadhama Pengo ameyasema hayo alipokuwa akiongea mbele ya viongozi wa dini, waliohudhuria mkutano wa mkuu wa mkoa.

Askofu huyo amesema alikuwa anawaza sana kuwa nani atakuwa Rais baada ya Magufuli lakini kwa namna alivyomsikiliza Makonda hana wasiwasi tena ya kumpata mrithi sahihi wa Rais Magufuli.
 
Huyu nyumbu anatafuta huruma baada ya juzi jiwe kufanya ile ya MUPE MURUKE, bila hiana alimkwepa kumpa mkono huyu mbwa mwitu,
Huyu jitu sjui kama lina akili za kibinadamu au za kinyani
View attachment 1266006

John Stuart Mill aliwahi kusema ukizoea kujipendekeza sana unaweza kumtukana mtu unayejipendekeza kwake ukidhani umemsifia.

Dar - Mbeya 813 Kms.
Dar - Mwanza km 1114 Kms.
Mwanza - Musoma 222 Kms.
Dar - Mtwara 560 Kms.
Iringa - Dodoma Km 240
Dodoma - Arusha Km 432

Na nyingine nyingi zilizojengwa kabla ya JPM. Kimsingi utawala uliojenga barabara nyingi zaidi tangu uhuru ni utawala wa Kikwete. Alianzisha miradi mingi ya barabara hata alipoondoka aliacha mingine ikimaliziwa ambayo JPM alichofanya ni kuizindua tu.

Mwaka 2005 nilitoka Arusha kwenda Dodoma kwa basi, ilikua safari ya kutwa nzima kuzungukia Chalinze. Leo ukitoka Arusha asubuhi, saa 4 unakunywa chai Dodoma kwa kupitia Kondoa. Wananchi wa Iringa nao kwenda Dodoma walilazimika kuzunguka Morogoro. Lakini kwa sasa ni mwendo wa masaa machache kupitia Mtera. Unaweza kutoka Iringa kwenda Dodoma kufanya shopping na ukageuka tena Iringa siku hiyohiyo.

Tuache kujipendekeza. Lets give credit where credit is due. JK pamoja na madhaifu yake mengine lakini ndiye aliyeunganisha mtandao wa barabara nchini kuliko Marais wote waliomtangulia na hata huyu aliyemfuatia.

JPM ana yake aliyofanya lakini si kwenye barabara. Kwenye ndege apewe credit (regardless zinajiendesha kwa hasara). Kwenye reli apewe credit (japo ni mradi wa hasara). Lakini kwenye barabara NO THANK U. Hakuna nominal impact.

JK alitaka kuwa na mtandao wa barabara wa kuunganisha mikoa yote jirani. Akaanza Dom to Iringa (via Mtera), Arusha to Dom (via Kondoa), Singida to Tabora (via Itigi) etc.

Lakini ndoto hii ya JK imezimwa. Barabara ya Singida - Tabora ambayo JK alishajenga zaidi ya 250Kms, JPM ameshindwa kumalizia 80Kms tu zilizobakia. Kipande kinachounganisha Morogoro - Tanga JK alikijenga, but JPM kashindwa kumalizia 70Kms tu za Turiani - Handeni. Kipande cha Sikonge - Chunya kimetelekezwa, Njombe - Moro (via Lupembe) kimetelekezwa, Ifakara - Songea kimetelekezwa.

Leo tunaambiwa JPM ndio anaongoza kwa kujenga mtandao wa barabara? Labda hizi za Goba na Kinyerezi, ambazo hata hivyo zilijengwa na JK yeye kafanya kumalizia tu.!

Na G Malisa
 
Ulimuuliza kama ni barabara kuu au za mijini maana kaavcha fumbo sasa muulize kisha utegue. Usijeingia na wewe kukosea.
 
Askofu mwizi wa pesa za escrow,atashindwaje kuipa sifa serikali mbovu.
Katika watu wanao mkufuru Mwenyezi Mungu huyo pengo ni wa kwanza.
 
Mr stone mda sio mrefu ataanguka, anguko lake litachangiwa kwa asilimia kubwa sana na hyu bwa mdogo.
 
Ohhhh....
Mungu njoo....
Fanya uje ujione ulio wateuwa wakifanya sjui manini tuu....
Yaani nimepata moto hadi natetemeka wallah..
Lakini, ebu ngoja nikae tu kimya nisije nikajiletea kesi na jamuhuri
 
Back
Top Bottom