Paul Makonda amefanikiwa kuiweka CCM katika mioyo na midomo ya Watanzania

Paul Makonda amefanikiwa kuiweka CCM katika mioyo na midomo ya Watanzania

Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika uteuzi uliofanywa na chama cha Mapinduzi chini ya uongozi shupavu, imara na madhubuti wa Rais na mwenyekiti wa CCM Taifa Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan , kumteua Mheshimiwa Paul Christian Makonda kuwa

IMG_6223.jpg
 
Ikiwa Serikali iliyopata uhalali Kwa wananchi imeshindwa kudhibiti mfumuko wa Bei na tatizo la Umeme.

Mwenezi asiyetambulika popote ataweza?
Mfumuko upi wa bei ambao serikali imeshindwa kudhibiti.
 
Amefanikiwa kushusha bei ya bidhaa inayopanda siku hadi siku?

Mtanzania utamshawishi endapo tu utafanikiwa kushusha gharama za maisha ambazo wananchi wengi hawamudu kwa kipato chao kiduchu.

Siasa anazofanya ni za kuwafurahisha wana ccm wenzake tu ambao hawajitambui ila mwananchi wa kawaida anayeelemewa na mzigo wa gharama za maisha hawezi kukaa kusikiliza porojo za Makonda.
 
Amefanikiwa kushusha bei ya bidhaa inayopanda siku hadi siku?

Mtanzania utamshawishi endapo tu utafanikiwa kushusha gharama za maisha ambazo wananchi wengi hawamudu kwa kipato chao kiduchu.

Siasa anazofanya ni za kuwafurahisha wana ccm wenzake tu ambao hawajitambui ila mwananchi wa kawaida anayeelemewa na mzigo wa gharama za maisha hawezi kukaa kusikiliza porojo za Makonda.
Kazi ya chama cha siasa na viongozi wake ni kuwasemea wananchi juu ya kero mbalimbali zinazowakabili.jambo ambalo linafanywa vizuri na chama chetu .ndio maana kinaendelea kupendwa na kuungwa mkono.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika uteuzi uliofanywa na chama cha Mapinduzi chini ya uongozi shupavu, imara na madhubuti wa Rais na mwenyekiti wa CCM Taifa Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan , kumteua Mheshimiwa Paul Christian Makonda kuwa katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa umekuwa ni uteuzi wa kihistoria na karata ya ushindi iliyochezwa na Rais Samia. imeonyesha uhodari wa Rais Samia kuusoma mchezo wa kisiasa na kujuwa nani aingie wakati gani kuipatia timu na chama ushindi na kuwapa matumaini watanzania kwa chama.

Kiukweli Mheshimiwa Paul Makonda amekirejesha na kukiamsha chama mitaani ,ameleta hamasa iliyokuwa imelala,imeinua matumaini ya watanzania kwa CCM,amefanya chama kuwa kimbilio la wanyonge,kwa kuwa Watanzania siku zote walikuwa wanahitaji kuona CCM yenye kuwajali,kuwasikiliza,kuwafuata waliko ili kujuwa maisha wanayoishi na changamoto zinazowakabili na wanazopitia na kuzipatia majibu stahiki.

Watanzania walihitaji sauti ya chama cha mapinduzi katika kuwasemea, kuwatetea,kuwa nyuma yao,kuwapigania dhidi ya dhuluma, unyonyaji, unyanyasaji,uporwaji wa haki,ukandamizwaji,uonevu pamoja na kuwafuta machozi,kuwapa matumaini,faraja na kuwashika mkono pale wanapokuwa wameishiwa nguvu.

Haya yote kwa sasa yanatekelezwa na CCM kwa mkono na kinywa cha Mheshimiwa Makonda ambaye amejitoa na kujitolea kukibeba chama mabegani mwake kukipeleka kwa wananchi ambao ndio wamekuwa dhamana kuu ya CCM kuwepo na kusalia madarakani kwa karibu nusu karne sasa. Mheshimiwa Makonda anazungumza lugha za watu,kero za watu,.anamsikiliza kila mtu kwa unyenyekevu.anakisemea chama na serikali kwa nguvu zake zote.ameiacha na kuwa mbali na familia yake ili kwenda kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao.

Ameiacha familia yake mke na watoto wake kwa ziara ndefu ili kwenda kuwafuta machozi Watanzania walioelemewa na mizigo ya kero na tabu katika mioyo na vifua vyao.ndio maana kwa sasa mitaani habari iliyoteka na kutawala katika vinywa vya watu ni kuhusu Mheshimiwa Makonda ,CCM na Rais Samia. hiyo ndio habari kuu iliyoteka hisia za watu wote. Ndio habari inayofuatiliwa kwa karibu hata na wapinzani wa nchi hii kama CHADEMA.ndio maana unaona walivyo karibu katika kufuatilia kila kinachoendelea katika ziara zake.

Sasa kupitia maelekezo ya Mheshimiwa Makonda akitoa maelekezo ya chama kwenda kwa wakuu wote wa mikoa na wilaya nimeshuhudia wakuu wa mikoa wakitekeleza agizo la wao kwenda kwa wananchi kuwasikiliza kero zao na kuwapa majibu.hivi hapa nilipo ilikuwa ni jana ambapo viongozi wote wa mkoa walikuwepo mtaani kwangu kuja kusikiliza kero za wananchi na kutoa majibu,jambo ambalo liliwapa matumaini makubwa sana wananchi, ambao walihudhuria na kutoa kero zao.

Unaweza kuona namna Mheshimiwa Makonda alivyoleta mapinduzi mapya ya kiutendaji kwa viongozi.kwa sasa wananchi wanaona kuwa ukinyimwa au kudhulumiwa haki yako basi ni CCM Pekee unapoweza kupata ufumbuzi na tumaini la shida yako.kwa kuwa ni CCM Pekee inayoweza kutoa msukumo na kuweka nguvu ya wewe kupata haki yako.ndio maana tunaona na kushuhudia mikutano ya Mheshimiwa Makonda ikifurika na kumiminika watu kusikiliza na wengine wakipigana vikumbo kwa jasho na machozi kutafuta kupata nafasi ya kuwasilisha kero zao kwa Mheshimiwa Makonda.

Hii ndio maana ya kuwa chama cha siasa kinachotawala na kuongoza serikali kuhakikisha kuwa kinakuwa karibu ya watu na kuwa kimbilio namba moja la watu, ndio maana sasa watu wanaona ni bora uende kwa Mh Makonda utapata haki yako haraka kuliko kwenda huko kwingine ukaishia kuzungushwa tu kama mpira.

Rai yangu ni kwa wakuu wa mikoa,wilaya,wakurugenzi na viongozi mbalimbali huko mikoani kuendeleza utamaduni huu ambao Mheshimiwa Makonda ameupandikiza na kuja nao kwa kuhakikisha kuwa mnatoka maofisini katika baadhi ya siku na kwenda kwa wananchi kuwasikiliza wananchi.kwa kuwa ninyi ndio mpo na wananchi kila siku na mkilipwa mishahara kwa kazi hiyo ya kuhudumia watu.hakikisheni mnakuwa karibu ya mwananchi,hakikisheni mkiletewa jambo mhakikishe kuwa linapatiwa ufumbuzi na mwenye haki anapatiwa haki yake.

Maana katika ziara za Mheshimiwa Makonda nimesikia wengine wakisema kuwa jambo hili nimefikisha hadi kwa mkuu wa wilaya,mkoa n.k.hii maana yake ni kuwa wengine huwa hamfuatilii kuhakikisha kuwa maelekezo yenu na maagizo yanafanyiwa kazi na watu wanapata haki zao.ndio maana inapotokea ziara za viongozi wakuu wananchi wanajitokeza na mabango wakilia na kububujikwa machozi kwa kuwa ninyi mnakuwa mlishindwa kuwapatia majibu na kuwasaidia kupata haki zao.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.View attachment 2892767
Wewe jamaa habari zako zote ni kuhusu DAB tu,
Ni anakulipa au ndo mambo ya multiple IDs??
 
Wewe jamaa habari zako zote ni kuhusu DAB tu,
Ni anakulipa au ndo mambo ya multiple IDs??
Basi na wewe andika habari zingine unazoona sijaandika.maana mimi naandika kuhusu maeneo mengi na masuala mengi tu .
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika uteuzi uliofanywa na chama cha Mapinduzi chini ya uongozi shupavu, imara na madhubuti wa Rais na mwenyekiti wa CCM Taifa Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan , kumteua Mheshimiwa Paul Christian Makonda kuwa
Hivi uchawa nao ni kazi kama kazi nyingine au uchawa ni kujitolea tu mkuu?
 
Mwenyekiti wa CCM Ni maarufu kuliko mwingine yeyote yule kutokana na kugusa maisha ya watu na kuleta Tabasamu na furaha katika mioyo yao.ndio maana aliamua kuleta mtu ndani ya chama atakayeendana na kasi yake na mahitaji yake ya kuwahudumia watanzania kwa unyenyekevu na utayari wa hali ya juu.ndio maana akatuletea Watanzania Mheshimiwa Makonda mwenye moyo wa unyenyekevu,upendo na ukarimu wa hali ya juu sana.ndio maana tunaona namna alivyo kimbilio la wanyonge kwote apitako huko katika ziara yake ya mikoa ishirini bila kupumzika.
Kila nisomapo bandiko lako huwa ninawahurumia sana majirani zako na wote unaoishi nao karibu.

Wewe jamaa ni mnafiki wa kutupwa..!
 
Kanuni ya kupendwa na wananchi ni kuwasikiliza na ikibidi kutatua kero zao.

Kama huwezi kufanya hivyo hakuna muujiza utakao fanya upendwe na wananchi.

Mhe. MAKONDA ameamua kuwasikiliza wananchi tumwache afanye kazi.
 
Back
Top Bottom