Paul Makonda amefanikiwa kuiweka CCM katika mioyo na midomo ya Watanzania

Paul Makonda amefanikiwa kuiweka CCM katika mioyo na midomo ya Watanzania

Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika uteuzi uliofanywa na chama cha Mapinduzi chini ya uongozi shupavu, imara na madhubuti wa Rais na .

Rai yangu ni kwa wakuu wa mikoa,wilaya,wakurugenzi na viongozi mbalimbali huko mikoani kuendeleza utamaduni huu
Makonda hakika Mungu ampe maisha marefu, yaani watanzania tunampenda sana tena sana. Dkt Samia angeweza kuwa kama Makondana kosa lake mwanzo ilikuwa kuanza kumdharau Dkt Magufuli (yaani alianza kushindana na mifupa ya marehemu), na matokeo yake Dkt Samia anachukiwa sana tena sana. Angalau ujio wa Makonda umebadili upepo, bila Makonda Dkt Samia alikuwa hashindi uchaguzi wa 2025, sababu kubwa ni chuki aliyopandikizwa na baadhi ya wasiomtakia mema.

Ila kwa sasa Dkt Samia anaaza kukubalika kupitia Makonda. Akitaka aupige mwingi atumbue viongozi wote kama Bashe wanaombeza Makonda, amuondoe Katibu Mkuu Nchimbi aliyemdharau Dkt Magufuli, ampige chini Naibu waziri mkuu aliyewahi dharau chuo ambacho rais Dkt Samia alisoma mwanzo.
 
Luca unazingua, uwe unatenganisha basi mambo ya kusema Watanzania unatujumuisha wengine katika upumbavu sio sawa.
Tusameheane tunapokoseana.sisi sote ni binadamu hatuwezi kufanana mitizamo.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika uteuzi uliofanywa na chama cha Mapinduzi chini ya uongozi shupavu, imara na madhubuti wa Rais na mwenyekiti wa CCM Taifa Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan , kumteua Mheshimiwa Paul Christian Makonda kuwa katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa umekuwa ni uteuzi wa kihistoria na karata ya ushindi iliyochezwa na
Kumbe lengo siyo kutatua kero za wananchi ? Lengo ni kukirudisha chama ccm midomoni????
 
Kumbe lengo siyo kutatua kero za wananchi ? Lengo ni kukirudisha chama ccm midomoni????
Unawezaje kukiweka midomoni na mioyoni kwa watu chama ikiwa hutatua kero zao wala kujibu maswali na kutoa utatuzi wala kukata kiu ya wananchi wala kuwapa matumaini wala kuwa na mipango yenye kugusa maisha ya watu?
 
Unasababisha matatizo. Halafu unayatatua au siyo luca? Wewe kweli mjinga wa taifa kama makonda ni solution sasa hawa mawazir wa kisekta tunaowapa ma v8 wann sasa
 
Nani kasema anaiumbua serikali? Kwa hiyo furaha yako unataka watu wafe na shida zao majumbani mwao? Unataka watu waendelee kuteseka na shida zao? Unataka waliopokwa haki zao na watu huko mitaani wasitafute msaada kwa chama? Ziara za Mheshimiwa Makonda zinasaidia sana wananchi na kuonyesha nini kifanyike huko mikoani.ndio maana kwa sasa viongozi kama ma RC na Ma DC wameanza kwenda kwa wananchi kuwasikiliza kero zao na kuwapatia majibu ya kero zao
Hizo shida zimeletwa na nani
 
Ndugu yangu suala la sukari kupanda bei lilishaelezwa na kutolewa ufafanuzi na serikali na tayari sukari imeshaingia nchini na muda siyo mrefu itaanza kusambazwa nchini na hivyo bei kupungua.

Suala la maisha ndugu yangu ni kuwa lipo katika juhudi za mikono yako. Umaskini katika familia zetu Watt zitaondolewa na sisi wenyewe watanzania kwa kufanya kazi kwa bidii, juhudi,maarifa na kujituma kwa hali ya juu.kazi ya serikali ni kuweka mazingira wezeshi kutusaidia Watanzania kujikwamua kiuchumi
Hapo kwenye mazingira wezeshi ndo tatizo kubwa lilipo
 
Watu wa kitengo wana mbinu nyingi ya kuwatoa watu katika "attention" ya mambo yaliyokuwa "talk of the town and equally embracing public cencures" Serikali iliyopo madarakani inakabiliwa na udhaifu mkubwa wa kiutawala ikiambatana misukosuko mingi katika kila nyanja za kiuchumi na kijamii.

Ili kujihami na hili wamemleta domokaya huyu kimkakati ili kuwaondoa watu kwenye "attention" ya kuweza kuhoji vitu vya msingi. DAB ni mtu wa mfumo ambaye ameletwa kwa kusudi maalum na mkakati huo maalum wa ku "dilute" mapungufu na fikra chovu za watawala na mfumo wenyewe.

MENE, MENE, TEKELI & PERESI
 
Acha porojo zako wewe.mheshimiwa Makonda anabebwa na uchapa kazi wake na unyenyekevu wake katika kusikiliza kero za watu na uwezo wake mkubwa wa kuweza kumsikiliza kila mtu.
 
Nchi nZima iko gizaniii ziiiii

Na giza hili vibaka,wezi wanafanya yao

Na,giza hili watu wana nyanduana tu

Ova
 
Nchi nZima iko gizaniii ziiiii

Na giza hili vibaka,wezi wanafanya yao

Na,giza hili watu wana nyanduana tu

Ova
Tuwe na subira maana TANESCO wameshatoa taarifa kuwa kuna hitilafu imejitokeza na wapo wanapambana ili umeme uwake haraka sana.pole sana kwa usumbufu wote uliojitokeza kwetu watanzania na hasara zote zilizopatikana kutokana na kukatika huko kwa umeme.
 
Unaandika makala za kujipendekeza lakini kwa vile zinakosa maudhui ndiyo maana huitwi,unatwanga maji kwenye kinu yataishia kukulowesha tu. Wanakudharau sana.
Mimi sijipendekezi kwa mtu bali naandika ukweli ambao pengine wewe huupendi kwa kuwa unakuumiza.
 
Acha porojo zako wewe.mheshimiwa Makonda anabebwa na uchapa kazi wake na unyenyekevu wake katika kusikiliza kero za watu na uwezo wake mkubwa wa kuweza kumsikiliza kila mtu.
Lucas ukiwa kama chawa halisi na mtoto wa kufikia wa mama, kuna "issues" huwezi kabisa kuzitendea haki. Basi baki kama ulivyo kwa asili ya hadhi na haiba yako.
 
Anafanya kazi iliyotukuka kwa niaba ya Rais wetu, na wananchi tunalijua hilo
Ikiwa Serikali iliyopata uhalali Kwa wananchi imeshindwa kudhibiti mfumuko wa Bei na tatizo la Umeme.

Mwenezi asiyetambulika popote ataweza?
 
Back
Top Bottom