Paul Makonda amefanikiwa kuiweka CCM katika mioyo na midomo ya Watanzania

Paul Makonda amefanikiwa kuiweka CCM katika mioyo na midomo ya Watanzania

Kanuni ya kupendwa na wananchi ni kuwasikiliza na ikibidi kutatua kero zao.

Kama huwezi kufanya hivyo hakuna muujiza utakao fanya upendwe na wananchi.

Mhe. MAKONDA ameamua kuwasikiliza wananchi tumwache afanye kazi.
Wananchi wanataka kusikilizwa changamoto zao kisha zibebe kama kiongozi sitafutie ufumbuzi! Ni ajabu watu wanasema Makonda hana mamlaka yoyote ilihali JPM alifanya akiwa na Mamlaka wakawa wanakasirika! Hapa ndipo Mabepari utawajua kwa rangi zao!

Nashangaa Rais Samia huwa hataki kusikiliza kero za wananchi wake alafu anategemea kurudi ane kumuomba kura ambae hataki kumsikiliza! Kukaa jukwaani kuhutubia wewe tu kisha kuondoka then kisha utoe press release kuwa umeongea na wanachi sio kweli, hutopendwa ata kidogo.
 
Ni wananchi wajinga pekee ukiwemo mtoa mada ndiyo mnampenda huyo Bashite wenu.
Tunapenda anachofanya kama kiongozi kusikiliza wananchi wake na kubeba changamoto zao kisha kuzishuhulikia. Ndiyo kiongozi tumtakae.
 
Ukitaka kujua kwanini serikali ya ccm inahakikisha wananchi wa Tanzania hawapati elimu iliyo bora angalia jinsi kulivyo na umati mkubwa unaomiminika kusifia mambo ya kijinga mitandaoni na offline.
 
Failure ya Mifumo iliyosababishwa na Uzembe na RUSHWA katika Serikali ya CCM na Bunge lake la Chama Kimoja anachofanya Makonda ni kulidhihirisha hilo.

Wekeni TUME HURU tuingie kwenye UCHAGUZI HALALI muone acheni MAIGIZO.
 
Alichofanikiwa Makonda na ziara zake ni kwa wananchi kupata mahala pa kutolea tension na stress za matatizo na kero zilizojilimbikiza muda mrefu. Kuhusu kurejesha CCM kwenye mionyo yao sina uhakika. kutokana na unafiki uliokthiri kwa sasa kwa watu wetu.
 
Back
Top Bottom