Paul Makonda amtaka Gwajima afike ofisini kwake kutolea ufafanuzi juu ya kumkashifu Pengo

Paul Makonda amtaka Gwajima afike ofisini kwake kutolea ufafanuzi juu ya kumkashifu Pengo

Paul Makonda huna adabu hata kidogo. nilidhani ungemshauri rais wako jk ampe ukuu wa wilaya askofu gwajima badala yake unamuita ofisini kwako? huna khaya!

wewe Paul Makonda ulimpiga hadharani mzee warioba, ukazawadiwa ukuu wa wilaya. vivyo hivyo, ulipaswa kumshauri rais amteue gwajimu kuwa RC au DC. umeona eeh?
 
Last edited by a moderator:
Huyu GAMBA anayepiga wazee wetu naye ana uadilifu gani wa kumwita na kumuhoji Gwajima??
Nchi inaongozwa na mazombi hii.
 
Kichaa kapata RUNGU.Polisi wameshaanza mambo ya kisheria na wewe Makonda unaingilia je? Achia polisi wafanye kazi zao.Pia muite nayule aliye mkwita Waziri mkuu mstafu Warioba,wote walivunja sheria.

Lawama zote naelekeza kwa prof tezi kwa kumkabidhi rungu kichaa.
 
Pole sana Gwajima yaani ukahojiwe na Makonda aiseee inasikitisha sana. Yote haya kisa umemgusa Askofu wa CCM..
 
Makonda huyu huyu aliye mpiga makofi mzee Warioba?? Si Makonda wala gwajima wote nidhamless
 
ni kama vilevile ambavyo
Warioba hakumjibu
marehemu kapteni Komba.
 
Mmmhhh!!!

Na yeye Makonda anapata wapi madaraka kikatiba kumuita mtu ambaye kafanya 'jinai'...?

Makonda anatafuta umaarufu tu hapa...
 
Huyu jamaa alivyomtusi Lowassa mbona hakuitwa polisi?!

gwajima usiende kwa makondakta, utaongea nini na konda tuone atafanya nini jinga tu,kama gwajima ana kesi ya kujibu si apelekwe mahakamani
 
Kama mlikuwa hamjui gwajima kamgusa mwenye nchi haya yaliyo mkuta gwajima ndio yaliyo mkuta ponda pengo ndio kiongozi katika nchi hii bora umtukane mkuu wa kaya kuliko pengo sisi ndio tunaujua mfumo kristo unavyo tawara nchi
ACHA UPUUZI
mimi ni mkatoliki kuliko wewe

PENGO AMEKOSEA, PENGO AMEDHARAU MAASKOFU,
GWAJIMA hajatukana ukatoliki tena ukimsikiliza umeliheshimu sana kanisa pale alipodai limemlea

kwa taratibu za kikatoliki zilivyo ni marufuku kupinga jambo lililoamuliwa pamoja na pengo alikuwa na nafasi ya kupinga hili jambo ndani ya vikao akasubiri kujidhalilisha

KWA KADRI GWAJIMA anavyohangaishwa ndivyo tunavyozidi kuamini PENGO ni askofu wa serikali na sii kanisa
 
ACHA UPUUZI
mimi ni mkatoliki kuliko wewe

PENGO AMEKOSEA, PENGO AMEDHARAU MAASKOFU,
GWAJIMA hajatukana ukatoliki tena ukimsikiliza umeliheshimu sana kanisa pale alipodai limemlea

kwa taratibu za kikatoliki zilivyo ni marufuku kupinga jambo lililoamuliwa pamoja na pengo alikuwa na nafasi ya kupinga hili jambo ndani ya vikao akasubiri kujidhalilisha

KWA KADRI GWAJIMA anavyohangaishwa ndivyo tunavyozidi kuamini PENGO ni askofu wa serikali na sii kanisa

.......Martina.....ni vema ungemwelewa Pengo.....Nilivyomuelewa mimi .....sio msaliti hata kidogo....tambua aliruhusi barua isomwe jimboni kwake kitu ambacho angeweza kukataa......pili walipohamua kikao kilifanyika Arusha yeye hakuwepo alikuwa ITALY na baadae INDIA.....na alisema kabisa anachotoa ni MAWAZO YAKE BINAFSI....kama yeye....alipokosea ni wapi sasa.......jamani tuweke dini zetu pembeni tuuvae Utanzania........hili taifa ni letu sote...sio la wakristu peke yao....tambua wapo wasioamini Mungu, waislam na wengine.....kila mtu akija na maazimio kutakuwa na nchi kweli..... ........SOMA ALICHOKISEMA LEO

UFUATAO ni ujumbe mfupi wa Muadhama
Polycarp Kardinali Pengo alioutoa leo katika
Kanisa la St. Joseph jijini Dar es Salaam
kuhusiana na waraka wa maaskofu uliotolewa
hivi karibuni kwa Wakristo nchini
kujiandikisha kikamilifu na kisha kuikataa
Katiba Inayopendekezwa wakati wa kura ya
maoni kwa vile haikujadiliwa kiuadilifu.
"Maaskofu hatuna mamlaka ya kuwaamulia/
kuwalazimisha waumini wetu wafanye
uamuzi gani kuhusu katiba, kuwaamulia ni
kuwadharau kuwa hawawezi kufanya uamuzi
sahihi wao wenyewe na kuingilia uhuru wao.
Waraka huu unaleta utengano katika taifa
kuwa Wakristo, tumechukua uamuzi dhidi ya
serikali na wengine....
Tuwaache waumini wafanye uamuzi kwa
tafakari yao binafsi bila shinikizo letu.....
Wakati hili linajadiliwa nilikuwa Italy katika
kusimikwa makardinali na baadaye India,
wengine wakavumisha nimelazwa,..wengine
nimefariki, lakini namshukuru Mungu hizo ni
dua za kuniongezea maisha marefu na afya
(makofi).
Nililetewa waraka nikausoma, umepitishwa
baada ya tafakari kubwa nauheshimu. Lakini
nadhani tuwaache waumini wafanye uamuzi
kwa uhuru baada ya kutafakari....
Si sahihi tukaenda katika katiba kama
Wakristo kwa shinikizo la kupinga katiba...
Wawe huru anayepinga kwa hiari yake
anayekubali kwa dhamiri yake....
Sidhani kama viongozi wa dini sasa tuna amri
ya kulazimisha uamuzi juu ya katiba....
Hivi kila dini ikianza kuchukua misimamo
kuhusu mambo ya kisiasa Tanzania
itabaki???
 
Anatafuta umaarufu mbona kabla hajaitwb na polisi alikaa kimya anataka kumpiga aliyepigwa.Askofu Pengo anatoka mkoa mmoja na waziri mkuu lazima aitete serikali.
 
Back
Top Bottom