minuz
JF-Expert Member
- May 8, 2014
- 624
- 216
.......Martina.....ni vema ungemwelewa Pengo.....Nilivyomuelewa mimi .....sio msaliti hata kidogo....tambua aliruhusi barua isomwe jimboni kwake kitu ambacho angeweza kukataa......pili walipohamua kikao kilifanyika Arusha yeye hakuwepo alikuwa ITALY na baadae INDIA.....na alisema kabisa anachotoa ni MAWAZO YAKE BINAFSI....kama yeye....alipokosea ni wapi sasa.......jamani tuweke dini zetu pembeni tuuvae Utanzania........hili taifa ni letu sote...sio la wakristu peke yao....tambua wapo wasioamini Mungu, waislam na wengine.....kila mtu akija na maazimio kutakuwa na nchi kweli..... ........SOMA ALICHOKISEMA LEO
UFUATAO ni ujumbe mfupi wa Muadhama
Polycarp Kardinali Pengo alioutoa leo katika
Kanisa la St. Joseph jijini Dar es Salaam
kuhusiana na waraka wa maaskofu uliotolewa
hivi karibuni kwa Wakristo nchini
kujiandikisha kikamilifu na kisha kuikataa
Katiba Inayopendekezwa wakati wa kura ya
maoni kwa vile haikujadiliwa kiuadilifu.
"Maaskofu hatuna mamlaka ya kuwaamulia/
kuwalazimisha waumini wetu wafanye
uamuzi gani kuhusu katiba, kuwaamulia ni
kuwadharau kuwa hawawezi kufanya uamuzi
sahihi wao wenyewe na kuingilia uhuru wao.
Waraka huu unaleta utengano katika taifa
kuwa Wakristo, tumechukua uamuzi dhidi ya
serikali na wengine....
Tuwaache waumini wafanye uamuzi kwa
tafakari yao binafsi bila shinikizo letu.....
Wakati hili linajadiliwa nilikuwa Italy katika
kusimikwa makardinali na baadaye India,
wengine wakavumisha nimelazwa,..wengine
nimefariki, lakini namshukuru Mungu hizo ni
dua za kuniongezea maisha marefu na afya
(makofi).
Nililetewa waraka nikausoma, umepitishwa
baada ya tafakari kubwa nauheshimu. Lakini
nadhani tuwaache waumini wafanye uamuzi
kwa uhuru baada ya kutafakari....
Si sahihi tukaenda katika katiba kama
Wakristo kwa shinikizo la kupinga katiba...
Wawe huru anayepinga kwa hiari yake
anayekubali kwa dhamiri yake....
Sidhani kama viongozi wa dini sasa tuna amri
ya kulazimisha uamuzi juu ya katiba....
Hivi kila dini ikianza kuchukua misimamo
kuhusu mambo ya kisiasa Tanzania
itabaki???
alichokosea pengo ni kilekile alichokosea kilaini,infwakti sio makosa ni makusudi,pengo kaulizwa waraka usomwe au usisomwe alishindwa nini kusema usisomwe?kama sio unafiki halafu baada ya kupewa za kichwa na gwajima ndio anaongea hayo matakataka,hamna kitu hapo kafeli kama kilaini.kilaini nae pesa za sadaka miaka 3 kanisa halijui kama kuna sadaka hata kununua spika na mic basi angalau waumini wakimwimbia bwana sound zitoke stereo hakuna,lahauraa salaree