Paul Makonda amtaka mwandishi kumuuliza mama yake baada ya kumhoji tuhuma za kumshambulia Lissu

Kuna Watanzania wengi sana wajinga hayo mambo ya due diligence, ku balance story etc, hawaelewi. Au haeataki kuelewa.

Ndiyo kwanza wanamsifia Makonda.

Hata hawaoni tatizo kiongozi wa chama kitaifa kujibu kihuni hivyo.
 

..Lissu amewataja Magufuli, Kipilimba, na Makonda.

..Katika hao watatu nadhani Makonda is the odd one.

..Wanaopaswa kuchunguza, kukamata, na kushtaki, no jeshi la Polisi na Dpp.

..Serikali itoe taarifa kwanini waliomshambulia Lissu hawajakamatwa mpaka leo hii.
 
Mwalimu aliulizwa kuwa kuna hisia kuwa yeye Mwalimu alihusika katika njama za kutaka kumpindua Moi. Nyerere alimtaka mwandishi atumie akili zake kwa sababu Nyerere hakuwa na ugomvi na Moi wala Kenya. Nyerere aliona kama mwandishi hakufanya bidii ya kumwelewa Nyerere anasimamia nini katika siasa kabla ya kumwuliza swali hilo.
 

..basi kulikuwa na FURSA kwa Makonda kutoa "maelekezo" na " suggestions" kwa Igp/Polisi kuhusu tukio la kushambuliwa Tundu Lissu ktk eneo la makazi ya viongozi wa serikali na bunge.
 


Unadhani Makonda is the odd one, kwanini?

Hilo jeshi la polisi limemuita mara ngapi huyo muhanga kutoa ushirikiano ili kukamilisha hizo tuhuma?

Wanatoaje taarifa juu ya washambuliaji kukamatwa bila kuthibitisha kwanza washambuliaji ni akina nani?
 
..basi kulikuwa na FURSA kwa Makonda kutoa "maelekezo" na " suggestions" kwa Igp/Polisi kuhusu tukio la kushambuliwa Tundu Lissu ktk eneo la makazi ya viongozi wa serikali na bunge.


Ni wazi Makonda ameamua kutokutumia hiyo FURSA.

Ameamua kutumia njia ambayo kwake anaamini ni sahihi, sioni kosa lake.
 

..kuna tukio lingine la Mwalimu Nyerere kumjibu vibaya mwandishi wa Kenya aliyemuuliza kuhusu kumuunga mkono mmoja wa watia nia wa Uraisi kupitia Ccm mwaka 1995.

..Mwalimu alimjibu vibaya muandishi wa habari, sasa tujiulize kama tuhuma za muandishi zilikuwa za kweli au uongo. Je, Mwalimu alikuwa na mgombea au hakuwa na mgombea?

..Hili suala uliangalie zaidi KISAIKOLOJIA na jinsi watu wanavyosema ukweli au uongo.
 
Unadhani Makonda is the odd one, kwanini?

Hilo jeshi la polisi limemuita mara ngapi huyo muhanga kutoa ushirikiano ili kukamilisha hizo tuhuma?

Wanatoaje taarifa juu ya washambuliaji kukamatwa bila kuthibitisha kwanza washambuliaji ni akina nani?
usiwe chizi, kama Lisu na dereva wake wangekufa ina maana kungekuwa hakuna kesi ndivyo jinai inavyoenndeshwa nchini kwenu
 

We nawe kichwa maji,Lisu alishasema Makonda alihusika yeye kupigwa risasi,sasa mwandishi alimtaka Makonda athibitishe au akanushe uhusika wake kupigwa risasi TL.mwandishi ana kosa gani hapo?Ukiangalia kwa kwa makini hilo jibu alilotoa Makonda linaonyesha kuna kitu alifanya!upo hapo?
 
Unadhani Makonda is the odd one, kwanini?

Hilo jeshi la polisi limemuita mara ngapi huyo muhanga kutoa ushirikiano ili kukamilisha hizo tuhuma?

Wanatoaje taarifa juu ya washambuliaji kukamatwa bila kuthibitisha kwanza washambuliaji ni akina nani?

..Makonda is the odd one kwasababu kwa tukio kama lile chain of command inakuwa nimekwenda nje kidogo.

..Mwanzoni Polisi walikuwa wanadai wameshindwa kuchunguza kwasababu Lissu amekimbia nchini.

..Madai hayo yamethibitika kuwa ni uongo. Lissu amekuwepo nchini. Na amefika mara kadhaa ktk vituo vya Polisi. Juzi tu Lissu aliitwa Polisi kuandika maelezo kuhusu mkutano alioufanya maeneo ya Loliondo.
 
Kuna baadhi ya majibu huwezi kushangaa mtu kujibiwa maana ameuliza swali la kipuuzi
wewe kwa akili zako unaona ni swali la kipuuzi? hoja hapa makonda na hasa wanasiasa wakishindwa au ukiwabana sawasawa wanaruka kama alivyoruka makonda.
mfano mwengine Pasco alimuuliza Magufuri swali badala ya kujibu Magufuri akasema mbele ya waandishi kuwa "mayala kwa kiruga chao ni njaa"
cc pasco
 


Bado sijaridhika na hiyo sababu yako ya kumfanya Makonda “the odd one” vinginevyo tuseme ni easy target to accuse?

Sio mwanzoni tu, hata kipindi cha uchaguzi 2020 wakati wa kampeni ameitwa mara ngapi na hakwenda badala yake akamjibu IGP wa wakati huo kupitia mikutano yake ya kisiasa majukwaani?

Kuwepo kwa Lissu nchini ni sahihi lakini katika uwepo wake aliitikia wito wa dhahama yake mara ngapi?

Ulitaka alipoenda kuandika maelezo Loliondo wamlazimishe kuitikia wito wa tuhuma zake juu ya dhahama dhidi yake?
 

..Lissu angestahili lawama kama jeshi la Polisi lingemuita kutoa maelezo kuhusu tukio lake halafu akakataa.

..Kinachotokea sasa ni aibu kwa jeshi la Polisi. Kwamba wameweza kumhoji Lissu kuhusu mkutano wa Loliondo lakini wameshindwa kumhoji kuhusu shambulizi alilofanyiwa.

..Na kuna kipindi tulishuhudia Lissu akifika kituo kikuu cha Polisi Dodoma. Na alifika hapo baada ya mawasiliano na miadi na makamanda wa Polisi wa Dodoma.

..Binafsi sijashawishika na maelezo na mwenendo wa jeshi la Polisi kuhusiana na jaribio la kumuua Lissu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…