Paul Makonda amtaka mwandishi kumuuliza mama yake baada ya kumhoji tuhuma za kumshambulia Lissu

Paul Makonda amtaka mwandishi kumuuliza mama yake baada ya kumhoji tuhuma za kumshambulia Lissu

Kwa hiyo kwa akili yako angesema ajahusika ndio majibu yamepatikana kuwa hajahusika? Kwanini Muandishi asimuamini Lissu aliyesema ameambiwa na watu wake kuwa Makonda alihusika?
Muandishi mwenye akili alitakiwa kumuamini Lissu au yeye binafsi afanye uchunguzi!

Sasa anatakiwa akamuulize mama yake kama Makonda alihusika kumshambulia Lissu au lah…halafu aje atupe jibu kamwambiaje?

Kwanini asiende jeshi la polisi kuwahoji badala ya kupoteza muda tuuu…..
Mwandishi hawezi kuandika habari yenye tuhuma nzito hivyo bila kuuliza upande unaotuhumiwa. Ndio weledi wa uandishi. Waandishi wanalipa gharama ya profesionalism. Na hata kuandika majibu aliyopewa na Makonda ni weledi pia. Jamii ya watu wenye akili watajua kama Lissu alisema ukweli au alidanganya.
 
Hawa Waandishi wengine Huwa wanajitafutia matatizo wenyewe.Ukiwa unasomea udreva unaambiwa Ukiona kuwa unaweza kuzuia ajari jitahidi uizuie hata kama wewe utakuwa upande sahihi.
Unamaanisha nini hapa?

Hii inahusiana vipi na swali la mwandishi na jibu la Makonda kwa mwandishi huyo?

Kwanini swali rahisi analitolea jibu gumu linaloleta maswala mengi mengi zaidi?

Huyo ndugu yenu aliona shida gani kujibu tu hapana sihusiki au sijui lolote?

Ukiniuliza mimi nina maoni gani juu ya jibu hili la Makonda, jibu langu ni rahisi tu, kuwa;

Huko ni kuweweseka. Ni ukiri wa kificho pasipo hata yeye kutambua kuwa anakiri kuhusika kwake..!

Huyo ndugu yenu hana akili kabisa. Ananuka damu za watu. Hukumu yake ipo inakuja kwa kasi sana...!!
 
Ndio jibu alilopaswa kupewa huyo muandishi! Kwa hiyo kama ni kweli huyo Muandishi alitegemea apate jibu la ndio kutoka kwa makonda!

Mimi naongezea na akamuhoji na baba yake…..
Jambazi mwingine huyu hapa
 
Back
Top Bottom