Mara kadhaa Lissu amekiri kuwa serikali ndiyo inawajua waliomshambulia pale alipotakiwa kutoa ushirikiano kwa dola kuwabaini ili wachukuliwe hatua.
Awali alipoishutumu serikali (kwa kutokuchukua hatua) akijenga hoja yake hiyo, alisema anawajuwa waliomshambulia.
Leo baada ya uteuzi wa PCM anasema PCM anahusika na shambulizi lake.
Sote tunajuwa wazi kuwa madaraka ya PCM aliyonayo leo siyo ya ki-dola ya kuweza kumtisha mtu kiasi kwamba aogopwe.
Pia wakati PCM alikuwa benchi mbona Lissu hakumtaja? Mbona wengine walijitokeza kupambana naye Mahakamani bila woga?
Lissu alishindwa nini kutumia fursa hiyo kumtaja PCM kuhusika na shambulizi lake?
Huenda kesho akishindwana na Mbowe ndani ya CHADEMA atasema Mbowe anahusika na shambulizi lake.
Ndugai amepoteza nguvu ya kisiasa baada ya kuachia Uspika, Lissu hamtaji kuhusika na shambulizi lake.
Kesho Ndugai akipata uteuzi wa kumfanya kuvuma kisiasa utamsikia Lissu akimtaja kuhusika na shambulizi lake.
Nadhani Lissu kumtaja PCM kuhusika na shambulizi lake ni mbinu ya kuuzima moto wa PCM unaowaka nchi nzima na kubadili mwelekeo wa siasa nchini.
Hivi ni nani hasa alimshambulia Lissu?
Lakini pia ni nani hasa anajuwa kwa uhakika aliyemshambulia Lissu?
Jamani siasa!!? Tuchuje sana tunayoyasikia. Unaweza ukapandikizwa dhambi ya kumchukia mtu asiyehusika.
Sent from my SM-A260F using
JamiiForums mobile app