Paul Makonda amtaka mwandishi kumuuliza mama yake baada ya kumhoji tuhuma za kumshambulia Lissu

Paul Makonda amtaka mwandishi kumuuliza mama yake baada ya kumhoji tuhuma za kumshambulia Lissu

Makonda amehojiwa na mwandishi wa habari kwamba Lissu amesema ulihusika na shambulia lake Dodoma

Jibu amepewa kamhoji MAMA YAKO

Bashite ameshindwa hata kukana kwamba hakufanya lile tukio, ni wazi jibu la kwanza ilikuwa ni kukataa kuhusika

Damu ya mtu ni nzito bana.

Team Mwendakuzimu Jiwe wanaanza Kuanikwa Mchana kweupeee
 
Waandishi mliambiwa anayetaka kujua endapo alimpiga Lisu risasi 16 ama la, aende akamuulize mamake.


Chonde chonde mm naleta ombi kwenu waandishi, kwa yeyote aliyeyapata majibu ya swali hili atuwekeemajibu yake hapa.tafadhali.

Tunao
 
Hawa Waandishi wengine Huwa wanajitafutia matatizo wenyewe.Ukiwa unasomea udreva unaambiwa Ukiona kuwa unaweza kuzuia ajari jitahidi uizuie hata kama wewe utakuwa upande sahihi.
je ni kweli kwamba lisu alishambuliwa?
je ni kweli kwamba waliomshambulia mpaka leo hawajulikani?
je ni kweli kwamba makonda alikuwa mkuu wa mkoa mwenye nguvu wakati huo?
je ni kweli kwamba hapana uchunguzi wowote umefanyika mpaka leo?
je ni ni kweli kwamba amri ya raisi dictator magufuli ilikuwa chachu kwenye kushambuliwa kwa lisu?
ni hayo tu kwa sasa
 
Watanzania tunauwawa kama kuku. Akitokea wa kuhoji, jibu ni kama: muulize mama yako, wewe ni chadema, wewe ni ccm, umetumwa na Nape? TUTAKUFA HADI LINI? Waongoza mauaji wanazawadiwa vyeo!

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
 
Hivi unaelewa unachoandika lakini? Aliyezungumzia Mahakama za Kimataifa ni mimi?

..aliyezungumzia mahakama ya kimataifa ni wewe kwasababu nime-quote post yako.

..labda una tatizo la kumbukumbu, au una ID nyingi hapa jukwaani, na hiyo inasababisha ushindwe kukumbuka unacho-post.🤣
 
Lisu bi mwongo sana akisema akirudi tu tanzania atakuja kuwataja wote waliohusika mpaka sasaa hakuna kitu na gari yake ameshaichukua Hawajui huyo
 
Watanzania tunauwawa kama kuku. Akitokea wa kuhoji, jibu ni kama: muulize mama yako, wewe ni chadema, wewe ni ccm, umetumwa na Nape? TUTAKUFA HADI LINI? Waongoza mauaji wanazawadiwa vyeo!

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
Kikwete na mwinyi waliua watu maelfu kwa kipindupindu na madawa ya kulevya ..ila msio na akili amwezi kujua kuwa jpm alikuwa mwokozi...sasa maisha ya lissu ni muhimu kuliko maelfu walio teketezwa na madawa ya kulevya na kipindupindu
 
Ndio jibu alilopaswa kupewa huyo muandishi! Kwa hiyo kama ni kweli huyo Muandishi alitegemea apate jibu la ndio kutoka kwa makonda!

Mimi naongezea na akamuhoji na baba yake…..
Mara kadhaa Lissu amekiri kuwa serikali ndiyo inawajua waliomshambulia pale alipotakiwa kutoa ushirikiano kwa dola kuwabaini ili wachukuliwe hatua.

Awali alipoishutumu serikali (kwa kutokuchukua hatua) akijenga hoja yake hiyo, alisema anawajuwa waliomshambulia.

Leo baada ya uteuzi wa PCM anasema PCM anahusika na shambulizi lake.

Sote tunajuwa wazi kuwa madaraka ya PCM aliyonayo leo siyo ya ki-dola ya kuweza kumtisha mtu kiasi kwamba aogopwe.

Pia wakati PCM alikuwa benchi mbona Lissu hakumtaja? Mbona wengine walijitokeza kupambana naye Mahakamani bila woga?

Lissu alishindwa nini kutumia fursa hiyo kumtaja PCM kuhusika na shambulizi lake?

Huenda kesho akishindwana na Mbowe ndani ya CHADEMA atasema Mbowe anahusika na shambulizi lake.

Ndugai amepoteza nguvu ya kisiasa baada ya kuachia Uspika, Lissu hamtaji kuhusika na shambulizi lake.

Kesho Ndugai akipata uteuzi wa kumfanya kuvuma kisiasa utamsikia Lissu akimtaja kuhusika na shambulizi lake.

Nadhani Lissu kumtaja PCM kuhusika na shambulizi lake ni mbinu ya kuuzima moto wa PCM unaowaka nchi nzima na kubadili mwelekeo wa siasa nchini.

Hivi ni nani hasa alimshambulia Lissu?

Lakini pia ni nani hasa anajuwa kwa uhakika aliyemshambulia Lissu?

Jamani siasa!!? Tuchuje sana tunayoyasikia. Unaweza ukapandikizwa dhambi ya kumchukia mtu asiyehusika.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Huyo muandishi kuuliza ilo swali ni mpango wa msoga gang ... Nape ndiye aliye mtuma kuuliza ilo swali ....makonda anatakiwa kujua kua ana maadui wengi sana nyuma ya pazia wanao toka msoga gang .....huyu mzee kikwete na mwinyi wasipokufa mapema nchi itapitia magumu mengi sana


Hapana.

Unapotosha, makusudi ama bahati mbaya sijui.

Ila unapotosha.
 
Kuna wasukuma wenzake humu wanaona alijibu vizuri kabisa yaani kiongozi mwenye akili nzuri atatoa jibu Kama hilo kwa hadhira/uma??
 
Labda kuna ukweli fulani hapo kwani leo hii mama akiamua tu, kesho waliohusika tutawajua mradi hakati tawi alilokalia.


“Askari wa serikali ya CCM akipiga risasi 3 akakosea, atawajibika.” - Samia Suluhu Hassan (akiwa mgombea mwenza kampeni uchaguzi mkuu) 5 September 2020
 
Back
Top Bottom