Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kuna Watanzania wengi sana wajinga hayo mambo ya due diligence, ku balance story etc, hawaelewi. Au haeataki kuelewa.Yaani kuna watu wana akili za hovyo sana kudhani jibu la makonda ni sahihi.
Kwenye ulimwengu wa uandishi wa habari. Kuna kitu kinaitwa kubalance story.
Na hii story ya makonda huyo mwandishi akiamua kumkaanga makonda anaweza kuweka bonge la headline.
Mwandishi ataweka tuhuma dhidi ya makonda kama ilivyosema na Lissu.
Kisha atasema alipoulizwa Paul Makonda juu ya tuhuma hizo. Hakukanusha wala kuonesha kusikikitishwa zaidi alijibu "kamuulize mama Yako".
HIvyo mwandishi anaweza kusema mengi mabaya dhidi ya Makonda kwa sababu makonda alipewa nafasi kujibu hoja badala hata kuikana kwanza kisha kutoa maelezo mengi. Amekaa kimya na kutoa kejeli.
Ingekuwa mahakamani naamini unajua hakimu angefanya nini. Umesomewa shitaka badala ya kulikana kwanza, umeishia kutoa kejeli
Ndiyo kwanza wanamsifia Makonda.
Hata hawaoni tatizo kiongozi wa chama kitaifa kujibu kihuni hivyo.