GE2025 Paul Makonda anazunguka Nchi Nzima na Kuweka Mikutano kama nani?

GE2025 Paul Makonda anazunguka Nchi Nzima na Kuweka Mikutano kama nani?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Nimeona Clip ya Makonda aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na sasa mgombea ubunge Arusha akipita Kanda ya ziwa na maeneo mengine nchini na magari yake akihotubia umma na kusema watu wasikubali alichofanyiwa magufuli afanyiwe Samia.

Mimi swali langu ni Makonda alitakiwa afanye kampeni zake Arusha, kwa sababu ndiko anakogombea. Hiyo ya kuzunguka nchi nzima anasimamisha watu anafanya kama kiongozi yupi. Au vibali vya kampeni vinasemaje.

View: https://www.instagram.com/reel/DPq1jH1jJkX/?igsh=dzM5YWpxcnc0MnU4
 
Watz mmeshaingizwa cha kike
 
kama mwanachama wa CCM tafadhali Sema Makonda kaidiwa cheo kikubwa waziri lazima
 
Aishie huko huko kanda ya ziwa kwa mangosha wenzake
 
Matokeo ya kukosa upinzani sahihi, badala ya kuomba kura jimboni kwake yupo kanda ya ziwa kuwaomba wasukuma wenzake kura za Urais kwa Samia.

Hata Nape alimpigia Samia kamoeni kanda ya kaskazini

Majimboni kwao hakuna ushindani wanasubiria kuapishwa
 
Mtoa mada umewaza vizuri sana. Lakini ni wazi kuwa kampeni zilishaporwa na walafi wa madaraka. Na uchaguzi walishamaliza kitambo. Matokeo wanayo tayari mifukoni mwao. Nilimuiza M/kiti wa Mtaa mmoja kwanini mgombea wenu hana habari na jimbo lake? Alicho jibu ni kwamba uchaguzi ulishamalizika ile siku anateuliwa kuwa mgombea. Hivi sasa ni maigizo tu. Ingawa hata sisi hatupendi lkn hatuna la kufanya wenye nguvu wameshikilia mpini. Na posho zetu tulishachukuwa kitambo. Wewe unafikiri hiyo asante tulipewa ya nini kama kazi ingekuwa haijamalizika??

Uliwahi kuona wapi mgombea ubunge analiacha jimbo lake bila hata kwenda kuwatemelea/kujitambulisha kwenye Kata mbalimbali kwa wapiga kura wake?? Yuko busy kwenye majimbo ya wenzake utafikiri huko hakuna wagombea. Upuuzi mtupu. (Haya maneno siyo yangu bali ni ya M/kiti wa Mtaa).

Huyu zero brain ukimuuliza jimbo lake lina Kata na Mitaa mingapi wala hana jibu. Licha ya kero za wananchi. Arusha CCM imewadharau sana tena sana.
 
Wewe ni mwana CCM? Kama ndiyo huijui itikadi ya chama na kama siyo kausha hayakuhusu. Makonda ni mwenezi mstaafu na anakipigania chama chake.Siyo ajabu ukamwona Nape akiwa Musoma akipiga kampeni au Ridhiwani Kikwete akiwa Kigoma akipiga kampeno, hakuna cha ajabu hapo Sheikh
 
Back
Top Bottom