Paul Makonda ateuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi

Paul Makonda ateuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi

View attachment 2789085

Ndugu Paul Makonda ameteuliwa na CCM kuwa Katibu Mwenezi.

===

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 22 Oktoba, 2023 mjini Dodoma, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Ndg. Dokta Samia Suluhu Hassan, pamoja na masala mengine, imeridhia kwa kauli moja na kuielekeza Serikali kuendelea na hatua ya utiaji saini mikataba ya uendelezaji na uwekezaji wa bandari.

Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kwa kumteua Ndugu Paul Makonda kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, akichukua nafasi ya Ndugu Sophia Edward Mjema ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masala ya Wanawake, Watoto na Makundi Maalum.

Halmashauri Kuu ya CM Taifa pia imemteua Ndugu Rabia Abdallah Hamid kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), akichukua nafasi ya Ndugu Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki.

Aidha katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imezipongeza Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya Rais Dokta Hussen Ali Mwinyi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025.

===

Pia soma: Paul Makonda kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM!
Vijana wa kimkakati kama kina Nnape na Makamba hawana furaha hapa
 
Very disappointed with the appointment,I choose to reserve my comments,BUT LET THEM CCM GO AND LISTEN TO THE SONG OF THE LATE LUCKY DUBE,..,''YOU GONNA REAP,JUST WHAT YOU SOW''...
Pole ....!!! Mimi siku hizi stress sitaki Hata kidogo. Enjoy Mkuu, halafu siyo Kila jambo unaloona sawa sote tunaliona sawa!!
 
Hawa ndio CCM sasa.
CCM Ni genge la wanyang'anyi lenye maslahi yanayofanana. Huu Ni mduara wa kula keki ya Taifa.

Haya Ni maandalizi ya Uporaji wa Uchaguzi Mkuu 2025.

Hakuna CCM msafi na hakuna wa kumnyooshea mwingine kidole.

Nb: Mimi siwalalamikii CCM kwa sababu nami najitahidi nikipata connection najiunga ktk ulaji.

Nafasi cjapata tu!
 
Siasa balaa hata Former PM Nawaz Sharif kapokelewa kwa vifijo na furaha wakati alikuwa mwizi mkubwa na kukimbia nchi
Ila maisha ndio yalivyo huwezi kujua ila kuna utabiri
 
Siku dp world wanasaini mkataba, a controversial appointment is made...
Samia kweli kaiva sasa anaupiga mwingi, amejua kucheza na akili za watanzania...
Pembeni alikuwapo Jk kikwete the engineer...!
Binafsi iam happy for makonda, ila najua ameteuliwa kwa ajili ya kutumika kuzima mjadala wa dp world...
 
Makonda kafanya maisha ya wengi yawe magumu mnamrudisha wa nini ?

alipoondoka alihojiwa ofisini alisema anachojutia hajafanikiwa kuwapima wanaume wa Dar tezi dume (kwa njia ya dole)

Hapa stop ya kwanza anaenda kuendeleza visasi vyake.
Mmeingia mkenge kumjadili makonda badala ya mkataba mlioupinga... kweli manyumbu ni manyumbu... na mkiendelea kupiga kelele atateuliwa sabaya kwenye nyadhifa yoyote ili muachane kabisa na ishu ya mkataba wa dp world mjadili hawa watu...
 
Maza alimkingia kifua asishughulikiwe...
Jamaa alipata malalamiko sana kutoka kwa Wahindi.. Walienda pale PCCB Upanga..
Wahindi walichotwa sana na Bashite...

Ila safari hii sidhani kama ataleta ubabe tena wa kiMagufuli
Wivu Kama mwanamke!
 
Makonda alifanya mambo mengi mazuri. Huu ndiyo ukweli. Wakazi wa Dar es Salaam ni mashahidi. Ni mchapakazi mzuri sana, ni muongeaji (orator) mzuri sana na mhahasishaji (community mobilizer) mzuri kwa rika zote.

Kati ya mambo mazuri aliyoyafanya ni pamoja na hili hapa chini.


View: https://youtu.be/QUomwpKMfx8?si=kouuz2tUWTzq6e5u
 
Makonda alifanya mambo mengi mazuri. Huu ndiyo ukweli. Wakazi wa Dar es Salaam ni mashahidi. Ni mchapakazi mzuri sana, ni muongeaji (orator) mzuri sana na mhahasishaji (community mobilizer) mzuri kwa rika zote.

Kati ya mambo mazuri aliyoyafanya ni pamoja na hili hapa chini.


View: https://youtu.be/QUomwpKMfx8?si=kouuz2tUWTzq6e5u

Shetani alimsikia sana Makonda akauawa Mwendazake na mama sasa anatanua. Mbona sasa wanamsema vibaya au nalo hili anasemaje?
 
Ni muda sasa wa wasanii kuonyesha unafiki wao. Wataanza kumpost na wengine kumwita Dady. Mwendazake Lemutuz angekuwa hai sijui ingekuwaje.. angeendelea kumuita Le Commandant? Natumaini safari hii Makonda hatafanya upuuzi tena aliofanya akiwa RC. Huyu jamaa alikuwa mtu safi sana wakati akiwa DC Kinondoni ila ukuu wa mkoa ulimpumbaza. Kwa hali ya hewa ya kisiasa CCM imefanya uamuzi sahihi kwasababu hadi hapo tayari genge la Sukuma limekufa rasmi. 2025 Mama ana uhakika wa kura toka kwenye kila kundi la watanzania wakiwemo BAWACHA, Sukuma gang, Bodaboda na wafuasi wengi wa Mbowe.
Kuna yule shehe wa dar aliemkana makonda Mara 3 kule kigamboni[emoji28]
 
Mtapoteana sana huku kwenye Sacco's yenu ya CHADEMA maana mpaka sasa mmechanganyikiwa kabisa

..Makonda is not intelligent.

..Hiyo nafasi inahitaji mjenga hoja nzuri kitu ambacho Makonda hana uwezo nacho.

..Makonda alikuwa akivuma na kutamba kwasababu ya mamlaka ya kukamata na kufunga kitu ambacho sasa hivi hana.
 
alipoondoka alihojiwa ofisini alisema anachojutia hajafanikiwa kuwapima wanaume wa Dar tezi dume (kwa njia ya dole)

Hebu nisaidie chanzo, gazeti ama clip, inayomwonyesha Makonda akisema anachojutia kutofanikisha kama RC Dar ni kuwapima wanaume tezi dume kwa njia ya kidole.
 
Kuna yule shehe wa dar aliemkana makonda Mara 3 kule kigamboni[emoji28]
😄😄😄 ni muda muafaka wa kuwatambua wanafiki. Marehemu hasemwi ila Lemutuz alikiwa mnafiki wa karne. Yaani alimkana fasta sana Makonda.
 
CCM Ni genge la wanyang'anyi lenye maslahi yanayofanana. Huu Ni mduara wa kula keki ya Taifa.

Haya Ni maandalizi ya Uporaji wa Uchaguzi Mkuu 2025.

Hakuna CCM msafi na hakuna wa kumnyooshea mwingine kidole.

Nb: Mimi siwalalamikii CCM kwa sababu nami najitahidi nikipata connection najiunga ktk ulaji.

Nafasi cjapata tu!
Hahahaha..namwona pale uwanjani kama Sabaya, Yuko anapasha mwili viungo, naye aweze kuingia........kaazi kwelikweli.
 
Back
Top Bottom