Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ikifika Aprili 15, 2024 atawataja kwa majina Watu wakiwemo Mawaziri wanaotoa fedha za kuwalipa Watu ili wamtukane Rais Samia mitandaoni kama hawataacha.

Akizungumza wakati wa Kumbukumbu ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, amesema "Kaka zangu mnaotuma na kulipa watu kumchokoza Mama yangu Samia mnanijua na mimi nawajua, wengine ni Mawaziri leo tarehe 12 iwe mwisho"

Aidha Makonda amemwomba Rais Samia kutoa Fedha za ujenzi wa Kilomita 20 za Lami Jijini humo na kueleza kuwa Wananchi wamemtuma amuombe Mama yake na wanampima kama ni Mama yake kweli

=========

Akitoa salaam za mkoa kwenye kongamano la kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine leo hii 11 April 2024, amesema kuna watu, wakiwemo mawaziri wanawatuma watu kumtukana Rais Samia mitandaoni.

Makonda kasema anawajua na wao wanamjua. Amewataka waache kufanya hivyo leo hii. Ameonya wasipoacha atawataja majina yao siku ya Jumatatu tarehe 14 April 2024.

Unaweza kubashiri ni mawaziri gani wanafanya hujuma hizi dhidi ya bosi wao? Au Makonda anatafuta kiki?

Maana hata jiwe alimdanganya kama hivi, ndiyo maana jiwe akawa karibu sana na Makonda. Jiwe alipokuja kugundua kuwa aliingizwa chaka akamtema.

View attachment 2961639

Source:. Kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine

Pia, soma=> Rais Samia akiashiriki Misa Maalumu ya miaka 40 ya kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine
Sijui Samia amempendea nini Makonda.
 
Vetting system ni muhimu sana kwa Viongozi Wakuu.
Ni muhimu watumishi Serikalini wasiwe wanasiasa.
Kwa mfano Mh.Rais Dr.Samia angelimtaka Mh.Makonda kusema pale pale hao wanaohusika,nadhani ingeleta picha tofauti kabisa na kuaribu dhima nzima ya Kumbukizi ya Hayati Waziri Mkuu Edward M Sokoine.
Presha presha za namna hii ndizo zinafanya baadhi ya Wasomi either kuogopa kusema ukweli au kutojihusisha kwa namna yeyote kusaidia Nchi katika ushauri/maamuzi hasa katika nyakati ngumu za uajibikaji.
 
Naamini hujafanya utafiti wa kutosha kwamba waponama la. Kwa hiyo huna haki ya kuhitimisha kuwa hawapo mawaziri wa namna hiyo.
Yeye kasema ni mawaziri wanaume na wanajuana (anawajua na wanamjua)
Subiri muda.
Makonda ni mropokaji tu,wakati ule aliwataja watu kibao kuwa wanauza ngada je kati yao nani alifikishwa mahakamani hadi leo? Huyu ni mbwakoko anabwekabweka tu.
 
Back
Top Bottom