Hili suala la viongozi kujipendekeza kwa Raisi Samia sasa limeanza kupita kiasi, na lisipodhibitiwa litaleta mtafaruku nchini.
Mfano ni hili suala la Raisi Samia kutukanwa. Siamini kabisa kwamba Raisi Samia anatukanwa, kwamba maneno ya kumkosoa na kumpa majina kama Mama Tozo sijui ni jambo jipya kwa raisi wa Tanzania ambalo halikuwahi kutokea kwa maraisi wengine. Kina Nyerere waliitwa Haambiliki; Mwinyi Koti; Mkapa Fisadi; Kikwete Dhaifu; Magufuli Dikteta Uchwara. Hakuna alieimba eti raisi anatukanwa. Huenda wapo watu wachache wanatukana kama ilivyokuwa kwa maraisi wengine, lakini kumbuka kuna viongozi nchini wametukanwa matusi mabaya na wakakaa kimya. Na baadhi ya waliotukana ni haohao wanaojifanya kuumizwa kuwa wewe unatukanwa.
Ninachoona kikitokea hapa ni viongozi kama Makonda na wengine kama yeye kutafuta kila namna ya kujipendekeza kwa Raisi Samia na kujifanya wana uchungu sana na yale wanayosema Watanzania dhidi ya Raisi Samia, na kuyakuza sana kuwa ni matusi, kama vile Raisi Samia ndie raisi pekee nchini kupitia vitu kama hivyo. Na pia matusi hayawi matusi au kuuma zaidi pale tu unapokuwa raisi.
Ninamtahadharisha Raisi Samia asiache watu hawa kuanza kuingia kichwani kwake, kwa kukubali huruma zao fake na kuanza kuwaona kama watetezi wake waaminifu. Asichoelewa Raisi Samia ni kwamba hawa watu wameshaiona saikolojia yake, kwamba anapenda kusifiwa kama ilivyo silka ya wanawake (maana sijawahi kumsikia akikemea kusifiwa kwa kufanya kazi yake) na sasa, zaidi ya kumsifia, wameamua kumwonyesha kuwa wanaumizwa sana na yanayosemwa dhidi yake.