Pre GE2025 Paul Makonda: Gambo usitake umaarufu wa kijinga, uwe unahudhuria vikao vya maendeleo Mkoa wa Arusha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nidhamu ni kutumikia wananchi mambo mengine Waafrica tunapenda kujitukuza tu!
Waziri ni mtumishi wa wananchi kama ni nidhamu anayestahili kupewa ni mwananchi!
Wewe ndo wale mkipata cheo mnataka kuabudiwa badala ya kutumikia wananchi!
Huyo Waziri ni nani mpaka umuone anastahili kuheshimiwa sana kana kwamba ukiwa Waziri basi sio mwanadamu wa kawaida!
Taifa hili linatakiwa liwaheshimu sana wananchi sio kuabudu viongozi!
 
Mbona mkuu wa mkoa mwenyewe anapenda kuheshimiwa tena sio kuheshimiwa tu anapenda kuabudiwa na kunyenyekewa, mtu anaye tafuta sifa huwa yupo hivyo , kama ingekuwa kweli wananchi kwanza madaraka nyuma basi msingekuwa mnawateka wanao wakosoa na kuikosoa mambo yake ya hovyo, mbona mnateka na kuuwa hao wananchi wakiyasema mabaya yenu kama kweli mnawatumikia wao?wapeni full power basi ili tujue kweli mnawatumikia kikamilifu, siyo kutafuta kukubalika kwa kuwachafua viongozi wenzio ukowa nyuma ya mtutu wa bunduki, Acha unafiki?
 
Unaushahidi au unaongea tu kwa mihemko!
Hao waliotekwa ni nani kawateka na kwa ajili ya nini mimi sijui!
Ila nakwambia tu mara nyingi watu kama nyinyi ndo mnasumbua sana mkipata nafasi.
Mzizi wa Mamlaka na uongozi ni watu na hao watu au wananchi ndo wanapenda kutumikiwa na kuheshimiwa!
Kwa hiyo kiongozi kushikwa bega na kiongozi wa umri na cheo karbia sawa ni urafiki na linaonesha bond kati ya viongozi,Hata Biden anapenda sana kushika mikono na mabega ya viongozi wenzake alkadharika Trump.
 
Kwa nini anaongea huku anamshika shika bega waziri kama mtu mdogo kwake?!
Huyu mkuu wa mkoa protocol hazijui au waziri hajui protocol
Kushikana shikari mabega ni kama anampa maelekezo waziri
 
Makonda hakumtendea haki Gambo.Mbunge hata kama analijua jambo linalohusu maendeleo ya jimbo lake,bado anatakiwa aliongee au aliulizie hadharani ili wapiga kura wake nao wapate taarifa ya kinachoendelea.
 
Huwezi kutumia maneno makali kwa kiongozi mwenzio mbele ya vyombo vya habari.
Napendekeza mheshimiwa Rais Samia, huyu RC Makonda atenguliwe.
Naaam.
 
Huwezi kutumia maneno makali kwa kiongozi mwenzio mbele ya vyombo vya habari.
Napendekeza mheshimiwa Rais Samia, huyu RC Makonda atenguliwe.
Naaam.
Hayo mawazo ni ya watu wajinga tu wasiopenda uwajibikaji!
Hata Zito Kabwe japo ni mpinzani bado hajaunga mkono hoja za Mrisho Gambo kujitetea!
Kwa kifupi Gambo ana sifa za kijinga!
 

DAB ni tatizo. japo Gambo naye ni walewale tu. shoe wine!

YESU NI BWANA&MWOKOZI
 
Paulo hapindishi live bila chenga unakula vyuma
 
Anakuja kuwa Boss wake ? Chongolo alikimbia mapema kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…