Paul Makonda: Hivi hili Taifa tutaacha lini kupenda Umbea, Majungu na Uongo?

Paul Makonda: Hivi hili Taifa tutaacha lini kupenda Umbea, Majungu na Uongo?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Anaandika Paul Makonda katika mitandao ya kijamii

Hivi hili Taifa tutaacha lini kupenda Umbeya, Majungu na Uongo. Na hata kama hakuna habari mbaya bado tunalazimisha tu ziwepo. Unaambiwa kabisa siyo kweli we bado unabisha tu ulazimishe ni kweli. Ona sasa ukitumia akili kidogo tu utagundua hata safari zinazosemwa ni za Utalii na wala siyo Matibabu. Ndani ya siku mbili ameingia Kenya [emoji1139] Nairobi hospital ndani ya siku mbili hizo hizo kafikishwa South Africa [emoji1221] ndani ya hizo siku yuko India [emoji1128] na sasa Germany [emoji629]. Haya ni matibabu au Utalii.

Ebu tuombeane Mema, ebu Tamani jambo jema kwa Mwenzako, huu ni wakati wa ku share habari njema na wala siyo kuongeza hofu na taaruki. Ebu tuombee familia zetu, ebu kila Mtu atafakari mahusiano yake binafi na Mungu, ebu wajulie hali ndg zako walioko vijijini na kama unanjia ya kuwasaidia ebu fanya jambo la kuwapa faraja ikiwezekana tafuta hata watu uliosoma nao wajulie hali Badala ya kupoteza bando lako kusambaza na kuulizia uzushi.Biblia inasema Shetani ni baba wa uongo, nina wasiwasi atakuwa na Watoto TANZANIA [emoji1241]

My Take
Nami naungana na Paul Makonda kukemea chuki na uongo. Ila kabla sijakemea nina mambo ya kuhoji.

1. Mbona mwahubiri upendo kwa baadhi ya watu tu? Humuoni kama mnaushangaza huo upendo na ndio maana umetoweka? Ulikuwa wapi upendo dhidi ya Ruge Mutahaba na Clouds Media ulioivamia na silaha za moto? Wewe Makonda umetajwa kwenye matukio mengi maovu ambapo baada ya kuondoshwa yalipungua. Ushahidi ni wewe kupigwa marufuku kuingia Marekani kwa kilichotajwa kukiuka haki za binadamu.

Upendo huo umekujia lini?
Unakumbuka kipindi cha vyeti feki, wakatumbuliwa wengi wewe ukaachwa. Upendo ikawa kwako tu. Hapo mlipanda chuki kiasi gani?

2. Mbona mwakataza uzushi kwa baadhi ya watu fulani tu. Pale anapozushiwa Mbowe kafa inakuwa sawa. Akizushiwa Lissu ni shoga inakuwa sawa,maana hatuwaoni mkikemea. Ila wakizushiwa wengine ndio noma yaani. Hamuoni kama mnaushangaza uzushi ndio maana unaamua kuwafanyia wehu? Wewe Makonda ulimzushia mtoto wa Mbowe ana korona. Nasema ulimzushia kwa sababu wewe hukuwa daktari. Unakumbuka ulipomzushia mzee Lowasa kuwa ametelekeza binti huko Kigamboni? Ukatengeneza movie kibao, hatujui ziliishia wapi.

Kabla ya hapo uliwazushia kina Mbowe madawa ya kulevya,kiko wapi?Mahakama ipi ikiwatia hatiani? Unakumbuka mlivyokuwa mnazushiana na Askofu Gwajima? Haaa haaa

Sasa imekuwa zamu ya dad kuzushiwa.

Siwatetei wazushi na wachuki ila nasisitiza Tupande amani na upendo kwa kila mtu, tupande haki na wajibu kwa kila mtu,halafu tusubiri kiangazi. Ila kwa sasa tunavuna tulichopanda. Usikute hata wewe wanakusubiri kwa hamu, ukutwe na baya wanywe bia.
 
Huyu hana udhu hata wa kumkemea jambazi sugu. Akiyofanya juu ya uhai wa Watanzania wenzetu ni ya kutisha kuliko hata Jombi wa Mbeya. Muuaji anahubiri kuombeana mema?

1. Kwa mema yapi aliyowaombea marehemu alioondoa uhai wao?
2. Kwa wema upi baada ya kuzushia wenzake vifo, magonjwa na madawa ya kulevya kwa sababu za kisiasa?
3. Kwa wema upi baada ya kuteka watu na kuwarejesha baada ya masharti magumu na vitendo vya kinyama dhidi yao?
4. Kwa wema upi baada ya kupiga wazee wanaoweza kumzaa kwa sababu ya tofauti ya maoni?

KWA WEMA UPI? UPI WEMA WA MAKONDA LEO ZAIDI YA UNYAMA KWA MASLAHI BINAFSI?
 
My Take
Nami naungana na Paul Makonda kukemea chuki na uongo. Ila kabla sijakemea nina mambo ya kuhoji.

 
Leo huwenda ukawa ni umbea kuulizia kama bado yu hai lakini bashite ajue watu wamejawa na chuki juu ya mkuu wa giza,ajue ni kweli watu wanaomba ni bora afe,watu hawaombi mazuri juu ya ibilisi kwani wametiwa majereha kila sehemu.

Swali la msingi hapa ni je kumuombea mtu kufa nako ni umbea?Ninyi endeleeni kuonea watu na kwakuwa majeshi na magereza yapo chini yenu,mahakama ni mali yenu,DDP mchukua pesa za watu naye wakwenu,ila mjue ya kwamba maombi ni maombi tu yawe ya heri ama ya Shari kuna siku Mungu atayasikia.

Kumbukeni ule usemi wa washirikina kwamba hata mganga wakienyeji naye anamwomba Mungu.Na sote ni mashahidi hata duwa za washirikina huwa zinatimia haijalishi ni za heri ama maonevu.Kikubwa ni lengo lamuhusika litimie haijalishi ninyi mtamuona ni wa imani gani.

Badilikeni acheni kuonea watu,acheni ubabe usio na maana kwani hii nchi ni yetu sote kila mtu anahitaji awe na furaha.Kwa mwendo huu wa watu kuishi kama digidigi hawataacha kuwaombea mfe.
 
Back
Top Bottom