PreGE2025 Paul Makonda kila Siku mahesabu yako ya kuwania Ubunge unayakosea na kuja Kujutia baadae

PreGE2025 Paul Makonda kila Siku mahesabu yako ya kuwania Ubunge unayakosea na kuja Kujutia baadae

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,685
Reaction score
128,178
Kazi pekee ambayo unaiweza na nashangaa kwanini Mama (Mwenyekiti CCM Taifa) Samia Suluhu Hassan hakuamini nayo ni ya kuwa Mwenezi wa CCM na nina uhakika kuwa hapa ungemsaidia mno na angekuja hata Kukushukuru baadae.

Labda nikusaidie tu kukuambia Makonda kuwa Siku zote Umaarufu wako unatokana na Nguvu ya Serikali hasa pale ukiwa Mkuu wa Mkoa kwakuwa Unaogopwa ila ukitoka tu katika Mfumo huna lolote na haraka mno tu Umaarufu wako nao unashuka na hata kuanza Kusahaulika mapema.

Kwa wenye Akili kubwa tunajua kuwa Mtifuano wako na Mrisho Gambo una Kishindo kikubwa cha Kushindwa huo Ubunge uutakao kwani endapo CCM itakuteua Wewe kugombea Ubunge na kumtema Gambo nina uhakika kwa Hasira Gambo atawahamasisha Wafuasi wake wampigie Kura zote Mpinzani atakayegombea kutoka ama CHADEMA au ACT kwa kile wana Simba SC tunachokiita UBAYA UBWELA na kupelekea Kushindwa Kwako vibaya.

Hakuna Watu WANAFIKI na MAFIA kama wa Arusha Mkoa ambao nimeuishi nikiwa Chalii huku hata Ubatizo wangu nao nikiupatia hapo katika Kanisa Katoliki la Kaloleni.

Yaani Watu wa Arusha waache kuwapa Kura ama Gambo wao au Lema kisha wakupe Wewe Kikaragosi mwenye Dharau, Matukio mabaya ya nyuma na Fisadi? Hizo Fedha zako Watu wa Arusha watazila zote bado katika Uchaguzi wa Ubunge kama ukigombea bado Watakutosa mazima.

Tunza huu Uzi wangu kwani najua hiki nilichokisema / nilichokiandika hapa kitajitokeza Kwako ndipo utajua na kuamini kuwa GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE "Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer" ni Habari nyingine kwa Maono na kunusa HATARI zijazo.
 
Back
Top Bottom