Paul Makonda kufikishwa Mahakamani Februari 3, 2022 katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka

Kwa hiyo leo RC akitoa tamko linalohusu Kina mama kulipa Hela wakati wa kujifungua Waziri wa afyaa hatakiwi kusema kitu???? Kwenye suala la kuvunja sheria mtu anawajibishwa na mamlaka iliyopo juu yake na sababu waziri wa habari ana dhamani hiyo bhasi nape alikuwa sahihi kukemea kile kitendo na kuomba tume ichunguze ila HAKUMFUNGULIA MASHTAKA so mahakama ndo ingemuita Makonda enzi zile lakini ndo hivyo Bongo bongo tuu sababu Paulo alikuwa kipenzi cha Baba yakatokea yaliyotokea.
 
Nadhani clouds walishatoa ushirikiano kupitia tume iliyoundwa na Nape. Na kumbuka Nape karudi pale pale kwenye nafasi yake.
Na unapokua unamchunguza kiongoz ni kwamba anakaa pembeni kwa uchunguzi hadi ukamilike. Nape alimweka pembeni makonda?Alichokua anafanya Nape ni utovu wa nidhamu na kutojua mambo yanaenda vipi.Rais ndio mwenye mamlaka ya kumweka pembeni RC na kuagiza vyombo vya sheria vimchunguze. Tunaona Kwa Sabaya, Rais alimweka pembeni Sabaya ndipo PCCB ikafanya kazi.Isingewezekana PCCB imchunguze Sabaya bila mamlaka yake ya uteuzi kumweka pembeni na kuamuru achunguzwe.Tukitoa Mihemko na mahaba tutaona Kwanini Nape alitumbuliwa.
 
Kufungua kesi ni jambo moja, ushahidi wa kumtia hatiani ni jambo lingine.

Hata kesi za ubakaji nyingi zinafika Polisi na Mahakamani changamoto inakuwa ushahidi.

Sidhani kama wale wa redio watajitokeza maana wale jamaa wanasomaga alama za nyakati, wakiona Gavoo haipo interested sidhani kama mtawaona.

Ile ya Mwenzake Saa mbovu ni tofauti kidogo maana Gavoo ilikuwa interested, na Mashahidi 'wale' akina 'Sahiid'ni rahisi kule juu kuwaambia "msiogope tupo"....na kina Mroso wale, Mchaga ukigusa pesa yake haogopi kitu liwalo na liwe.
 
RC akikosea, Waziri inatakiwa afikishe maoni yake kwa Rais juu ya mteule wake na sio yeye kuanza kumshughulikia.Elewa tu Kila kiongoz ana mamlaka yake ya nidhamu. Kuwa juu kicheo haina maana unaweza muajibisha wa chini.Unataka kusema Waziri anaweza muajibisha katibu mkuu wake?Unapounda tume ya uchunguzi LAZIMA mtu akae pembeni, Nape wakati anamchunguza makonda, alimweka pembeni kupisha uchunguzi?Jibu ni no,Sasa uliona wapi huo utopolo?
 
Nakumbuka jinsi makonda alivyokua mtu katika watu! Ukitaka kumuona anko magu ili iwe rahis bas lazima upite kwa makonda! Na ukitaka kumpata makonda upite kwa lemutuZ, hlf utakutana na walinzi kama kumi hiv ndipo umpate makonda! Nakumbuka kuna waheshimiwa fulan hiv tena wanawake walikua wanatumika kuuza ngada ilikua kila mara wanaenda kuripoti kwa makonda ila hawa ilikua wakifika tu pale ofisin kwake mlinz anawaambia jamaa yupo nenda tu! Aseee! Mtu kafukuzwa kazini anaenda kumuona makonda na anarudishwa kazin! Mtu kafungwa jela anaenda kumuona makonda na Anatole wa jela! Ukimuuzi makonda ujiandae kuhama nchi au kutumikia adhabu ya wazi kabisa!! Alikua anatembea na kajala akamuhonga noah walipoachana makonda akataka noah yake kajala akaenda kulia sana kwa nape kuwa makonda amsamehe asichukue gari! Dah! Kwel ile enzi makonda alikua mtu buahana!!
 
Muda mfupi baada ya Nape kumaliza kusoma ripoti yake kwa waandishi wa habari, Rais John Magufuli alitangaza kumfuta kazi.
Meaning mwenye 'kazi' hii alikuwa mh. Pombe, Makonda alitumwa tuu!
 
Pia tunaomba ajibu haya

1. Nani alimuua Ben, Azory, Mawazo Lwajabe.

2. Nani alimteka, Roma, Nondo, Mo,

3. Waliookotwa kwenye viroba ufukweni walikuwa akina nani

Kumbukeni huyu ndiye aliyekuwa anatoa taarifa kuwa Fulani atapatikana siku Fulani.
Na pia atuambie lini aliteuliwa kuwa hakimu wa kuhukumu wanaume kwenye mahusino na wapenzi wao?
 
Kwa wajuzi wa sheria, kwenye kesi kama hii ambayo ni criminal offense lakini anayeshitaki ni raia mwema...

Je, Makonda anatafuta yeye mwenyewe mawakili au anapewa mawakili na serikali?

Kama atatafuta yeye mawakili, gharama zake zitalipwa na anayefungua mashtaka au Makonda mwenyewe?
 
Yeye aliunda tume ya kuchunguza Uhalifu ule na sio Makonda...!! Kusemq asubiri ruhusa ya Rais inakuwa haina maana ya kuteuliwa kufanya majukumu ya kumiwakilisha Rais.. Bhasi niambie RC hawezi hana Mamlka ya kurekebisha maovu ya RAS..
 
Damu za marehemu zipo nae hadi mwisho.
Fanya dhambi zote na sio kuua
 
Laiti Jf ingekuwa na really registration and avatar sidhani kama wengi tungeandika kama hivi vinavyosomeka.

Although kwa kiasi kikubwa nimegundua zile tabia zetu za kiafrika ndizo zinaApply kwa kila event!.
 
Haya yote yataondoka ikija katiba mpya[emoji23]
 
Alikua mutu ya watu,, Lemutiz yeye ni Fixer forever, toto ya mujini[emoji851]
 
Alikua mutu ya watu,, Lemutiz yeye ni Fixer forever, toto ya mujini[emoji851]
 
Ile tume ilikua batili. Waziri hana mamlaka ya kuunda tume kumchunguza RC na ndio maana alifukuzwa kazi.Kila nafasi ina mamlaka yake ya nidhamu.Mfano leo RC aunde tume ya kumchunguza DC,hiki kitu hakipo.
waziri hakuunda tume kumchunguza RC, aliynda tume kuchunguza tukio la uvazi wa kituo cha clouds, kitu ambacho kilikua sahihi tu, kama makonda alitokea kweny uchunguzi wa tukio hilo ni matokeo ya uchunguzi lkn sio kua kachunguzwa yy
 
waziri hakuunda tume kumchunguza RC, aliynda tume kuchunguza tukio la uvazi wa kituo cha clouds, kitu ambacho kilikua sahihi tu, kama makonda alitokea kweny uchunguzi wa tukio hilo ni matokeo ya uchunguzi lkn sio kua kachunguzwa yy
Sijui kama unaelewa kilichoandikwa. Unaunda vipi tume ya kuchunguza tukio ambalo RC ni muhusika na asichunguzwe na wala kuwekwa pembeni?Nyinyi watu rudini darasani mkasome mambo ya uongozi na utawala bora na taratibu zake.Elewa hoja sio makonda kuhusika au kutohusika, Swala ni Waziri ana uhalali kwa alichofanya?
 
Waziri aliunda Tume ichunguze tukio.. Kama atashtakiwa na serikali au vip sio maamuzi yake yeye kazi yake ni kukemea uovu uliofanyika
 
Waziri aliunda Tume ichunguze tukio.. Kama atashtakiwa na serikali au vip sio maamuzi yake yeye kazi yake ni kukemea uovu uliofanyika
huyo jamaa anajifanya anajua sana wakati ni mtupu kichwani ndo maana niamua nimuache tu
 
huyo jamaa anajifanya anajua sana wakati ni mtupu kichwani ndo maana niamua nimuache tu
Mpuuzi tu anataka Rais ndo amkee makonda... Hajui hata kama rais anaowateua pia wanatofautiana mamlaka na wachini lazima amtii wa juu lakini wachini akijikuta mwamba ndo haya ya SABAYA...bashite nae yatamkuta tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…