Paul Makonda kufikishwa Mahakamani Februari 3, 2022 katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka

Paul Makonda kufikishwa Mahakamani Februari 3, 2022 katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka

ALIYEKUWA Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania, Paul Christian Makonda, sasa ameamriwa kufika mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kinondoni, Dar es Salaam, tarehe 3 Februari 2022, kujibu mashitaka ya jinai yanayomkabili.l

Taarifa kutoka Mahakama hapo na ambazo zimethibitishwa na mwandishi wa habari mwandamizi, Saed Kubenea, ambaye ndiye aliyefungua shauri hilo zinasema, tayari mhimili huo umetamtaka Makonda kufika siku hiyo.

Katika kesi hiyo ambayo imevuta hisia za wengi na kuibua mjadala mzito kila kona ya nchi hususani katika mitandao ya kijamii, Kubenea anamtuhumu Makonda kwa makosa mbalimbali.

Miongoni mwa makosa hayo, ni matumizi mabaya ya madaraka ya umma, wakati akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kesi dhidi ya Makonda, imesajiliwa mahakamani kama Miscellaneous Criminal Application Na. 1 ya mwaka 2022 na imepangwa kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi, Aron Lyamuya.

“Ni kweli kwamba kesi tayari imesajiliwa na kupangiwa hakimu wa kuisikiliza na kwamba, Mahakama imetoa amri (summons), inayomtaka Bwana Makonda kufika mahakamani, Februari 3 mwaka huu,” ameeleza Kubenea

Katika kesi hiyo, Kubenea anawakilishwa jopo la mawakili wakiongozwa na Nyaronyo Mwita Kicheere na Hekima Mwasipu.

Kupatikana kwa taarifa hizi kunakuja siku tatu, baada ya gazeti hili kuripoti kuwa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, imeziagiza Mahakama za Kinondoni na Kisutu, kufungua shauri la jinai dhidi ya Makonda.

Mahakama ilitoa maelekezo hayo, baada ya Kubenea kuandika barua ya malalamiko kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, akisema Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Kinondoni, zimegoma kufungua kesi yake.

Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Joseph Luambano, Januari 14 mwaka huu, ni kwamba Kubenea “anayo haki ya kufungua shauri hilo la jinai, iwapo anataka kufanya hivyo.”

Kabla ya hatua hiyo, Kubenea alikuwa amefungua shauri katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni na kusajiliwa kama – Miscellaneous Criminal Application No. 7/2021 – akiomba kuruhusiwa kumshitaki Makonda.

Aidha, Desemba 3 mwaka jana, akawasilisha maombi Mahakamani ili kuondoa shauri lake, kwa ajili ya kufanyia marekebisho baadhi ya maeneo, jambo ambalo Mahakama ililikubali; lakini katika mazingira ya kutatanisha, baadaye Mahakama hiyo hiyo, ikagoma kupokea kesi hiyo.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Makonda anadaiwa kuwa siku ya tarehe 17 Machi 2017, akiwa na watu waliobeba silaha za moto, alivamia Clouds TV na kumuagiza mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu kurusha video inayomwonesha mwanamke aliyejulikana kwa jina la Grace Athuman.

Katika video hiyo, ambayo haijulikani nani ameiandaa, mwanamke huyo alidaiwa kuonekana akifanya tendo la ndoa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

Kwa mujibu wa ushahidi wa video za CCTV, Makonda anaonekana kuvamia kituo cha Clouds saa nne usiku, akiwa anaendesha mwenyewe gari namba T553BFM.

Vilevile, Camera za CCTV pamoja na kitabu cha kumbukumbu za walinzi, vinamuonesha Makonda aliingia Clouds akiwa na askari wanne waliokuwa na sare tofauti za majeshi ya ulinzi na usalama, kati yao watatu wakiwa na silaha za moto.

Askari hao waliingia hadi chumba cha utangazaji, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za utangazaji, huku Makonda akitumia vitisho dhidi ya wafanyakazi wa Clouds kwa kutumia silaha za moto.

Kwa mujibu wa hati ya kiapo ya Kubenea, kitendo cha Makonda cha kuvamia televisheni ya Clouds, tena akiwa ameongozana na askari waliobeba silaha za moto, ni kinyume cha sheria ya Kieletroniki na Posta ya mwaka 2010.

Maombi ya kutaka kumshitaki Makonda yamewasilishwa mahakamani, chini ya kifungu cha 99 (1) cha Sheria ya mwenendo wa mashauri ya Jinai, Sura ya 20.

Kubenea ambaye amewahi kuwa mbunge wa Ubungo (Chadema), katika Bunge lililopita anasema, hatua ya Makonda kuvamia Clouds, ni matumizi mabaya ya madaraka, chini ya kifungu cha 96 ya Kanuni ya adhabu (Penal Code), Sura ya 20 na kuingilia moja kwa moja, mawasiliano ya Kieletroniki.

Mbali na Makonda, wengine walioitwa mahakamani siku hiyo, ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Wawili hawa wanadaiwa wameshindwa kuchukua za kumfungulia mashitaka ya jinai mtuhumiwa huyo.

Maombi ya kumshitaki Makonda yameambatanishwa na wito maalum (Chamber Summons) na hati ya kiapo (Charge Sheet).

Katika kujenga hoja yake mahakamani, wakili wa Kubenea ameambatanisha ripoti ya uchunguzi ya Kamati Maalum iliyoundwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye.

Ripoti ya Nape iliyochunguza tukio la kuvamiwa Clouds, ilimtia hatiani Makonda na kupendekeza kwa mamlaka yake ya uteuzi, kumchukulia hatua za kinidhamu; Makonda mwenyewe kuwajibika binafsi na kuwaomba radhi Clouds na wananchi kwa ujumla.

Hata hivyo, mapendekezo yote ya Kamati ya Serikali hayakutekelezwa. Muda mfupi baada ya Nape kumaliza kusoma ripoti yake kwa waandishi wa habari, Rais John Magufuli alitangaza kumfuta kazi.

Nape alirejea kwenye baraza la mawaziri wiki iliyopita, kufuatia Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye alishika madaraka ya urais baada ya kifo cha Magufuli, kuamua kumrejesha katika wizara hiyo.

Kamati ya Nape ilithibitisha kuwa Makonda alivamia kituo hicho cha televisheni akiwa anaendesha mwenyewe gari lenye namba T553 BFM na kuingia hadi chumba cha utangaji, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za utangazaji.

Tangu kuripotiwa kufunguliwa kwa shauri dhidi ya Makonda, kumekuwa na matukio mbalimbali yanayojitokeza. Katika gazeti la Jumatano iliyopita, wakili mwingine wa kujitegemea, Peter Madeleka, alinukuliwa akisema, yuko tayari kujiunga na mawakili wengine watakaoteuliwa na Kubenea, kuendesha kesi hiyo.

Madeleka ambaye alikuwa ofisa wa Jeshi la Polisi alisema, anataka kutumia ujuzi wake wa kisheria na kiuchunguzi, kuendesha kesi hiyo aliyoita, “imebeba maslahi ya taifa.”

“Lengo siyo kushinda tu. Kesi hii, inalenga kuzionyesha mamlaka za kuendesha mashitaka ya Jinai (DPP), kwamba kuna mtuhumiwa mmoja anastahili kuburuzwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili. Lakini hawajaweza kufanya hivyo na kunyamaza kwao, ni kuvunja Ibara ya 59 (B) Ibara ndogo ya (4) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano,” ameeleza Madeleka.

Alisema, “ikumbukwe kuwa hata mataifa makubwa kama Marekani, yamewahi kumuwekea vikwazo vya kwenda nchini humo Makonda na familia yake, kutokana na tuhuma za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

“Pamoja na Marekani kuwa taifa mshirika na Tanzania kwenye mambo kadhaa kihistoria, pamoja na uwezo wa Marekani kuweza kutambua mambo mbalimbali yanayotokea duniani, lakini serikali imeshindwa kufanyia kazi taarifa ya Marekani kuhusiana na matendo ya Makonda.”

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, 31 Januari 2020, ilieleza kuwa serikali ya nchi hiyo, imempiga marufuku Makonda na mke wake, Mary Massenge, kufuatia tuhuma za ukandamizaji wa haki za wananchi; kunyima watu haki ya kuishi, haki ya uhuru wa kujiamulia mambo na usalama wa watu.

“Wizara ina taarifa za uhakika kuwa Makonda amehusika katika uvunjifu huo wa haki kupitia nafasi yake kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Katika nafasi yake hiyo, pia amelaumiwa kwa kukandamiza upinzani wa kisiasa, kukandamiza haki ya kujieleza, na kushambulia makundi yasiyo na sauti,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Michael Pompeo alitumia mtandao wake wa Twitter kutangaza marufuku hiyo.

Alisema, “…leo tumetangaza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Christian Makonda, hataruhusiwa kuingia Marekani, kutokana na kushiriki kwake katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.”
Haya tusubiri kuona kitakachotokea "under this current politically compromised judicial system".
 
View attachment 2093416

Here are the facts about the universe I am sure you don’t know about.
..................................

Jua kumbe alipo still na lenyewe linazunguka galaxy kwa speed ya kilometre 210 kwa sekunde. Galactic year for the sun ni sawa na miaka 230 ya dunia.

Kwa maana hiyo sasa dunia, sayari zote na kila celestial body ndani ya solar system vinalikimbiza jua kwa speed yake 210km/second.

Hapo hizo celestial bodies linaizunguka jua; dunia kwa mfano inatumia siku 365 na kwenye kufanya ivyo inaenda 67000 miles per hour, hapo hapo tena dunia inazunguka katika mhimili wake 1000m/h (wewe unaishi kwenye surface ya dunia wala uoni kitu).

Halafu kuna masela huko NASA kwa kutumia law of physics and applied mathematics modelling wanatengeneza chombo kinaitwa ‘Parker Solar Probe’ jamaa kwa hesabu zao wanakwambia hiko chombo wakitaka kifike karibu na jua haraka wakipeleke kwanza Jupiter na kutumia magnetic fields zake kitakipeleka mapema zaidi kuliko kwenda moja kwa moja through Venus and all that requires timing,

Kifaa kinaruka kinakwenda mpaka Jupiter na kweli kinapelekwa mpaka wanapotaka siku zile zile zilizopangwa. Kinanasa kwenye gravity ya jua kama walivyopanga, wanakifungua wakati wapo million miles apart, kina record; all that just to learn about the outer core of the sun solar flares (not sure ata unajua impact zake kwa dunia ili wachukue tahadhari).
............. ............

What’s the point of all that, there are so many things to amuse the mind with kuliko uthenge mnaojaza kwenye vichwa vyenu yaani binafsi inanisikitisha how is it possible kuna binadamu wapo so shallow minded.

I don’t understand yaani mtu unapata wapi muda wa kuangaika na binadamu mwingine, seriously. Ama kweli akili ni nywele na kila mtu na zake.
Gazeti reeeefu,la kutumia Kama toilet paper.
 
This post appears to be the best post of the year in JF. However, sijacheki kuona kama details ulizoziweka kwenye post hii ziko sahihi ama la. Still, I believe they might be more than correct
 
Waziri aliunda Tume ichunguze tukio.. Kama atashtakiwa na serikali au vip sio maamuzi yake yeye kazi yake ni kukemea uovu uliofanyika
Hilo tukio alikua anawachunguza akina nani kama sio wafanya tukio ambo ndio RC?Sielewi mnaongea vitu gani.
 
Hilo tukio alikua anawachunguza akina nani kama sio wafanya tukio ambo ndio RC?Sielewi mnaongea vitu gani.
Wewe Pale ulimuona makonda tu???? Kulikuwa na wanajeshi pia... So uchunguzi ni kujua nani kafanya tukio akishirikiana na nani kwa lengo gani.. Baada ya hapo ripoti akabidhi kwa Rais sasa yeye atajua kama anamtengua kwa makosa yake na kisha ashtakiwe au aendelee kumlea kama mwanae mpendwa
 
Tukio lilikua wazi Makonda (RC)Akiwa na walinzi wake walienda Clouds usiku. Unataka uchunguzi wa nani kafanya tukio kivipi tena?Hoja yako ingekua na LOGIC kama makonda angekuwepo sehemu ya wafanya uchunguzi. Kinyume cha hapo ni kwamba Makonda na walinzi wake walikua wanachunguzwa, Sio kitu kibaya kuchunguzwa lkn je WAZIRI ana mamlaka ya kuunda tume ya kuchunguza tukio ambalo RC yumo ndani yake?
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mkuu hata tume Haruhusiwi kuunda yani???????? Khaa wee jamaa bhanaa...

Huku kwenye Mikoa kila siku tume zinaundwa kuchunguza wizi kwani kwenye List ya kuhusu mapokezi ya hela na matumizi Wakuu wa mikoa..maras na wakurugenzi hawapo?????

Wewe achana na mambo ya Kudhani mtu akiteiliwa na rais anakuwa kama mungu mtu vilee. Wewe walinzi wa makonda unawajua?? Huwa wanavaa kadet za jeshi na kubeba bunduki eti... Yani we jamaa bhana
 
Waganga waliokula pesa zake walaaniwe.
Mganga ni mfanyabiashara mtaji wake ujinga wako
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mkuu hata tume Haruhusiwi kuunda yani???????? Khaa wee jamaa bhanaa...

Huku kwenye Mikoa kila siku tume zinaundwa kuchunguza wizi kwani kwenye List ya kuhusu mapokezi ya hela na matumizi Wakuu wa mikoa..maras na wakurugenzi hawapo?????

Wewe achana na mambo ya Kudhani mtu akiteiliwa na rais anakuwa kama mungu mtu vilee. Wewe walinzi wa makonda unawajua?? Huwa wanavaa kadet za jeshi na kubeba bunduki eti... Yani we jamaa bhana
Hakuna tume inayoundwa na Waziri kumchunguza RC akiwa bado madarakani.Kunapotokea kuna shida kwa RC,Waziri huwasiliana na mamlaka yake ya uteuz ambayo ni Rais na Rais anaweza mtumbua au kumuundia tume. Kuna Itifaki ktk utumishi wa umma. Kabla ya Magufuli, uliwahi sikia wapi Waziri kaunda tume kumchunguza RC au tukio ambalo RC naye ni mhusika na anatakiwa kuhojiwa?
 
Pia tunaomba ajibu haya

1. Nani alimuua Ben, Azory, Mawazo Lwajabe.

2. Nani alimteka, Roma, Nondo, Mo,

3. Waliookotwa kwenye viroba ufukweni walikuwa akina nani

Kumbukeni huyu ndiye aliyekuwa anatoa taarifa kuwa Fulani atapatikana siku Fulani.
KILA kitu kitakuwa wazi hawana Kinga tangu shetani apigwe minyororo
 
Siumii kwa lolote bali nawashangaa ninyi kwa kumsakama mtu ambaye hana madhara. Kiukweli, mnamkubali Makonda alikuwa JEMBE NA HAMTAMUWEZA!
Hana madhara kwa nyie mlionufaika.
Makonda ndie chanzo cha watumishi kufukuzwa Kazi kwa uonevu
 
naye atakuwa mjinga kama bado yuko nchini!!
Hana ujanja wa kuishi nje ya nchi,kwa pesa gani aliyonayo.
Hawana ujanja wa kuishi nje ya mshahara na kupewa hawa.
Kuishi kwa kupora ni tofauti na kuishi kwa kumake.
 
Imekua kama fasheni sasa kwa wanasiasa walio nje ya ulingo kuitumia mahakama kama daraja la kuwarejesha kwenye umaarufu wao.

Kesi ya Mbatia na hii ya Kubenea zote zinafanana kwa maana kwamba hazina tija yeyote.

Mahakama ilinde heshima yake kwa kufutilia mbali kesi za aina hii zenye harufu ya kisiasa na zinazotumika kuwapa umaarufu wanasiasa.
Kama imewezapokea ya Mbowe isiyo na ushahidi kwann isipokee ya makonda yenye ushahidi
 
Acha ujinga huo. Kwahiyo hao ndio wana ushahidi wa yeye kuvamia Clouds? Mbona Clouds wenyewe wamejitoa kuwa hawahusiki na lolote kuhusu kuvamiwa? Ikitokea wakaitwa wakasema hawajawahi kuvamiwa, hao matajiri watalazimisha? Eti matajiri watasema walilazimishwa kutoa hela, je wanaweza kuonesha jinai hapo? Hapo ushahidi ni JPM. Yupo kuthibitisha au kukanusha? Pumbavu!!!
Watatrace simu zake ushahidi wote upo mle.
 
Civil case only kudai hasara ya utapeli sio criminal offence ya kutaka jamaa aende jela ilo inabidi niende polisi walichukue.

Kesi ya jinai inafunguliwa na jamuhuri pekee.

Na civil case inataka relationship kitu ambacho Kubenea hana na Clouds.

Tusiache watu waharibu namna mambo yanavyotakiwa kuwa kisa visasi. Makonda kama ana makosa ashitakiwe na watu sahihi sio huu upuuzi.
Waliopo nyuma ya kubenea ndo wenye nguvu.
Kisasi ni muhimu Ili kuibalance Jamii isitende uovu.
 
Itumike busara ili isijeonekana kama kulipizana visasi.
La msingi ni kupima kwanza mazuri aliyofanya na mabaya yake ili upatikane uzani.
Na kama uzani utabalance ni mara mia kupotezea kwa kutoa tahadhali/notification kwa mamlaka za uteuzi kufanya review/kuangalia upya vigezo vya uteuzi/vetting ili baadae yasijirudie makosa mengine ya utendaji kwa wateuliwa.
Bila kisasi hakuna haki.
Vipi wale wajane na mayatima machozi yao yanafutwa na nani.
Ufanyi makosa kwa kujifichia kwenye mazuri.
Yapi ya faida aliyofanya zaidi ya propaganda binafsi
 
Hii ndiyo inaitwa open and shut case- Makonda hachomoki, ushahidi nje nje kudadeki!
 
Back
Top Bottom