PreGE2025 Paul Makonda: Msigeuze makanisa kuwa viwanja vya siasa

PreGE2025 Paul Makonda: Msigeuze makanisa kuwa viwanja vya siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,659
Reaction score
90,151
My Take
Nakubaliana kabisa na Paulo ,hao wanaojiita Maaskofu kazi zao ni porojo za Kisiasa kushabikia Wapinzani huku wamemsahau Yesu.

Wakidhibitiwa watasema uhuru wa dini unainhiliwa wakati wanageuza majukwaa ya dini kufanya siasa.
===================
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ametoa wito kwa viongozi wa dini na waumini kuhakikisha wanazingatia na kufuata mafundisho ya Mungu badala ya kutumia maeneo ya ibada kama majukwaa ya kisiasa, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Ameeleza kuwa kuna ongezeko la baadhi ya viongozi wa dini kuingiza siasa katika mahubiri yao, jambo ambalo linaweza kusababisha migawanyiko na taharuki miongoni mwa waumini."Watumishi wa Mungu niwaombe sana kwa unyenyekevu mkubwa, semeni yale Mungu amewaagiza kusema kupitia roho Mtakatifu na sio yale tunayowaambia sisi wanasiasa kwa kuwa yale yanayotoka kwa Mungu ni maneno yenye uponyaji." Amesema.

Aidha, amewaomba viongozi wa dini kutumia nafasi yao kuhubiri amani, upendo na mshikamano, hasa wakati huu ambapo taifa linaelekea kwenye kipindi nyeti cha uchaguzi Akisisitiza kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuimarisha umoja wa kitaifa kwa kuepuka lugha au matendo yenye viashiria vya uchochezi wa kisiasa.

 
My Take
Nakubaliana kabisa na Paulo ,hao wanaojiita Maaskofu kazi zao nk porojo za Kisiasa kishabikia Wapinzani.

Wakidhibitiwa watasema uhuru wa dini unainhiliwa wakati wanageuza majukwaa ya dini kufanya siasa.

View: https://x.com/Mwanahalisitz/status/1913637074068226320?t=SGcTTKHtGBB9MGwq5xxGcw&s=19


..yote hayo ni kwasababu hakuna HAKI nchini.

..viongozi wa Kidini kuingilia siasa ni dalili za watawala kufilisika kifikra na kukengeuka kiuongozi.

..kuna OMBWE na viongozi wa dini wameamua kuliziba.
 
..yote hayo ni kwasababu hakuna HAKI nchini.

..viongozi wa Kidini kuingilia siasa ni dalili za watawala kufilisika kifikra na kukengeuka kiuongozi.

..kuna OMBWE na viongozi wa dini wameamua kuliziba.
Haki ipi ambayo haipo? Makanisa yasifanye siasa
 
Aache ujinga,a some bibilia aone Mitume na manabii wa zamani walivyokuwa wanawakemea Wafalme kwa uovu wao
 
Back
Top Bottom