My Take
Nakubaliana kabisa na Paulo ,hao wanaojiita Maaskofu kazi zao ni porojo za Kisiasa kushabikia Wapinzani huku wamemsahau Yesu.
Wakidhibitiwa watasema uhuru wa dini unainhiliwa wakati wanageuza majukwaa ya dini kufanya siasa.
===================
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ametoa wito kwa viongozi wa dini na waumini kuhakikisha wanazingatia na kufuata mafundisho ya Mungu badala ya kutumia maeneo ya ibada kama majukwaa ya kisiasa, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Ameeleza kuwa kuna ongezeko la baadhi ya viongozi wa dini kuingiza siasa katika mahubiri yao, jambo ambalo linaweza kusababisha migawanyiko na taharuki miongoni mwa waumini."Watumishi wa Mungu niwaombe sana kwa unyenyekevu mkubwa, semeni yale Mungu amewaagiza kusema kupitia roho Mtakatifu na sio yale tunayowaambia sisi wanasiasa kwa kuwa yale yanayotoka kwa Mungu ni maneno yenye uponyaji." Amesema.
Aidha, amewaomba viongozi wa dini kutumia nafasi yao kuhubiri amani, upendo na mshikamano, hasa wakati huu ambapo taifa linaelekea kwenye kipindi nyeti cha uchaguzi Akisisitiza kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuimarisha umoja wa kitaifa kwa kuepuka lugha au matendo yenye viashiria vya uchochezi wa kisiasa.