Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Nawashauri sana viongozi wa serikali, mimi ninaishi Songea, ninasoma mitandao ya kijamii lakini nasikiliza maoni ya watu mitaani, vijiweni na hata kwenye viwanja vya mpira.
Paul Makonda anapendwa sana kwa namna anavyotumia kipawa chake kutatua kero za wananchi, kwa namna anavyosikiliza na anavyochukua hatua, wananchi wengi wa kawaida wanavutiwa sana na style yake ya uongozi, nataka kuwaambia viongozi wanaomsaidia Mhe. Rais kuwa imani ya wananchi kwa serikali kwenye mkoa wa Arusha imekuwa kubwa sana kutokana na uwepo wa Makonda.
Hivi majuzi tu Makonda amesaidia Zimamoto magari, Makonda huyo huyo amewezesha Polisi kupewa pikipiki, Makonda huyo huyo anatatua kero za maji, anasimamia rasimali za umma, amesema kila mwezi wanatoa taarifa za utendaji kazi kwa Waziri wa Tamisemi namna walivyosikiliza na kutatua kero, sasa unaenda kwenye mkutano kusikiliza kero unaambiwa kuna watu wamekula milioni 52, hapo unatatua kero kwa kuwavumilia wezi? Kwamba warudishe kwa muda ambao Mkurugenzi alimwambia RC?
Kwa namna ninavyofuatilia siasa za mkoa wa Arusha kwa elimu yangu ndogo, inaonekana kuna ubadhirifu mkubwa mnoo. Gambo akiwa mbunge amepambana hadi ameonekana mkorofi na anagombana na viongozi lakini tangu Makonda aingie Arusha, Gambo amekaa kimya kwa sababu anajua Makonda ni kama yeye, anajua ubadhirifu wote Makonda anaumaliza, Makonda ataufyeka mtandao wote wa wezi kule Arusha.
Wananchi kote kote sio Arusha tu, Makonda alipokuwa Mwenezi wa CCM wananchi walikuwa wanamsubiria mno kwenye maeneo ambayo hakupita, kwa sababu wanaona ndio mwenye roho ya paka.Serikali naiomba sana haya maneno ya kijinga kuwa anadhalilisha wanawake ni ya kifala sana, hao LHRC, Maria Sarungi na wengine wanaomponda Makonda wana wafadhili wao wanawatuma, Rais katukanwa sana na Mange Kimambi, Rais katukanwa na anatukanwa sana mama wa watu hadi sisi wengine tunajisikia vibaya lakini wapumbavu kama Maria Sarungi hawajitokezi kulaani wala hao wanaojiita watetezi wa haki za binadamu.
Tunataka viongozi wa aina gani sisi watanzania? Mbona kama tumerogwa hivi?