Paul Makonda Ndiye Mwanasiasa kijana Mwenye ushawishi na Ujasiri Mkubwa Barani Afrika

Paul Makonda Ndiye Mwanasiasa kijana Mwenye ushawishi na Ujasiri Mkubwa Barani Afrika

Ndugu zangu Watanzania,

Kuna wakati mwanasiasa kijana kutokea Afrika ya kusini Julius Malema alionekana kama ndiye kijana jasiri zaidi hapa Barani Afrika na ambaye alikuwa akilitetea hata Bara zima la Afrika hususani vijana wa ki Afrika, na kwa hakika wengi walitamani kuwa kama kijana huyo anayeongoza chama cha EFF kwa sasa, na ambaye amewahi kuwa mwanachama wa ANC na kiongozi wa vijana wa ANC kabla ya kufukuzwa uwanachama,Lakini kwa sasa kibao kimegeuka kabisa.

kwa sasa Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda ndiye Mwanasiasa kijana anayetajwa kuwa jasiri sana kuwahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni. Ni jasiri kwelikweli mithili ya wale makomandoo waliopikwa na kuivishwa kisawasawa kijeshi na kimedani kutoka Marekani waliokwenda Pakistani kwenda kupambana katika ngome ya Gaidi namba moja Duniani Osama Bin laden huku Rais wao akiwa anawatizama kutokea ikulu ya whitehouse Marekani namna wanavyopambana huku wakiwa wamelibeba Taifa lao mabegani mwao.

Haijapata kutokea hapa nchini kwa miaka ya hivi karibuni kuona kijana ambaye jina lake likitajwa kwenye taarifa ya mkurugenzi mkuu wa mawasiliano ya Rais ikulu katika uteuzi wa aina yoyote ile linatetemesha ,kutikisa na linateka habari zote mitaani,vijiweni,makanisani,virabuni, bar, shuleni, masokoni,viwanjani na kuzima mijadala yote mitaani inayokuwa inaendelea na kubakia yeye tu akitamba na kutawala katika medani za kisiasa ,utafikiri jeshi la Tanzania lilipokuwa linaingia katika ardhi ya Uganda kumsaka kwa hasira na uchungu mkali huku mioyo yao ikibubujikwa machozi ya hisia kali za uzalendo ili kumnasa Nduli Iddi Amini Dada.

Makonda ni Mwamba ni Mwamba kwelikweli ni Jabali la siasa ni fundi wa siasa, ni komando. Ni field Marshall wa siasa za Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania.

Ni kivutio na mfano halisi wa kijana jasiri na mzalendo wa kweli. Jina lake tu ni kama Taasisi ,ni mkubwa kuliko Sacco's kama CHADEMA nzima.

Anao ushawishi ambao sijapata kuuona wala kuushuhudia ,anakubalika utafikiri pesa. Ana nguvu iliyo kubwa sana ndani yake. Akiunguruma nchi nzima inatikisika na kubaki ikifanya mjadala tu juu yake.

Mwamba Makonda anazima na kufunika hadi habari za simba na yanga? Huyu mwamba siyo mtu wa kawaida, Mungu amempatia kibali cha kipekee kabisa na Karama ya uongozi.ndio maana ya kuona na kushuhudia namna alivyo na ushawishi na nguvu kubwa ya kisiasa.

Hata ukimtizama anapozungumza tu unaona kabisa huyu ni zaidi ya kiongozi,ni kiongozi mwenye mamlaka tokea ndani yake.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

View attachment 2951049View attachment 2951052View attachment 2951055
Umetumia takwimu gani au unaongea tu !
 
Ndugu yangu, hawapendi umtaje Mwamba wa Afrika, JPM. Jina la JPM linawatisha Viongozi wabovu, Mafisadi, Majizi na wapumbavu wengi waliopo kwenye mfuko.
Kwa hali ilivyo sasa, ukimtaja tu JPM, kama upo kwenye nafasi ya uteuzi, kesho yake uteuzi unatenguliwa.
By the way, "WA MBILI HAVAI MOJA"
Mungu akupe nguvu za kutokurudi nyuma kumtetea JPM, Mwamba wa Afrika.
 
Daah anayepewa pole bado ana ulaji tena eneo analolipenda sana
 
Ndugu yangu, hawapendi umtaje Mwamba wa Afrika, JPM. Jina la JPM linawatisha Viongozi wabovu, Mafisadi, Majizi na wapumbavu wengi waliopo kwenye mfuko.
Kwa hali ilivyo sasa, ukimtaja tu JPM, kama upo kwenye nafasi ya uteuzi, kesho yake uteuzi unatenguliwa.
By the way, "WA MBILI HAVAI MOJA"
Mungu akupe nguvu za kutokurudi nyuma kumtetea JPM, Mwamba wa Afrika.
HAYATI JPM NI KIPENZI CHA WATANZANIA WALIO WENGI. JAPO KIMWILI HATUKO NAYE, LAKINI ANGALI AKIISHI MIOYONI MWETU.
MAKONDA ENDELEA PALE PALE ULIPOISHIA.
 
Kusema ukweli Makonda ni Scofield wa CCM lakini Julius Malema ni habari nyingine

Makonda ni mtu wa 'aina yake' katika kufanikisha 'mission' ya nature na aina yoyote kwa kiwango kinachohitajika. Makonda ni 'wa pekee' na aina yake katika 'medani'

Nachotaka kusema hapa ni kwamba hata CHADEMA wakichukua nchi leo bado Makonda hatoachwa kamwe bila kazi ya kufanya!

Nafikiri tumeelewana ndugu zangu!
 
Mheshimiwa Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda Ni kiongozi mwenye maono makubwa sana na uzalendo wa hali ya juu sana.ni kiongozi mwenye ujasiri na ushupavu mkubwa sana katika kutekeleza na kutimiza maono yake yenye maslahi mapana kwa Taifa letu na yenye matokeo chanya kwa ustawi wa jamii nzima.
Kasharudisha zile nyumba alizopora kwa GSM? ni huruma ya mama tu, hiyu alipaswa kuwa Segerea.
 
Timu ya mtu 3 ambayo ikiaminiwa na kupewa madaraka nchi na taifa itafika mbali sana, 1Makonda, 2Polepole 3Gwajima. Ongeza na wewe
 
Mheshimiwa Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda Ni kiongozi mwenye maono makubwa sana na uzalendo wa hali ya juu sana.ni kiongozi mwenye ujasiri na ushupavu mkubwa sana katika kutekeleza na kutimiza maono yake yenye maslahi mapana kwa Taifa letu na yenye matokeo chanya kwa ustawi wa jamii nzima.
Namba yako tunayo, wala usijali endelea kuropokwa. Naona Tulia Ackson kakupiga stop
 
Back
Top Bottom