Pre GE2025 Paul Makonda ni Karata ya muhimu kwa Rais Samia kuelekea uchaguzi wa 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbona kwa sasa kama mnafanya kampeni peke yenu na mnajipima kwa kutoa max wenyewe?
Mna haha bure wakati wengine hawajaweka madhaifu yenu hadharani?
1. Hivi CCM inategemea kupata kura zozote kutoka kwa vijana waliomaliza masomo 2015 hadi leo? Hawa ambao wamekosa ajira, mitaji ya kibiashara wala support yeyote? Mmejiuliza ni % ngapi ya wapiga kura?
2. Watumishi wa umma waliopo kwenye ajira (zisizo na mianya ya wizi) na wastaafu ambao hatima za pension zao zimeminywa mnategemea kura zao?
3. Boda na wamachinga hao mnaoona wanawasindikiza kwa mbwembwe mkiwapa mafuta na incentives mnadhani ni wenu hao? Ni % ya wapiga kura?
Sasa ngoja hizo kampeni zikianza wapinzani watakapo weka uchafu wote mezani kama wananchi hawaja watapika. Ushindi wa CCM na huyo mama yenu unategemea kupora uchaguzi kama 2020 ndio maana tume huru hamuitaki wala katiba mpya.
Ila nadhani safari hii yale ya 2020 yakifanyika ni sawa na kuonja sumu, [emoji879]

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Huyo Mama anaewachekea Wapigaji? na huyo Makonda ambae ni Mwizi wa Pesa za TASAF na Muuaji na Mtekaji wa Wananchi?

Acheni kutuona MAZEZETA.
zezeta ni mtu aisie na mipango ni wa manung'uniko, mihemko na malalamiko with non stop kwa tafsiri yangu 🐒

hana impact yeyote zaidi ya kuzira na kususa
 
zezeta ni mtu aisie na mipango ni wa manung'uniko, mihemko na malalamiko with non stop kwa tafsiri yangu 🐒

hana impact yeyote zaidi ya kuzira na kususa
Hebu ache HADAA akubali tuwe na TUME HURU YA UCHAGUZI aone kama kuna Mtu atalalamika?

Hatulalami tuu for the sake ya kulalamika.
 
Macky Sal katesti mitambo leo Dakar Senegal Maandamano ya Hataree mbona sisi tunachezewa.
 
Hebu ache HADAA akubali tuwe na TUME HURU YA UCHAGUZI aone kama kuna Mtu atalalamika?

Hatulalami tuu for the sake ya kulalamika.
mwenye hadaa ni wewe unaoita waliotofauti na mtazamo na matamanio yako mazezeta 🐒

tume ipi na mliikimbia na kususa bunge la katiba ambalo lilikua na tume ambayo hakuna ata moja ambae hakuiridhia 🐒

Mnadandia treni kwa mbele Lazima muonje jotro ya jiwe ya kususa..
 
Dhana ya kupora uchaguzi ni dhana mfu,na haina ukweli wowote,ni watu wajinga tu ndio wanaweza kuamini upuuzi na ujinga kama huo.
 
Karata kwenye kumaliza tatizo la ajira owa vijana? umeme? au unazungumzia maigizo ya kuwafanyia wapumhavu waTaifa hili ambao ni asilimia 90
 
Tatizo ni kuwa wengi wanaodai katiba mpya hawamaanishi kutoka moyoni na hiyo ni kwasababu ya tamaa zao yaani wanalizungumzia jambo ili serikali iwape chochote kitu.
NO ONE IS REAL.
Typical. Talking points za CCM.
 
CCM wanasababisha matatizo kwa kiasi fulani sikatai lakini kwa kiasi kikubwa ni wananchi ndio wameacha hayo yatokee.
Yaani kwa kifupi wananchi wameamua bora shetani uliyemzoea kuliko malaika usiyemjua.
Mkuu kazi yako ni kueneza talking points za CCM, sio?

Eti “CCM ni mbovu lakini hata wapinzani ni wale wale tu. Bora kubaki na CCM”! Hakuna mbadala!

Huo SIO msingi wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Mtu mmoja (individual) haiwezi kujua na kusema wananchi wanataka nini! HUO NI USHIRIKINA.

Acha uchaguzi huru na wa haki uonyeshe kile hasa wananchi wanachofikiri na kutaka.
 
Dhana ya kupora uchaguzi ni dhana mfu,na haina ukweli wowote,ni watu wajinga tu ndio wanaweza kuamini upuuzi na ujinga kama huo.

Hii sio dhana na ushahidi wa huo uhayawani upo. Ukiona ccm wanalazimisha kujimilikisha tume ya uchaguzi ujue hii ndio sababu.
 
Wenye akili timamu wanasema kuwa hakuna namna inayooneka na isiyoonekana ya kumuezesha mama Samia kurudi madarakani 2025 ikumbukwe kuwa taarifa hizi ni za jikoni, ujinga wa kusifia Hadi upuuzi umeachwa uendelee bila bughudha lakini 2025 jina la mama halitorudi and will be blow surprise to her majest and excellence even to those embedding her to be embedded.
 
Ninacho maanisha mkuu hapo ni kuwa Wananchi wameamua kwa maana bado wengi katika wananchi hawana utayari wa kuwaondoa CCM Madarakani na laiti kama wananchi wangekuwa na utayari hakuna haja ya kusubiri uchaguzi ungeshaona alert kungekuwa na Maandamano kila week kila mkoa.
Lakini jaribu kuangalia hali ya wananchi ilivyo, Mfumuko wa bei, Umeme lakini NO ONE REACT Ni Kama raia wamekubali CCM iendelee kuwaburuza
 
Vipi lakini mkuu yeye mwenyewe her majesty kwani anataka kuendelea 2025?
 
Kama tutaanza kuitana Ndugu fulani au Comredi fulani itapendeza sana !!
Hii kila mtu ni Mheshimiwa Naona haipendezi isipokuwa labda kwa wale wakubwa Zaidi wa Nchi hii 😅🙏🙏
Ni maoni yangu tu !!
 
Watu Nchi hii ni waoga hawako tayari kurisk kushiriki kwenye maandamano !
Ila kwenye matusi hapo tunaweza sana kutukanana !!
 
Kwa namna fulani uko sawa. Ingawa kwa upande mwingine unaweza kuona kuwa wananchi wameshaona jinsi serikali ilivyoandaa majeshi yetu kutesa, kujeruhi na hata kuua wale wote wanaopinga yake. Matukio ya 2001 kwenye uchaguzi mkuu kule Pemba; mauaji ya Mwangosi, Akwilina, risasi za Lissu, n.k. Na mengi mengine dhidi ya wapinzani hasa CHADEMA. A really murderous-ready regime when it comes to combatting dissent.

Halafu ukijumlisha na propaganda za kuwanasibisha wakosoaji/wapinzani na wasaliti. Na pia kuwalinganisha wanasiasa wote kama wasaka madaraka, pesa na waroho; kwamba wote ovyo tu: CCM=upinzani (CHADEMA) - hivyo afadhali CCM mnayoijua (Kazı wewe unayofanya hapa.), Watanzania wanaingia mashaka makubwa na kukosa guts za kujitoa muhanga kupigania haki zao.

Uoga+mashaka sio kukubali status quo. Certainly, the brink end point will soon be reached. Natarajia sitakuwepo. Tutaanza kushuhudia civil wars kama za Ethiopia, Sudan, Somalia. Sasa hivi CCM wana-enjoy kipindi cha bliss ya ubabe (dominance). Hawajali kufanya siasa za brinkmanship. Ila wajue kuwa vizazi vinabadilika. Hizo kauli za kuwasemea wananchi kuwa wanalikubali zimwi walijualo ipo siku zitafika mwisho na moto utawaka.
 
You'r 100% correct kwamba ipo time raia hawataweza ku-tolerate tena maana kila chenye mwanzo hakikosi mwisho.
Na kila tukio na zama zake itafika zama watu wataweza kuandama bila hata wapinzani kuwashawishi kwa kutumia nguvu kubwa, CCM inabidi walione hili mapema na waje na mbinu mbadala otherwise they make a timing bomb for themselves.
 
Maoni yako yapo sahihi, ila kuna shida mahala.

Makonda kafanya kazi yake nzuri ya kafumua uozo uliopo dhahiri serikalini kwa sasa, lakini hana 'mandate' ya kuwajibisha!

Tatizo linalofuata na litalokuja kwa Samia ni misimamo yake ya kukumbatia wahalifu.

Tangu aingie madarakani ushamuona kuchukua hatua yoyote ya maana kuwawajibisha viongozi mabaradhuli hata siku moja?

Makonda atamaliza ziara zake na kufumua uozo na kuuweka hadharani lakini hakuna hatua zozote za maana atazoweza kuzichukua Rais Samia zaidi ya panga pangua kwa uhamisho.

Kutokuchukua kwake hatua kwa uozo uliodhihirika wazi namna hiyo kutawafanya waTz wasimwamini tena kwa slogan yake yoyote mpya atayokuja nayo siku za mbeleni na hataweza kuuzika kwa mbinu yoyote kwa waTz walalahoi.

Na kwa hatua hiyo ya Rais kufumbia macho wahalifu wa wazi na wa kiuwajibikaji, Makonda atakuwa katengenezewa zengwe kubwa sana na maadui wa kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…