Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
Mbona kwa sasa kama mnafanya kampeni peke yenu na mnajipima kwa kutoa max wenyewe?Uchaguzi wa 2025, hakuna mchuano wowote kwa Rais Samia kwasababu kwa utaratibu wa CCM, 2025 Samia anapita kwa mserereko, inatolewa fomu moja tuu ya Samia!. Ila inaweza kutokea Samia asigombee kwasababu HII them bado Samia atachukua fomu yake na kumpa mtu atakaye mtaka!.
P
Mna haha bure wakati wengine hawajaweka madhaifu yenu hadharani?
1. Hivi CCM inategemea kupata kura zozote kutoka kwa vijana waliomaliza masomo 2015 hadi leo? Hawa ambao wamekosa ajira, mitaji ya kibiashara wala support yeyote? Mmejiuliza ni % ngapi ya wapiga kura?
2. Watumishi wa umma waliopo kwenye ajira (zisizo na mianya ya wizi) na wastaafu ambao hatima za pension zao zimeminywa mnategemea kura zao?
3. Boda na wamachinga hao mnaoona wanawasindikiza kwa mbwembwe mkiwapa mafuta na incentives mnadhani ni wenu hao? Ni % ya wapiga kura?
Sasa ngoja hizo kampeni zikianza wapinzani watakapo weka uchafu wote mezani kama wananchi hawaja watapika. Ushindi wa CCM na huyo mama yenu unategemea kupora uchaguzi kama 2020 ndio maana tume huru hamuitaki wala katiba mpya.
Ila nadhani safari hii yale ya 2020 yakifanyika ni sawa na kuonja sumu, [emoji879]
Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app