Pre GE2025 Paul Makonda ni Karata ya muhimu kwa Rais Samia kuelekea uchaguzi wa 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mimi mchango wangu ni huu.. at least nimewasanau wadau kuwa some politicians are using the so called "KATIBA MPYA" for their parsonal interest.
Ijapokuwa sipingi kuwa kuna umuhimu wa katiba mpya ila kuna udhaifu mkubwa katika kuidai.
Ndiyo unatakiwa uwe msitari wa mbele kuitadai
 
Habari wanajamvi!

Kwa anayefuatilia siasa za Tanzania atakubaliana na mimi kuwa kwa sasa Mh. Paul Makonda Katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndiye anayetamba katika anga za Kisiasa hapa nchini, Ujio wake umekuwa wa kishindo sana na hii ni karata muhimu kwa Rais Samia kuelekea mbio za uchaguzi wa 2025 nitaelezea kwa ufupi kwanini makonda ni karata ya muhimu kwa Rais Samia.

Tufahamu kuwa kipindi cha Hayati Dr. Magufuli alianzisha siasa zilizojulikana kama siasa za kutetea wanyonge na kupitia mbinu hii alifanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90% kuteka nyoyo na akili za watanzania hasa wa tabaka la chini ambao walikuwa wakifurahishwa na jinsi Dr. Magulfuli alivyokuwa akiwawajibisha viongozi.

Baada ya Rais Samia kupokea kijiti cha Urais aina ya siasa za Hayati Magufuli zilionekana kupotea na kundi kubwa la watu wa tabaka la chini halikupenda viongoizi wanapokosea kutowajibishwa na hii ilipelekea taratibu Rais Samia kuanza kupoteza mvuto hasa kwa raia wa hili tabaka la chini.
Inaonekana Samia alipewa ushauri wa kumrudisha Makonda kuwa active kwenye siasa tena ndani ya chama na akaukubali kwani Makonda anaziweza siasa za Hayati Dr. Magufuli na hivyo lile kundi kubwa la watu lililopoteza imani na serikali ya Dr. Samia taratibu litaanza kurudisha imani kwa serikali na hili linajidhihirishakupitia mikutano ya Mh. Makonda inayoendelea Tanzania. Hapa ni kusema kuwa ujio wa Mh. Makonda ni wa kimkakati Zaidi.

Niseme tu kama Mh. Samia kaamua kutumia karata hii ya makonda ni wazi kuwa timu Magufuli bado walikuwa na nguvu ndani ya chama na hivyo haikuwa sahihi kuwaapuuza lakini hii ni ishara huenda kufikia 2025 wengi katika wanasiasa wenye mrengo wa Hayati Dr. Magufuli wakarudishwa kundini ili kumsaidia Rais Samia katika kampeni za 2025, Ingawaje inaonekana mchuano utakuwa mkali sana ndani ya chama kwani kuna loophole nyingi sana zinazoweza kutumika kumuweka mgombea mwingine tofauti na Samia.

Hii inaitwa kujitekenya na kucheka mwenyewe, hiyo inayoitwa mbinu ya Magufuli ilikuwa ni hadaa tu ndio maana aliishia kupora uchaguzi. Kama kweli mbinu ile iliteka wanyonge tungeona uchaguzi wenye unafuu wangalau kwa ile demokrasia iliyokuwa wakati wakati wa JK.

Hayo mafuriko ya Makonda na hata Yale ya enzi za Magufuli yalikuwa yanachagizwa na nguvu ya Dola, Wala sio ridhaa ya wananchi walio wengi. Karata halisi ya Samia na ccm ni katiba hii mbovu na tume hii ya uchaguzi, na ndio maana ccm hawako tayari kwa katiba mpya Wala tume huru ya uchaguzi.
 
Habari wanajamvi!

Kwa anayefuatilia siasa za Tanzania atakubaliana na mimi kuwa kwa sasa Mh. Paul Makonda Katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndiye anayetamba katika anga za Kisiasa hapa nchini, Ujio wake umekuwa wa kishindo sana na hii ni karata muhimu kwa Rais Samia kuelekea mbio za uchaguzi wa 2025 nitaelezea kwa ufupi kwanini makonda ni karata ya muhimu kwa Rais Samia.

Tufahamu kuwa kipindi cha Hayati Dr. Magufuli alianzisha siasa zilizojulikana kama siasa za kutetea wanyonge na kupitia mbinu hii alifanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90% kuteka nyoyo na akili za watanzania hasa wa tabaka la chini ambao walikuwa wakifurahishwa na jinsi Dr. Magulfuli alivyokuwa akiwawajibisha viongozi.

Baada ya Rais Samia kupokea kijiti cha Urais aina ya siasa za Hayati Magufuli zilionekana kupotea na kundi kubwa la watu wa tabaka la chini halikupenda viongoizi wanapokosea kutowajibishwa na hii ilipelekea taratibu Rais Samia kuanza kupoteza mvuto hasa kwa raia wa hili tabaka la chini.
Inaonekana Samia alipewa ushauri wa kumrudisha Makonda kuwa active kwenye siasa tena ndani ya chama na akaukubali kwani Makonda anaziweza siasa za Hayati Dr. Magufuli na hivyo lile kundi kubwa la watu lililopoteza imani na serikali ya Dr. Samia taratibu litaanza kurudisha imani kwa serikali na hili linajidhihirishakupitia mikutano ya Mh. Makonda inayoendelea Tanzania. Hapa ni kusema kuwa ujio wa Mh. Makonda ni wa kimkakati Zaidi.

Niseme tu kama Mh. Samia kaamua kutumia karata hii ya makonda ni wazi kuwa timu Magufuli bado walikuwa na nguvu ndani ya chama na hivyo haikuwa sahihi kuwaapuuza lakini hii ni ishara huenda kufikia 2025 wengi katika wanasiasa wenye mrengo wa Hayati Dr. Magufuli wakarudishwa kundini ili kumsaidia Rais Samia katika kampeni za 2025, Ingawaje inaonekana mchuano utakuwa mkali sana ndani ya chama kwani kuna loophole nyingi sana zinazoweza kutumika kumuweka mgombea mwingine tofauti na Samia.
Na amempa heshima na itifaki yenye hadhi ya karata dume.

Kama alivyokuwa anaogopwa na Viongozi wa awamu ya 5 kutoa Rais hata Sasa anaogopwa na Viongozi kutoa Rais.
 
Mkuu usisahau kuna loopholes nyingi zinaweza tumika kuhalalisha kuvunjwa kwa utaratibu wa ka mserereko uliozoeleka.
Kwani Samia hakushindanishwa na wala hakuchukua form ya urais ila ameupata kwa bahati baada ya mapenzi ya Mungu kutimia.
Hivyo 2025 mpira unaanza 0 - 0 japo kuwa Samia Ana nafasi kubwa ya kubadili matokeo maana kwa sasa yeye ndie mwenye kadi zote nyekundu na njano na ameanza kuzitumia vizuri maana anajua ugumu wa mechi.
Nimependa hapo kwenye loopholes.. Hebu atokee basi mgombea mwingine tupumzishwe na Kizimkazi..
 
Haya maigizo kwa mtu mwenye akili timamu ataona kuwa yanaivua nguo CCM na Serikali yake tu na kumjenga Makonda yeye binafsi. Uozo unaoibuliwa kwenye ziara za Makonda ni kielelezo cha kushindwa kwa Serikali kuwatumikia wananchi. Hawa wanaolalamikiwa yaani wakurugenzi,wakuu wa wilaya na mikoa wote ni makada wa CCM na ni wateule wa Rais. Ina maana Rais na vyombo vyake amewashindwa wateule wake ndiyo Makonda atawaweza? Watu wanashangilia wateule hao kujambishwa na Makonda lakini hayo yote yanaishia hapo hapo jukwaani akishapita ni business as usual. WAJINGA NDIYO WALIWAO.
 
Uchaguzi wa 2025, hakuna mchuano wowote kwa Rais Samia kwasababu kwa utaratibu wa CCM, 2025 Samia anapita kwa mserereko, inatolewa fomu moja tuu ya Samia!. Ila inaweza kutokea Samia asigombee kwasababu HII them bado Samia atachukua fomu yake na kumpa mtu atakaye mtaka!.
P
Na kwa mfano Samia mwenyewe akisikia sauti ya YEYE na akaamua kuitii nini kitatokea?(Picha imejitundika kwa bahati mbaya)
photo_2021-08-11_09-06-26.jpg
 
Nimependa hapo kwenye loopholes.. Hebu atokee basi mgombea mwingine tupumzishwe na Kizimkazi..
Loopholes zitatumika vizuri tu mkuu ila inategemea na nguvu ya Samia ndani ya chama kama itakuwa ndogo then its over!
Tukumbuke kuwa kuna ma- beast yapo inactive kwa sasa ila watakuwa activated soon kuja kubadilisha upepo wa 2025.
 
Haya maigizo kwa mtu mwenye akili timamu ataona kuwa yanaivua nguo CCM na Serikali yake tu na kumjenga Makonda yeye binafsi. Uozo unaoibuliwa kwenye ziara za Makonda ni kielelezo cha kushindwa kwa Serikali kuwatumikia wananchi. Hawa wanaolalamikiwa yaani wakurugenzi,wakuu wa wilaya na mikoa wote ni makada wa CCM na ni wateule wa Rais. Ina maana Rais na vyombo vyake amewashindwa wateule wake ndiyo Makonda atawaweza? Watu wanashangilia wateule hao kujambishwa na Makonda lakini hayo yote yanaishia hapo hapo jukwaani akishapita ni business as usual. WAJINGA NDIYO WALIWAO.
Ujue kwa mambo yalivyo sasa ni wazi kuwa Samia kalemewa na huu mzigo wa Urais na amepoteza imani kwa wananchi hivyo best option iliyokuwepo ni kumtumia Makonda ambaye kwa kiasi anaweza kujitoa ufahamu na kuwatandika vitasa hata CCM wenzake. Yote hii Samia anafanya ni Trial & error kuona njia gani itakuwa sahihi ili aaminike na watanzania.
 
Hili linaweza kutokea pia mkuu.!
Hili lipo ila linafichwa ili kuepusha mtafaruku kwa akina Lameck na Marope na wengineo. Gazeti la Uhuru ni mouthpiece ya CCM ,chapisho lile halikutoka kwa bahati mbaya, it was well calculated, hata kukanushwa ilikuwa mbinu tu ya kuweka pazia kwa kinachoendelea.
 
Na amempa heshima na itifaki yenye hadhi ya karata dume.

Kama alivyokuwa anaogopwa na Viongozi wa awamu ya 5 kutoa Rais hata Sasa anaogopwa na Viongozi kutoa Rais.
Inaonekana jamaa ana kitu cha ziada tofauti na tunavyomuona maana kuna kundi kubwa ndani ya chama halipendi jinsi Makonda anavyoendesha mambo ila ndio hivyo hawana cha kumfanya.
 
Ujue kwa mambo yalivyo sasa ni wazi kuwa Samia kalemewa na huu mzigo wa Urais na amepoteza imani kwa wananchi hivyo best option iliyokuwepo ni kumtumia Makonda ambaye kwa kiasi anaweza kujitoa ufahamu na kuwatandika vitasa hata CCM wenzake. Yote hii Samia anafanya ni Trial & error kuona njia gani itakuwa sahihi ili aaminike na watanzania.
You are correct. Ila kwa kinachoendelea nafikiri Bimkubwa anajuta, hakujua kuwa itakuwa hivi.
 
Inaonekana jamaa ana kitu cha ziada tofauti na tunavyomuona maana kuna kundi kubwa ndani ya chama halipendi jinsi Makonda anavyoendesha mambo ila ndio hivyo hawana cha kumfanya.
Marais wanaomkubali,hao wengine wasipompenda haimuhusu Makonda watajuana wao Kwa wao,ndio maana kapewa ulinzi na Wasaidizi
 
Habari wanajamvi!

Kwa anayefuatilia siasa za Tanzania atakubaliana na mimi kuwa kwa sasa Mh. Paul Makonda Katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndiye anayetamba katika anga za Kisiasa hapa nchini, Ujio wake umekuwa wa kishindo sana na hii ni karata muhimu kwa Rais Samia kuelekea mbio za uchaguzi wa 2025 nitaelezea kwa ufupi kwanini makonda ni karata ya muhimu kwa Rais Samia.

Tufahamu kuwa kipindi cha Hayati Dr. Magufuli alianzisha siasa zilizojulikana kama siasa za kutetea wanyonge na kupitia mbinu hii alifanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90% kuteka nyoyo na akili za watanzania hasa wa tabaka la chini ambao walikuwa wakifurahishwa na jinsi Dr. Magulfuli alivyokuwa akiwawajibisha viongozi.

Baada ya Rais Samia kupokea kijiti cha Urais aina ya siasa za Hayati Magufuli zilionekana kupotea na kundi kubwa la watu wa tabaka la chini halikupenda viongoizi wanapokosea kutowajibishwa na hii ilipelekea taratibu Rais Samia kuanza kupoteza mvuto hasa kwa raia wa hili tabaka la chini.
Inaonekana Samia alipewa ushauri wa kumrudisha Makonda kuwa active kwenye siasa tena ndani ya chama na akaukubali kwani Makonda anaziweza siasa za Hayati Dr. Magufuli na hivyo lile kundi kubwa la watu lililopoteza imani na serikali ya Dr. Samia taratibu litaanza kurudisha imani kwa serikali na hili linajidhihirishakupitia mikutano ya Mh. Makonda inayoendelea Tanzania. Hapa ni kusema kuwa ujio wa Mh. Makonda ni wa kimkakati Zaidi.

Niseme tu kama Mh. Samia kaamua kutumia karata hii ya makonda ni wazi kuwa timu Magufuli bado walikuwa na nguvu ndani ya chama na hivyo haikuwa sahihi kuwaapuuza lakini hii ni ishara huenda kufikia 2025 wengi katika wanasiasa wenye mrengo wa Hayati Dr. Magufuli wakarudishwa kundini ili kumsaidia Rais Samia katika kampeni za 2025, Ingawaje inaonekana mchuano utakuwa mkali sana ndani ya chama kwani kuna loophole nyingi sana zinazoweza kutumika kumuweka mgombea mwingine tofauti na Samia.
People talk to people not at people!
 
Makonda anakuwa na mvuto kwenye chama na siasa ktk nchi kuliko Mama. Watu wanaona ni kama nusu Magu. 2025 bora agombee yeye na mama apumzike. Raisi mpya wa Namibia (aliyeapishwa baada ya kifo cha raisi mchaguliwa) asema hana mpango wa kugombea uraisi.
 
Back
Top Bottom