Sijawahi mkubali na bado simkubali Paul Makonda. Lakini hilo haliondoi ukweli kuwa aina ya siasa anazofanya ndizo zinazopendwa na wananchi. Siasa za kuikimbiza serikali(Watumishi wa serikali) na kupazia sauti matatizo ya wananchi. Wazee wengi wa CCM wanasiasa za zamani. Siasa za ulaghai laghai huku wakiplay safe. Hawataki kuzua Taharuki. Siasa za kuongea wasiyomaanisha na kisha kurudi kwao wakiwa wameingiza siku. Siasa na porojo za kuishia majukwaani.
Aina ya siasa za Makonda ni za kuzua taharuki. Za kuamsha watu. Za mchakamchaka kama zilivyokuwa za Magufuli.
Mkubali Makonda au usimkubali lakini aina yake ya siasa ndiyo inayoeleweka kwa wananchi kwa sasa. Siasa za Wazee kama Nchimbi na Makalla, siasa za porojo bila kugusa wananchi zimepitwa na wakati.