Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again


Nimesoma comment hiyo huko Instagram nikashtuka sana.

Haiba ya Paul Makonda inalingana sana na ya Adolf Hitler, fuhrer wa dola la Ujerumani baada ya WWI

Kwa mantiki hiyo si ajabu wataalamu wa kuchunguza mienendo na tabia za viongozi wenye traits za ukatili duniani, kutoka Serikali ya Marekani waliona Makonda siyo kiumbe wa kuedekeza, wakampiga pin mapema asitie mguu kwenye ardhi yao bali abaki kuwa tatizo letu Tanzania.

Kabla ya kuanza vurugu zake, Adolf Hitler alipenda sana kujionesha kuwa ni mcha Mungu na hotuba zake nyingi alimalizia kwa kuapa kwa Jina la Baba, na la Mwana, na Roho Mtakatifu....viongozi wengi wa dini wakaingia kwenye mfumo baadaye walikiona cha mtema kuni...mfano mzuri ni Martin Niemoller.

Hitler aliwafanya Wajerumani waamini kwamba yeye peke yake ndiye mwenye suluhu ya maisha magumu kufuatia baada ya WW I.

Alibeba kisasi moyoni mwake, akatafuta jamii ya kuilaumu baada ya vita hiyo, akaelekeza lawama zake kwa Wayahudi na Wakomunisti.

Makuzi ya Makonda na ya Hitler hayatofautiani sana, wote ni watu ambao hawakuwa na uwezo wowote shuleni lkn wamejaliwa vipaji vya kuhamasisha Umma. Kwa maana hii Makonda anatumia kila fursa ndogo kiasi gani, hata shughuli zisizo na maana kujionesha kuwa yeye ni Messiah, wakati mwingine akijisahau kabisa kuwa kuna viongozi wake wakuu wa Kitaifa.

Hoja yangu:
Wote tunaolitakia mema Taifa letu, tusimdekeze huyu kiumbe, kuna siku matukio ya kitaifa yasiyotabirika yanaweza kumpropel tukajikuta ni kiongozi mkuu wa kitaifa na hapo ndipo tutalimia meno kama mentor wale Magufuli alivyojaribu kutulimisha.

Niwapongeze CCM angalau kwa kumwondoa huko kwenye Uongozi wa Kitaifa.

Huyu hapo alipofikia inabidi iwe mwisho wake asipande zaidi ya nafasi hiyo, tutakuja kulia kilio cha kusaga meno, he is a thug.
 
Hoja ya kijinga kabisa..

Kwako wewe Marekani ndiyo wana standard ya kudefine tabia na mwenendo wa mtu...?

Wakati wanaivamia Iraq kwa kisingizio inamiliki siraha za maangamizi ulikua hujazaliwa?

Makonda anaweza kuwa mbaya ila sio kama mnavyomwelezea...

Mnajaribu kutuaminisha vitu ambavyo havipo kabisa, utazani sisi ni wageni Tanzania...

Character assassination hufaulu ilisindikizwa na ushahidi usio shaka.
 
Nyinyi majizi huwa hamkosi wasiwasi, Acheni wizi muone kama mtakuwa na haja ya kuwachukia wanasiasa dizaini ya kina hayati JPM na kina makonda
 
Makonda amefanya maovu yafuatayo:-
1. Alimteka Mo.
2. Alivamia kituo cha cloudstv.
3. Alimpiga risasi Lisu.
4. Alimpoteza Ben Sa8.
5. Alowapora pesa wafanyabiashara wa DSM.

Unataka mpk akuue wewe ndipo ujue kuwa ni muovu??
 
3. Alimpiga risasi Lisu.
4. Alimpoteza Ben Sa8.
5. Alowapora pesa wafanyabiashara wa DSM.
Weka ushahidi hapa

Kwa tuhuma hizi unataka kutuaminisha wewe una Intelligence kubwa kuzidi waliomteua?

Au wanajua na wamemwogopa Makonda?

Au unatuaminisha kwamba walimtuma?
 
Nchi hii hapa ilipofikia inahitaji mtu kama Hitler au Carl Peter awanyooshe waswahili kama mleta mada.
 
Makonda amefanya maovu yafuatayo:-
1. Alimteka Mo.
2. Alivamia kituo cha cloudstv.
3. Alimpiga risasi Lisu.
4. Alimpoteza Ben Sa8.
5. Alowapora pesa wafanyabiashara wa DSM.

Unataka mpk akuue wewe ndipo ujue kuwa ni muovu??
Hivi ww ni mtakatifu sana mbona unahesabu mabaya tu🥶Kwamba makonda hana mema hivi umeangalia Arusha watu wazima wazee wanalia na kushukuru japo sasa wamepata mtu wa kumweleza shida zao harafu mpuuzi km ww ulie shiba mali za wizi na dhuruma utampendaje Makonda . ila kuna siku mtazitapika tu hizo hela za dhuluma washenzi nyie
 
MAKONDA BOMAYEEEEE
 
Makonda amefanya maovu yafuatayo:-
1. Alimteka Mo.
2. Alivamia kituo cha cloudstv.
3. Alimpiga risasi Lisu.
4. Alimpoteza Ben Sa8.
5. Alowapora pesa wafanyabiashara wa DSM.

Unataka mpk akuue wewe ndipo ujue kuwa ni muovu??
MAKONDA BOMAYEEEE.........NA WAVIMBE WAPASUKE
 
Mtoa mada uliliwa kiboga na makonda
una chuki kubwa mno na mtu ambaye pengine anakuzidi Kila kitu.

Kama wewe ni mjuaji jitokeze hadharani useme haya uliyo andika
 
Hitler hakuwatesa wajerumani
Hitler aliipambania ujerumani yake
Nyakati za Hitler dunia Ilikuwa kwenye dimbwi la ukatili, (vita, utumwa, unyonyaji, unyanyasaji na ukoloni)dhidi ya walimwengu, hivyo Hitler alikuwa anafuata mkondo tu
Hitler angelikuwa Rais wa ulimwengu wa Leo asingekuwa yule unayemjua, angekuwa Raisi mchapakazi, mjenzi wa uchumi imara, mkatili kwa Watumishi wa hovyohovyo Kama JPM

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Umeandika mistari mingi ambayo haina maana sana,mm nadhani usingetangulia kumlaumu Mdogo wangu Paulo Makonda ila ungejikita kuona kile ambacho makonda anakisimamia na ungejua ni kwa jinsi gani mamlaka nyingi Tanzania hazitoi huduma kabisa kwa wananchi na ungejua kwa nn wananchi wengi wamekaa kimya lkn mioyoni mwao wana maumivu makali ya kukosa haki,kudhulumiwa na wenye kiburi cha pesa ktk Tanzania.Ninachokiona kwako na maandishi yako ni kwamba ww kuna mtu amekufundisha kumchukia makonda tu bila kujali anachokifanya kwa wananchi maskini wanaoonewa.
 
Watu wa dizain ya mleta mada ni wa kutandika viboko tu kwa sababu anaonyesha wazi anatoka kundi la wezi tu.
 
Reactions: Tui
Tatizo la watu aina ya Makonda Magu ni kuwakumbatia watu wa kipato cha chini na kuaminisha jamii kua wanaowapinga ni majizi, matapeli na mafisadi. Ajabu iliyoje watu huwaamini kabisa kabisa aisee.

Ukiongozwa na watu wa hivyo tegemea kutokua na reasoning yoyote kwa wanaoongozwa nae.
 
Kinachomuangusha Makonda ni kisasi amebeba visasi na shida vinampofua utendaji wake

Unakuwa na maigizo mengi kuliko uhalisia kujaribu kutengeneza picha yake iliyqchafuliwa msimu ule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…